Watu wengi hupendelea asali, dhidi ya sukari au viongeza utamu vingine, kwasababu kitu hiki chenye sukari asilia pia kina uwezo au sifa ya kukabiliana na bacteria na kuzuia uvimbe mwilini. [1] Kwa mfano, asali inaweza kuhifadhiwa kwa muda usiojulikana, kwani vijidudu vya magonjwa haviwezi kabisa kuotea juu ya asali. Mbali na wingi wake wa sukari, asali pia ina viwango vingine vidogo vya vitamin na madini, ikiwemo riboflavin (B2), madini joto (iron), zinc, vitamin B6, na nyuzi lishe (dietary fiber), kati hizo.
Maji ya limao yana kiongezo chenye nguvu kinachitwa citric acid, ambacho ni kawaida kutumika kama wakala wa usafishaji kwasababu ya nguvu yake ya kuzuia bacteria na uchafu. [2] Malimao, maji ya limao, na mafuta ya limao pia ni muhimu kwa mbadala au wataalamu wa tiba asilia, kwasababu ya vingo vya juu vya viondosha sumu na virutubiso vilivyomo kwenye tunda hili.
Wakati malimao ni viamsha afya vizuri kwa namna yao, yanakuwa na nguvu zaidi yakichanganywa na asali!
Namna ya Kutengeneza Kinywaji cha Asali na Limao?
Wakati watu wakiongelea namna ya kuchanganya asali na limao kuwa kama chakula flani cha kuamsha, mara nyingi huwa wanamaanisha asali limao maji, ijapokuwa kuna uchanganyaji wa aina nyingine- pamoja na baking soda au viongeza vingine vya virutubisho– pia una athari nzuri. Fata hatua hizi nyepesi kwa afya bora!
Mahitaji
- maji ya limao kutoka kwenye malimao 2
- Asali Mbichi vijiko viwili vya chai.
- 237ml za maji
Maelekezo
- Kutengeneza kinywaji kizuri cha asali na limao , chemsha maji na yaache yapoe kidogo. Kama unataka unywe kikiwa cha baridi, usichemshe maji.Japo imesemwa hivyo, maji ya vuguvugu ni bora zaidi kiafya na husaidia kwenye kupunguza uzito. Pia husaidia kwenye homa na kushindwa kupata choo.
- Kamua malimao mawili kwenye maji.
- Koroga asali mbichi, isiyochanganywa na chochote.
- Sasa furahia kinywaji chako!
Jinsi ya Kutengeneza Mask ya Uso ya Asali-na-Limao?
Utapigwa na butwaa kwa matokeo ya mazuri ya mask ya uso ya asali-na-limao. Baada ya kuitumia, ngozi yako itaachwa ikiwa safi, yenye unyevu nyevu, na yenye kuwaka pamoja na afya nzuri! Fata maelekezo haya kutengeneza mask yako mwenyewe!
Mahitaji
- 1/2 limao (au)
- Matone 5 ya mafuta ya limao
- Asali vijiko 2 vya chai (asali mbichi isiyochanganywa na chochote mara zote itakuwa ni wazo zuri)
Maelekeo
- Kutengeneza mask ya uso ya asali-na-limao, kamua limao 1/2 kwenye bakuli. Ongeza vijiko 2 vya chai ndani yake na ukoroge vizuri hadi ifanane na dawa kikohozi ya maji.
- Kabla ya kuitumia mask, osha uso wako vizuri. Hakikisha usisafishe sana ngozi ukaondoa seli zilizokifa za juu ya ngozi, kwa kiingereza inaitwa exfoliation, kwani maji ya limao yanaweza kuunguza ngozi iliyokuwa exfoliated.
- Acha mask ikae kwenye uso wako kwa takribani dakika 20, na jizuie kuongea au kutembeza misuli ya uso wako.
- Ukimaliza, nawa na maji ya baridi kwani inasaidia kuziba matundu ya ngozi. kausha uso wako kwa kutumia taulo na fuata hatua hizi kila siku asubuhi na usiku. Usisahau kupaka moisturizer nzuri baada ya mwenendo huu. Endelea kufanya hivi kwa wiki mbili kupata matokeo. Uso wako utauhisi soft, msafi, na utakuwa huru na chunusi. Kwahiyo, nikutakie mwenendo wenye furaha kwa ngozi yako.
Faida za Asali na Limao
Asali na Limao, kwa kuzichanganya, huzuia uzimbe,ni wakala wa kuzuia sumu mwilini, huzuia bacteria, huleta muamsho, huongeza hamu ya kula,na huamsha ufanisi wa kimetaboliki.
Huondoa Sumu Mwilini
Kwenye matibabu ya kiasili, maji ya asali na limao yamekuwa yakidhaniwa kuongeza ufanisi wa mwendo wa chakula kwenye utumbo (peristalic motion) kitendo kinachosaidia kusafisha utumbo na kuzuia bacteria hatari kuweka makazi. [3] Zaidi, maji ya asali-limao yanaweza kushinikiza ukojoaji, na ikitumika kama dawa ya kuweza kuondoa uchafu wa majimaji na chumvi mwilini (diuretic), mkorogo huu uharakisha kuondoa sumu kutoka kwenye mwili. Ukojoaji hutoa chumvichumvi isiyotakiwa, mafuta(fats), sumu, na maji kutoka kwenye mwili, na mkorogo huu wa afya huweka kitendo hicho kwenye mfumo wa mwili.
Kupungua Uzito
Ijapokuwa mchanganyiko huu una kiwango cha juu cha sukari, uzito wa madini na vitamini vinaweza kuufanya mwili ujihisi kushiba. Changanya hilo na muamsho wa ufanisi wa kimetaboliki unaotokana na mchanganyiko huu, na una kisaidizi kamili cha kupunguza uzito. Citrates zipatikanazo kwenye malimao yana umuhimu kwenye kazi za kimetaboliki ndani ya mwili.
Hutibu Kikohozi
Moja kati ya njia nzuri za kutumia asali na limao ni pale unaposumbuliwa na koo, kikohozi au tatizo la mfumo wa upumuaji. Mchanganyiko huu unaweza kurainisha njia za hewa na kuzuia muwasho, ambao unaweza kupunguza shida ya kikohozi, wakati huo pia ukiimarisha mfumo wa kinga mwilini na kupunguza maambukizi ya bacteria na virusi kwenye mfumo wa hewa.
Msaada kwenye Umeng'enyaji
Nguvu za kuzuia bacteria za asali na limao zinaweza zote zikaungana kwenye mchanganyiko huu, na kuifanya kuwa dawa nzuri kwa tumbo lako. Ilikuwa ikidhaniwa kuondoa bacteria hatarishi kutoka kwenye tumbo na njia za umeng'enyaji lakini pia kuongeza kasi ya umeng'enyaji, kutokana na acid iliyopo ya limao. [4] Kunywa maji yenye asali-na-limao pia kunaamsha uzalishwaji wa nyongo, ambao zaidi husaidia kwenye kazi ya umeng'enyaji wa chakula.
Huboresha Metaboliki
Asali na limao zote zina uwezo wa kuharakisha ufanisi wa kimetaboliki na toa nishati ya kutosha.Hii ni muhimu hasa ndio umepona kutoka kwenye ugonjwa au jeraha, ndio maana watu wengi hupendelea kuchagua kikombe cha chai ya moto yenye asali wakitaka kuikimbiza homa inayoishia.
Hutibu Chunusi
Kuna idadi ya viondosha sumu vipatikanavyo katika vyakula vyote hivi. [5] Unapokunywa mchanganyiko huu au kutengeneza mkorogo kwa ajili ya ngozi, inawezekana kupata matokea yanayopimika. Asali na limao hujulikana kuboresha muonekano wa chunusi na kuzuia maambukizi mengine ya ngozi, kwa sababu ya sifa au uwezo wa kuzuia bacteria na kiasi cha vitamin C kilichopo. Maji ya limao yakiwa yenyewe mara nyingi hutumika kwenye kuondoa madoa doa na makovu juu ya ngozi, lakini ukiipigia upatu na asali kwenye diet yako ni wazo la busara sana.
Huimarisha Mfumo wa Kinga ya Mwili
Mfumo wa kinga wa mwili hupata muamsho mkubwa unapochanganya asali na limao. Malimao yana kiwango cha juu cha vitamin C, vilevile virutubisho vingine muhimu na viondosha sumu, pia limao lina sifa ya kuzuia bacteria na kuzuia uchafu. [6] Asali, kwa upande mwingine, ni moja kati ya vizuia bacteria vyenye nguvu kuliko vyote vilivyowahi kufahamika! Kuvitumia vyote kwa pamoja, iwe kwa kula au kutumia kwenye ngozi, inamaanisha kwamba mfumo wako wa mwili unapata muamsho mkubwa!
Hudhibiti Acid mwilini
Ijapokuwa watu wanafikiri limao kama lina acid nyingi kiuhalisia, kipindi citric acid inapoingia kwenye miili yetu,kiukweli huwa na athari ya kialkali juu yetu! Hii ni muhimu sana kwasababu magonjwa hutokea kipindi mwili umezidiwa na acid. [7] Kwa kuongeza limao na asali kwenye msosi wako, unaweza kuweka sawa au kubalance hali ya acid ya mwili, ambayo mara nyingi huzidisha kiwango cha acid, kwa namna hiyo unapunguza hatari kuzalisha magonjwa sugu!
Madhara ya Kutumia Asali na Limao
Kuna watu wana allergy na asali, kwahiyo kuipakaa kwenye uso au majeraha kuharakisha kupona kunaweza kuleta madhara yasiyotegemewa. Pia, ikitumika kwenye ngozi na kuachwa kwa muda mrefu, asali yaweza kusababisha muwasho kwenye ngozi. Zungumza na mtaalamu wa ngozi au mtaalamu wa allergy kabla hujatumia hii tiba nyumbani. Wakati watu wengi hawapatwi na madhara yoyote kutokana na kimiminika hiki, ni jambo la muhimu sana kutazama mpokeo wa mwili wako juu ya kujaribu taratibu mpya ya kiafya!
Kinywaji hiki ni kizuri na kinaweza kutumika kwa watu wa hali zote.
JibuFutaNashukuru kwa elimu mnayotupatia
JibuFutaSafi y
JibuFuta