Faida 12 za kushangaza za Asali

Asali imekuwa ikitumika na tamaduni zisizohesabika duniani kwa zaidi ya miaka 2500 iliyopita. Wakati faida kadhaa za asali zimeifanya kuwa elementi muhimu za madawa ya asili kama vile matibabu ya Ayurvedic, wanasayansi pia wanafanya tafiti juu ya faida zake kuhusiana na madawa ya kisasa, hasa katika kutibu majeraha.

Inafahamika kama Honig Ujerumani, Miele Kiitalino, Shahad kwa kiHindi, Miel kwa Kifaransa na Kispanish, Mel kwa Kireno, мед kwa Kirusi, Honing kwa kiHolanzi, na μελι kwa Kigiriki; hakuna mahali karibia dunia nzima ambapo asali haitumiki kwa mapana na kusherehekewa kama sehemu ya chakula cha asili.

Lakini ni kitu gani kinafanya asali kuwa maarufu sana? Yawezekana sababu ikawa ni urahisi wake kuitumia. Unaweza kula moja kwa moja, kuweka kwenye mkate kama siagi au jam, itumie kwenye nafasi ya sukari kwenye juisi, au kuichanganya na maji ya uvuguvugu, juisi ya ndimu, mdalasini, na dawa nyingine za asili kwa matibabu ya nyumbani. Hupendelewa kwa ladha yake vilevile kwa faida zake kiafya, na kuifanya kuwa muimu mno.


Faida za Kiafya za Asali

Faida zake hujumuisha matibabu yafuatayo, yalichukuliwa kutokana na watabibu wa tiba asili na wataalamu wa madawa ya kisasa.

Kiongeza Utamu chenye Afya

Inaweza kutumika kama mbadala wa sukari kwenye vyakula na vinywaji vingi. Ina kama asilimia  69% za glucose na fructose, kuifanya asali kutumika kama kiongeza utamu (sweetener) ambayo ni bora zaidi kwa afya yako kwa ujumla kuliko sukari ya kawaida nyeupe. Bodiya taifa ya Asali ya Marekani huichukulia asali kama kitu cha muhimu kuwepo jikoni. [1]


Kupunguza Uzito

Ijapokuwa ina kalori nyingi kuliko sukari inapotumika pamoja na maji ya vuguvugu, asali husaidia kumeng'enya mafuta ya fati yaliyohifadhiwa kwenye mwili wako. Vivyo hivyo, asali pamoja na limao au mdalasini husaidia kwenye kupunguza uzito.

Huleta afueni kwa kikohozi

Mwaka 2012 jaribio lilifanyika kwa watoto 300 children wenye umri wa miaka kuanzia 1 hadi 5 kutambua athari ya asali kwenye kikohozi cha usiku na ubora wa kulala. Majibu yalichapwa kwenye majarida ya tiba za watoto na vijana walio kwenye baleghe(Pediatrics Journals) kwamba asali yaweza kutumika kwenye matibabu ya kikohozi na shida ya kupata usingizi yanayohusiana na mfumo wa upumuaji kipindi cha utoto unapopata maambukizi, upper respiratory tract infections (URIs). [2]

Huzidisha Nishati

Kulingana na USDA, asali imesheheni karibu kalori 64 kwenye kijiko cha mezani. [3] Kwahiyo, hutumika na watu wengi kama chanzo cha nishati. Kwa upande mwingine, kijiko kimoja cha mezani cha sukari kitakupa kama kalori 15 hivi. Zaidi, kabohaidreti iliyomo inaweza kubadilishwa kwa urahisi na kuwa glucose, kutokana na urahisi wake wa mwili kumeng'enya kitu hiki cha asili.




Huongeza Ufanisi

Tafiti zimeonyesha kwamba asali ina athari kubwa kwenye kuamsha ufanisi wa mwanamichezo. Ni njia nzuri ya kuweka sawa viwango vya sukari mwilini, kurudisha misuli kwenye hali ya kawaida, kurudisha glycogen baada ya mazoezi, sambamba na kuweka sawa kiwango cha insulin kwenye mwili.

Huboresha Kumbukumbu

Asali imesheheni polyphenols ambazo zinaweza kuimarisha na kuboresha kazi za ubongo zinazohusiana na kumbukumbu. [4] Hupambana na tatizo la kukumbuka na  huimarisha ufanyikaji wa kumbukumbu kwenye kiwango cha  kimolekyuli. Utafiti juu ya asali ya Tualang, asali ya maua tofauti tofauti mengi inayopatikana Malaysia, uligundua kwamba ulaji wa asali huboresha umbo la ubongo kuimarisha kazi kadhaa za kujifunza na kumbukumbu. [5]

Ina Utajiri wa Vitamini na Madini

Imesheheni aina  flani za vitamini na madini. [6] Aina za vitamini na madini na wingi wao hutegemeana na aina za maua zilizotumika kufugia nyuki. Kawaida asali huwa na vitamin C, calcium, na madini joto(iron). Kiwango cha vitamini na madini kwenye sukari ya kawaida,kwa upande mwingine, haina umuhimu kabisa.

Ina Sifa ya Kuzuia Vimelea Vya Magonjwa

Ina sifa za kuzuia bacteria na fangasi waletao magonjwa, ndio maana hutumika mara nyingi kama kizuia vijidudu asilia vya magonjwa kwenye tiba asilia. Kwenye majaribio ya vyombo vya glass vya maabara kwenye ngazi tofauti za kitiba asali imeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia bacteria hata kwenye uwepo wa bacteria wenye uwezo wa kuhimili antibiotic ambao husababisha madhara yanayotishia maisha ya mwanadamu. [7] Hatahivyo, uwezo wa kuzuia bacteria unatokana na chanzo cha nectar.

Sifa za Kuondosha Sumu

Asali ina nutraceuticals, ambazo zina athari kubwa kwa kuondoa sumu huru (free radicals) kutoka kwenye mwili. Matokeo yake, mfumo wa kinga ya miili yetu huimarika dhidi ya matatizo mengi sugu ya kiafya. Jaribio juu ya sifa za kuondosha sumu za asali, zilizochapwa kwenye jarida la Journal of Agricultural and Food Chemistry,  lilidai kwamba sifa hizi huchangiwa na uwepo wa kampaundi nyingi kwenye asali, zikiwemo phenolics, peptides, mazao ya Maillard reaction , organic acids, vimeng'enyi (enzymes), na vitu vingine vidogo vidogo. [8]

Sifa za Kuzuia Kansa

Pitio lililochapwa kwenye jarida la  Evidence-Based Complementary and Alternative Medicine limegundua kwamba kuna ushahidi unaoendelea kukua wa uwezo wa asali kuzuia kansa. [9] Hii huonyeshwa na uwezo wake wa kuzuia seli za tumor kukua( antiproliferative), kuua seli mbaya, kuingilia kati ukuaji wa seli haribifu, kuzuia uvimbe kutokea mwilini. Makala nyingine iliyochapwa kwenye jarida hilohilo limeonyesha kwamba kama kitu cha asili, asali ni chaguo muhimu na lenye gharama nafuu kwenye kuhudumia kansa kwa mataifa yanayoendelea. [10]


Matunzo ya Nywele na Ngozi

Maziwa na asali mara nyingi huandaliwa kwa pamoja kutokana na viongezo hivi vyote viwili husaidia kwenye kutengeneza ngozi laini na yenye kupendeza. Kwa sababu hii imekuwa jambo la kawaida kwa watu wa mataifa mengi kunywa mchanganyiko huu kila asubuhi. Jaribio lililochapwa kwenye jarida la European Journal [11] of Medical Research limegundua na kuhakikisha matumizi ya asasli kwa kuondoa mba na dermatitis (mfano wa chunusi zinazotokea nyuma ya goti, shingoni, sehemu ya mbele ya kiwiko cha mkono juu ya ngozi). Jaribio linasema kwamba asali mbichi inaweza kutibu tatizo la  seborrheic dermatitis, linahlousiana na kupoteza nywele na kuzuia tatizo kujirudia ikitumiwa kila wiki.

Uharaka wa Jeraha Kupona

Utafiti wa kina uliofanyika kujaribu faida zake kwenye kutibu majeraha. Majibu ilikuwa kama ifuatavyo hapa chini:

  • Asali ina miliki sifa kuzuia vijidudu viletavyo magonjwa.
  • Huimarisha autolytic debridement(mwili kutumia vimeng'enyi vyake na maji maji kulainisha gamba gumu linalotokea baada yakupona jeraha la kuungua kwenye ngozi).
  • Huondoa harufu kwa vidonda vyenye harufu mbaya.
  • Huzidisha haraka ya kupona kidonda kwa kuamsha tishu za vidonda.
  • Husaidia kwenye kuanzisha uponyaji kwa vidonda vya muda mrefu.
  • Husaidia pia kwenye kuimarisha uponyaji wa vidonda kwa kuvibakisha kuwa vibichi (moist wound healing).

Nguvu hizi za kutibu sio kwamba zimeorodheshwa bila ushahidi. Kitengo cha utafiti wa asali cha Waikato hutoa maelezo kwa kina juu ya tafiti za duniani zilizochukuliwa juu ya faida ya asali kwenye matibabu. Kulingana na ripoti ya shirika la habari la BBC madaktari wa hospitali ya Christie Hospital iliyopo Didsbury, Manchester awana mpango wa kutumia asali kwa ajili kupona haraka kwa wagonjwa wa kansa baada ya kufanyiwa upasuaji. [12] Utafiti kama huu utatoa ushahidi wa kisayansi kwa  imani iliyobebwa na wapenzi wa asali duniani kote na itasaidia kuleta faida kwa watu wengi.

Sasa unatambua faida za asali, unakulaje? Unaweza kuila kama ilivyo, kuiweka kwenye maji au kwenye vinywaji tofauti, na unaweza kuiongeza kwenye vyakula tofauti tofauti.



Vitu Vinavyosababisha Faida za Asali

Sio asali zote zimetengenezwa sawa, kwa hiyo ubora ni tofauti. Gharama na faida zake kiafya zote hutegemeana na ubora wake,kwahiyo imekuwa swala la muimu sana kwa watengenezaji na wanunuzi kutambua vitu kadhaa vinavyoathiri ubora wa asali. Baadhi ya vitu hivyo ni pamoja na aina ya maua yaliyotumika kutengeneza masiga, zoezi la kuchuja asali, mazingira ya kuhifadhia, jotoridi lililotumika, na zaidi. Vitu hivi vimeelezewa hapa chini kwa kina:

Aina ya maua:  Wakati asali ina ubora wa mwingi, sifa zake pia hutokana na chanzo chake. Jaribio lililochapishwa kwenye jarida la Asian Pacific Journal of Tropical disease limegundua kwamba chanzo cha asali hushinikiza sifa zake. Aina tofauti za asali zimeonyesha viwango tofauti vya kudhibiti bacteria. Asali iliyotokana na maua ya Clover yameonyesha uwezo wa juu zaidi wa kupambana na bacteria, ikifuatiwa na Asali inayotokana na matunda ya citrus au harufu za matunda hayo kama chungwa, limao, ndimu nanasi n.k (citrus honey) na ikifuatiwa na asali iliyotokana na maua ya pamba kwa mfuatano.

Uchanganyaji: Asali ya Polyfloral (ambayo hupatikana kutoka kwenye ua zaidi ya moja) ina faida zaidi kuliko ile iliyotokana na ua moja pekee (monofloral). Kwahiyo, kampuni nyingi leo hii huuza asali iliyochanganywa kwani hutoa faida nyingi.

Uhifadhi: Ikihifadhiwa kwa muda mrefu, asali huwa na rangi nyeusi. Hupoteza baadhi ya sifa zake na inaweza kufanyika na kuwa pombe kama kiasi cha maji kipo juu. Kwahiyo, uhifadhi wa muda mrefu unatakiwa kuepukwa. Asali iliyovunwa kipindi cha sasa hivi inatakiwa kupendelewa kutumika kwa faida zilizotajwa hapo juu.

Jotoridi: Kuchemsha asali hupelekea mabadiliko ya haraka kwenye muundo wake wa kikemikali. Matokeo yake, kuchemsha asali kwa joto kali hupunguza faida zake. Hii ndo maana watu hupendelea asali mbichi, isiyochanganywa na kitu chochote. asali mbichi humaanisha hakuna kuchuja na hakuna kuichemsha. 

Kiwango cha Maji: Asali inaweza kufanyika kuwa pombe pia. Kama kiwango cha maji kipo juu (zaidi ya 19%), uwezekano wake wa kufanyika kuwa pombe ni mkubwa. Unaweza kupima kiwango cha pombe kwa kutumia kifaa kiitwacho refractometer. Zaidi, asali inayomiminika kwa wepesi ina kiwango kikubwa cha maji au imechemshwa na kuharibu muundo wake wa asili, kwa mtindo huo kupunguza faida zake ambazo zingekufaa.

Rangi: Rangi ya asali ni njia moja ya kuhukumu ubora wake. Asali yenye rangi nyepesi mara nyingi hupendelewa kwani ina ladha ya kati. Asali pia yaweza kuwa nyeusi lakini huwa na radha kali kwasababu ya maua nyuki alipokusanya.

Kuchuja: Faida nyingi ni juu ya uwepo wa pollen ndani ya asali. Bila pollen, ni mchanganyiko wa kimiminika chenye glucose-fructose na ni mbaya kwako kama sukari. Kwa bahati mbaya, makampuni huweka sokoni asali nyeupe kama ndio yenye ubora mzuri, wakati, kwenye uhalisia, asali iliyochujwa sana haina faida nyingi kiafya kabisa. Kama hilo lishasemwa, unatakiwa kuwa makini wakati unatumia asali yenye pollen nyingi. Kama una allergy ya pollen, jizuie kuitumia.

Maoni