Njia 11 za asili Kuondoa maumivu ya Ngiri
Ngiri au Hernia huelezewa kama kiungo kilicho umuka/kuvimba au tishu ya fati kwenye eneo laini au dhaifu kwenye mwili. Kuna aina kadhaa tofauti tofauti na baadhi ni maarufu kuliko nyengine. Ngiri yaweza kuwa na maumivu makali mno na hata mtu ikampelekea kufa. Wakati matibabu ya madawa yanashauriwa kwa nguvu, Kuna baadhi ya tiba asili ambazo zinaweza kushusha au kuondoa shida za ngiri. Tiba hizi zaweza kujumuisha matumizi ya vipande vya barafu, tangawizi, massage, aloe vera, unga wa pilipili manga, na mafuta ya mnyonyo, vile vile mabadiliko ya mfumo wa maisha kama kupunguza uzito, mabadiliko ya ulaji wa chakula, na mazoezi.
Kulingana MedlinePlus, Ngiri huweza kujitokeza kupitia eneo dhaifu lililozungukwa na misuli au kuta za tishu.Yaweza kuonekana kama uvimbe chini ya ngozi. Ugonjwa huu kawaida huonekana maeneo chini ya kitovu, lakini pia unaweza kuonekana juu ya paja, kitovuni, na kwenye mpaka kati ya paja na kinena (groins). Wakati kukimbilia hospital kwa matibabu kunashauriwa zaidi pale tu ngiri imetambulika, matibabu kadhaa ya nyumbani yamejizolea umaarufu kwa kuleta tumaini la kutibu ngiri (hernia), pia vile vile mabadiliko ya aina fulani ya mfumo wa maisha ambayo yanaweza kupunguza hatari ya muendelezo wa hernia. [1]
Njia Asilia za Kushusha Maumivu ya Ngiri/Hernia
Matibabu ya nyumbani ya Ngiri ni kama yafuatayo:
Mafuta ya Mbegu za Mnyonyo
Kupitia historia, mafuta ya mbegu za mnyonyo zimekuwa zikitumika kwa upana juu ya mambo yanayohusu afya ya tumbo, kwani yanaweza kufunika tumbo kwa kuta nyembamba, kwa maana hiyo huzuia uvimbe na kuchangia umeng'enyaji wa chakula unaofaa. Unaweza kuandaa kimfuko Cha mafuta ya mbegu za mnyonyo na kuweka juu ya tumbo kupoozesha maumivu ya ngiri.
Aloe Vera Juice
Kama ni kampaundi ya asili ya kupingana na uvimbe na wakala wa kuleta utulivu, aloe vera mara nyingi hushauriwa kwa watu wenye Ngiri/Hernia. Aloe vera inaweza kuliwa Kila asubuhi kwenye mfumo wa juisi/sharubati. Kwa matokeo mazuri, inaweza kuliwa kabla ya kila mlo, kuondoa uwezekano wa ngiri kujitokeza. [3]
Mfuko wa barafu
Kipindi unasumbuliwa na ngiri, mara nyingi kunatokea uvimbe, damu kuvilia, na maumivu maeneo chini ya kitovu au groin. Yawezekana isiwe tiba rahisi kwako, kuweka mfuko wenye barafu moja kwa moja mahali palipo athirika kunaweza kusababisha kusinyaa na kupunguza uvimbe kwenye mwili, mara hupunguza maumivu na kuumuka kwake. [4]
Tangawizi
Inapokuja kesi ya kushusha maumivu chini ya kitovu na kuondoa matatizo ya uvimbe,vitu vichache hufanya kazi vyema kama tangawizi. Unaweza kuitumia dawa hii kwenye hali ya kimiminika kama juisi ya tangawizi, au kula tangawizi mbichi kuamsha tumbo lako na pengine kuondoa maumivu kwa kiasi kikubwa. Inaweza kulinda tumbo na umio (oesophagus) dhidi ya uwepo wa asidi, ambayo huweza tokea kwa kesi ya ngiri. Unaweza pia kunywa chai ya tangawizi na kuondoa maumivu na uvimbe. [5]
Licorice
Ngiri inaweza kusababisha uharibifu kwenye kuta za tumbo na njia ya chakula esophagus, na licorice imekuwa ikijulikana kwa kipindi kirefu kama kichocheo ponyo kwenye maeneo haya ya mwili. Kutumia chai ya licorice kunaweza kunaweza kuchochea kwa haraka kuhuisha tishu zilizoharibika na pia inaweza kuondoa maumivu na uvimbe kadri unavyozidi kutumia, kutokana na sifa zake za kutuliza maumivu. [6]
Lose Weight
Utapia mlo ni sababu hatarishi kwa wagonjwa wa ngiri, na inaweza kuzorotesha uponyaji. Kama ukipunguza uzito, mwili wako utakuwa chini ya mkazo (physical strain), kimo chako kitaimarika, na dalili zitapotea kiasili. Unatakiwa pia kula milo midogo, kwani itaweka presha ndogo tumboni na kwenye puru. [7]
Badilisha mlo wako
Kuna aina ya vyakula maalumu unatakiwa kuviepuka kama unatamani kuzuia au kutibu ngiri. Vyakula vyenye pilipili na vyenye asidi na vile vigumu kumeng'enywa vinatakiwa kuepukwa kama unavyo tayari au una mpango wa kula. Vyakula hivi huunguza kuta za tumbo zaidi, kutia ugumu zaidi kupona. [8]
Unga wa Pilipili Manga
Unga wa pilipili manga ni muhimu zaidi ya kuleta ladha kwenye chakula. Pilipili manga imekuwa ikihusishwa na kutibu matatizo ya tumbo na kuzuia uvimbe kwenye tumbo. Pia inaweza kudhibiti kiungulia na kuponyesha maeneo kwenye mwili ambayo yameshaharika kipindi kiungo kinaanza kusukuma kupitia kuta yenye uwazi. [9]
Punguza Msongo wa Mawazo
Sababu kubwa ya uwepo wa ngiri ni msongo wa mawazo na wasiwasi. Homoni za msongo uliokithiri zinaweza kudhoofisha viungo vya mwili na kwa urahisi kuweza kutia mgandamizo zaidi juu ya kazi za kimetaboliki kiujumla. Magonjwa ya tumbo na kiungulia yanaweza kuathiriwa na msongo wa mawazo, ambayo yanaweza kuongeza hatari ya kupata ngiri. Shughuli kubwa za kupunguza msongo wa mawazo zinaweza kuwa meditation, yoga, acupuncture, massages, vile vile matumizi ya mafuta tete (essential ois) na aromatherapy. [10]
Kuacha Mazoezi
Moja ya sababu kubwa ya ngiri ni mazoezi mazito au kujikamua kipindi unanyanyua vyuma vizito (weights) . Kama umewahi kupata ngiri siku za nyuma au una kawaida ya kujihusisha na mazoezi mazito, acha na fanya mazoezi mepesi kipindi unatarajia kupona, au kama njia ya kujizuia na ngiri. Mgandamizo unaohusika kwenye mazoezi unaweza kuwa sawa na mgandamizo kipindi chakula kinasafiri kwenye njia yake (bowel movements), ambayo nayo pia huweza kusababisha ngiri, kwa hiyo hakikisha unakunywa vimiminika vya kutosha na kula fiber za kutosha. [11]
Juisi ya Mboga za majani
Yawezekana, moja ya tiba rahisi na yenye uhakika kwa ngiri ni inaweza kuwa ni glasi ya juisi ya mboga mboga, hasa ambayo imeandaliwa na karoti, spinach, vitunguu, broccoli, na kale. Virutubisho vilivyosheheni na sifa ya asili ya kupinga uvimbe ya mboga za majani inaweza kuponyesha maumivu makali ya dalili za ngiri. Ongezo la chumvi kidogo kwenye juisi ya mboga za majani Inaweza kuwa namna nzuri ya kuimarisha athari zake. [12]
Neno la Tahadhari: Kama ngiri sugu haikutibika kwa upasuaji uliokamilika, mara zote kunakuwa na matatizo zaidi au hata kifo. Kama unahisi maumivu ya ngiri, inashauriwa kumuona daktari mapema uwezavyo. Matibabu haya ya nyumbani yawe kama nyongezea tu kwenye kesi nyingi za ngiri.
Kwa ushauri na tiba asilia
Tabibu Kweli
Tanzania 🇹🇿
Call: 0766107722
Whatsapp: 0658674553
Maoni
Chapisha Maoni