Asili yake ni nchi za Asia kama vile Indonesia, India, Pakistan, na hata maeneo ya nchi za Afrika Mashariki kama Zanzibar, karafuu ni kiungo kinachotoa faida nyingi za kiafya. Faida hizi zikiwemo kusaidia kwenye mmeng'enyo wa chakula, kuimarisha mfumo wa kinga mwilini, na kudhibiti ugonjwa wa kisukari. Karafuu pia ina sifa ya kuzuia visababishi vya kansa (anti-mutagenic properties) na kuzuia visababishi vya magonjwa yaletwayo na bacteria (anti-microbial properties), sambamba na kupambana na magonjwa ya kinywa na maumivu ya kichwa na pia hufikiriwa kuwa na sifa za kuongeza hamu ya tendo la ndoa (aphrodisiac properties).
Karafuu ni nini?
Karafuu ni kiungo maarufu kinachotumika duniani kote, haswa bara la Asia; Karafuu hutengeneza msingi wa mapishi kwenye nyingi za Asia.
Karafuu ni kikonyo kilichokauka cha ua kutoka kwenye mti wa mkarafuu, kwa jina la kitaalamu huitwa Syzygium aromaticum. Mti huu upo kwenye familia ya miti iitwayo Myrtaceae. [1] Ni mti wenye chanikiwiti muda wote unaokua vizuri kwenye hali ya ukanda wa kitropiki. Karafuu ni dawa ya asili ambapo watu hutumia sehemu tofauti ya mti wa wake, ikiwemo kikonyo kilichokauka, shina, na majani na kutengeneza dawa. Mafuta ya karafuu ni maarufu kwa sifa zake za enzi kwa kutibu.
Karafuu, kama viungo vingine vingi vimetokea bara la Asia, ina stori kubwa nyuma yake. [2] Kipindi cha karne ya 13 na 14, Karafuu ilisafirishwa kutokea Indonesia hadi China, India, Persia, Africa, na Ulaya. Kipindi hiki chote, karafuu zilikuwa zinauzwa kwa bei ya juu sana, na ndo maana vita dhidi ya umiliki wa karafuu ikaanza. Vita nyingi zilipiganwa ili kutaka kumiliki visiwa vya Maluku kipindi chote cha kale na zama za sasa. Waholanzi waliibuka washindi na kumiliki visiwa vya Maluku kwa kipindi kirefu. Leo hii, Karafuu ni zao la biashara muhimu mno duniani kote.
Matumizi ya Karafuu
Karafuu imekuwa ikitumika kwa maelfu ya miaka nchini India na China si kama kiungo na kiongeza ladha kwenye chakula lakini pia kama dawa kwa matatizo mengi. [3]
- Tiba za kijadi za kihindi za kale (Ayurvedic) zilitumia karafuu kutibu meno yaliyoharibika kuondoa harufu mbaya kinywani.
- Kwenye madawa ya Kichina, karafuu hufikiriwa kuwa na sifa za kuongeza hamu ya tendo la ndoa.
- Chai ya karafuu ni kinwaji maarufu kwa kutibu tatizo la kutopata choo.
- Mafuta ya karafuu hufikiriwa kusaidia kutibu maumivu ya kichwa, kujaa kwa gesi, vilevile kupunguza alama za mikunjo.
- Pia hutumiwa kufukuzia wadudu. Weka matone kiasi ya mafuta ya karafuu kwenye maji halafu tazama watakavyopotea!
Ukweli wa Virutubisho vya Karafuu
Kulingana na USDA [5] National Nutrient Database, virutubisho vilivyomo kwenye karafuu ni carbohydrates, protein, nishati, na nyuzi lishe (dietary fiber). Madini yanayopatikana ni potassium, sodium, na magnesium. Vitamini zinazopatikana ni vitamin E, folate, na niacin. Karafuu pia zina phosphorus, madini joto(iron), zinc, vitamim C, thiamin, riboflavin, na vitani A na K. Ukiangalia kiasi kidogo cha karafuu kinachotumika kwenye misosi mingi majumbani, wakati karafuu zina virutubisho vingi, hutakiwi kuacha kutumia kwa wingi.
Faida za kiafya za Karafuu
Faida za kiafya za Karafuu ni:
Mmeng'enyo Bora
Karafuu zinaweza kuimarisha mmeng'enyo kwa kuamsha uzalishwaji wa vimeng'enyi. [7] Karafuu pia ni nzuri kwa kupunguza gesi tumboni, tumbo kuvurugika (gastric irritability), kuvimbirwa, na kichefuchefu. Karafuu zinaweza kupikwa, kusagwa, au kuliwa pamoja na asali kwa afueni ya matatizo ya mmeng'enyo wa chakula. Katika kitabu chake [3] “Herbs that Heal: Natural Remedies for Good Health“ aliyeshinda tuzo kama mtaalamu wa tiba asili Dr. H.K. Bakhru ameandika: “Dawa hii ya asili ni tiba nzuri kwa ugonjwa sugu wa kuharisha(diarrhea) na kuharisha damu(dysentery).”
Sifa ya Kuzuia Bacteria
Karafuu imekuwa ikizungumzwa na wengi kwa sifa zake za kuzuia bacteria dhidi ya vimelea viletavyo magonjwa kwa binadamu.Bidhaa/vitu vitokanavyo na karafuu vimetosha kabisa kuua vimelea vya magonjwa. Zalisho llitokanalo na karafuu pia ni muhimu dhidi ya bakteria waenezao ugonjwa wa kipindupindu. [8]
Karafuu juu ya meza, chanzo: Shutterstock |
Sifa ya Kuzuia Kansa
Karafuu imekuwa muhimu kwenye jamii ya madawa kwa sifa zake za kuzuia kansa(carcinogenic properties). Utafiti uliochapwa kwenye jarida la Oxford Journal: Carcinogenesis imeonyesha kwamba karafuu zinaweza kusaidia kudhibiti kansa ya mapafu kwenye hatua za mwanzo. [9] Tafiti zinasema kwamba oleanolic acid inayopatikana kwenye karafuu husaidia kudhibiti tumor(uvimbe unaotokea kwenye tumbo), wakati utafiti mwingine umeonyesha kwamba eugenol inayopatikana kwenye karafuu ina uwezo wa kuzuia kansa dhidi ya kansa ya njia ya uzazi (cervical cancer). [10] [11] Wakati tafiti zaidi juu ya mada hii huitaji kufanyika,ugunduzi huu wa awali unaonyesha kwamba karafuu zingeweza kuwa suluhisho chanya kwenye eneo hili.
Ulinzi wa Ini
Karafuu zina kiasi kikubwa cha viondosha sumu, ambavyo ni muhimu kwa kulinda viungo vya mwili dhidi ya sumu huru (free radicals), hasa Ini. [12] Mfumo wa ufanyaji kazi wa kimetaboliki, kwenye mbio ndefu, huongeza uzalishwaji wa sumu huru na mafuta yaliyoganda, huku ukipunguza kiwango cha viondosha sumu kwenye Ini. Vizalishwa vya karafuu ni muhimu kwenye kupambana na athari hizi. [13]
Udhibiti wa Kisukari
Karafuu zimekuwa zikitumika kwenye matibabu ya kale kwa magonjwa mengi tu. Moja kati ya magonjwa hayo ni kisukari. Kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na kisukari, kiasi cha insulin kinachozalishwa na mwili kinaweza kuwa haba, au haizalishwi kabisa. Vizalishwa vya karafuu huiga insulin kwa namna fulani nyingi na husaidia kudhibiti kiwango cha sukari ya damu. Utafiti mmoja uliochapwa kwenye jarida la Journal of Ethnopharmacology umegundua kwamba karafuu zina msaada mzuri kwaenye ugonjwa wa kisukari kama sehemu ya chakula kitokanacho na mimea. [14]
Utunzaji wa Mifupa
Vizalishwa (extracts) vya karafuu zikiwemo kampaundi za phenolic, kama vile eugenol na kampaundi zilizotokana na eugenol, kama vile flavones, isoflavones, na flavonoids.
Tafiti zinasema kwamba kampaundi hizi zinaweza kusaidia kwenye kutunza uzito wa mifupa na kiasi cha madini ya mfupa, vilevile huongeza nguvu ya mifupa kwenye kesi ya osteoporosis . [15] Tafiti zaidi zinahitajika kuthibitisha uzito wa ugunduzi huu.
Huimarisha Kinga ya Mwili
Tib za kale za kihindi (Ayurveda) huchanganua bdhi ya mimea kuwa na athari nzuri kwenye kuendeleza na kuulinda mfumo wa kinga ya mwili. Moja kti ya mimea hiyo ni Karafuu. Ua hilo lililokaushwa la karafuu lina kampaundi zinazoimarisha mfumo wa kinga ya mwili kwa kuongeza idadi ya seli hai nyeupe za damu. [17]
Sifa za kuzuia Uvimbe
Kiungo hiki kina sifa za kuzuia uvimbe kwenye mwili nakuua maumivu. Majaribio juu ya karafuu yaliyofanyika kwa kumlisha panya wa maabara chakula chenye karafuu yanasema kwamba uwepo wa eugenol umepunguza uvimbe unaosababishwa na edema (kuvimba kwa sehemu ya mwili au mwili mzima kutokana na jeraha). Ilihakikiwa pia kwamba eugenol inaweza kupunguza maumivu kwa kuamsha vipokea maumivu(pain receptors). [17]
Afya ya Kinywa
Karafuu zinaweza kutumiwa kwa ajili ya kupunguza magonjwa ya fizi kama vile gingivitis na periodontitis. Kulingana na jaribio lililochapishwa kwenye jarida la Journal of Natural Products, karafuu huzuia na kudhibiti ukuaji wa vijidudu vya magonjwa mdomoni (pathogens), ambavyo hupelekea magonjwa kadhaa ya kinywa. Zinaweza pia kutumika kwa kutuliza maumivu ya meno kutokana na sifa zake za kuua maumivu. [18]
Matibabu ya Maumivu ya Kichwa
Maumivu ya kichwa yanaweza kupunguzwa kwa kutumia karafuu. Saga maua machache ya karafuu na changanya na chumvi ya mawe kiduchu. Weka mchanganyiko huu kwenye maziwa.Mchanganyiko huu hutuliza maumivu ya kichwa haraka na kwa uhakika. [20]
Madhara ya Karafuu
Vilivyomo ndani ya karafuu vinaweza kuleta madhara kama zikitumika kwa wingi au zisipozimuliwa. Zifuatazo ni baadhi ya bidhaa zitokanazo na karafuu ambazo zinatakiwa kutumiwa kwa umakini.
- Mafuta ya Karafuu: Mafuta maalum ya karafuu hayatakiwa kutumika moja kwa moja. badala yake, yapoze kwenye mafuta ya mzeituni (olive oil) au kweny maji safi. Mafuta ya karafuu husemekana kuwa ni salama, lakini jaribio limegundua kwamba yana sifa za cytotoxic(sumu za seli hai) . [21]
- Sigara za karafuu: Indonesia, karafuu hutumika katka kipimo kikubwa mnokatika mfumo wa sigara, maarufu kama kreteks. Sigara hizi za karafuu zimekuwa kama mbadala wa sigara za tumbaku, lakini tafiti zilionyesha kwamba sigara za karafuu ni hatari zaidi kiafya kuliko sigara za tumbaku. Kwenye kesi ya sigara za karafuu, kiwango cha nicotine, carbon monoxide, na tar kinachoingia kwenye mapafu kilikuwa ni cha juu mno kuliko kile cha sigara za tumbaku. [22]
Safi nimependa makala hii imeandikwa kitaalam
JibuFutaNimepata vizuri San watanzania kusoma ndio wavivu, Wana kosa mambo mazuri Sina Shaka na mwandish kazi nzuri
JibuFutanashukuru mwandishi ila nna swali vp kama ukitafuna karafuu bila kuchemsha
JibuFutaje ina madhara
Asante sana kwa somo zuri nimeelewa na nimepata elimu muhimu sana
JibuFuta