Mchanganyiko wa baking soda na maji ya limao una faida kadhaa za kiafya, ikiwemo uwezo wake wa kuondoa sumu mwilini, kuweka sawa viwango vya pH mwilini, na kuboresha mmeng'enyo wa chakula. Pia huimarisha mfumo wa kinga mwilini, huboresha afya ya moyo, huilinda ngozi, hutibu Ini, na huzuia ugonjwa sugu.
Tiba nyingi za kiafya zimejipatia umaarufu kwenye miaka ya hivi karibuni, lakini matumizi ya baking soda na limao yanatupeleka miongo kadhaa nyuma kwenye mzunguko wa tiba asili. Zikiwa zenyewe kama zenyewe, kila kimojawapo kina faida zake nyingi za kiafya, lakini vikichanganywa, vinaweza kuwa na wingi faida za kiafya kwa ujumla.
Kwa kuanza, maji yaliyokamuliwa kutoka kwenye limao (Citrus limon) yana utajiri wa vitamin C na antioxidants (viondosha sumu) ambavyo vina mahusiano ya karibu mno na mfumo wa kinga mwilini na athari za diuretics ( uwezo wa kuzidisha kiwango cha maji na cumvi-chumvi kutolewa nje ya mwili ) kwenye mwili. [1] Malimao yana wingi wa madini na vitamini, kuyafanya maji yake , mbali na ucachu wake, kuwa maarufu kwenye upishi na tiba mbadala.
Kwa upande mwingine, baking soda, pia hufahamika kama sodium bicarbonate, kiutaalamu huchukuliwa kama dawa, mbali na kutumika kwake kwingi kwenye shughuli za upishi. Athari za ki-alkali za baking soda hufahamika vizuri, ndio maana watu huitumia kwenye matibabu tofauti kwa matatizo ya ki-acid kama vile matatizo ya mmeng'enyo wa chakula, kiungulia, na kupunguza hatari ya kuzidi kwa kiwango cha acid mwilini (acidosis ). Baking soda inaweza kusaidia kupunguza acid kwenye mwili na kurudisha pH kwenye hali inayofaa ( homeostasis ).
Hata hivyo, ijapokuwa hayo yote yamesemwa, unahitaji kuongea na daktari wako au mtaalamu wako wa afya kabla hujaongeza baking soda kwenye mtindo wako wa afya. Inaweza kuharibu au kuingilia dozi nyingine inayotumika na inawezekana usishauliwe kutumia kwa ujumla.
Faida za Baking Soda na Maji ya Limao
Viwango Stahiki vya pH
Mara nyingi watu hudharau umuhimu wa kupunguza viwango vya acid kwenye mwili, lakini kuhakikisha kiwango staiki cha pH ni muhimu kwa afya nzima ya mwili. Sodium bicarbonate hujulikana kama alkalizing agent ambayo inaweza kushusha viwango vya acid, kupunguza vitu kama kiungulia na kuvimbilwa, lakini pia kuuweka mwili kiwango cha ki-alkali. Hii imethibitishwa kwenye utafiti uliofanywa [2] na Dr. Beverley Booth, Chuo kikuu cha Virginia, US. Pia, citric acid iliyopo kwenye malimao ina athari za ki-alkali pindi inapomeng'enywa!
Matunzo ya Ngozi
Kulingana na jaribio lililochapwa kwenye jarida la Kemia ya Kilimo na Chakula, maji ya limao ni kinywaji chenye viondosha sumu vingi mno. [3] Wingi wa viondosha sumu na citric acid vinaweza kupunguza vileta sumu na kuzuia athari hasi za free radicals ndani ya mwili. Hii ni nzuri kwa ngozi na inaweza kuzorotesha dalili za uzee, kupunguza madoa yatokanayo na Jua na mikunjo, na kuipa ngozi yako mng'ao wa kiafya. [4] Maji ya limao na baking soda pia husaidia kupunguza makovu ya chunusi.
Sifa za Kusafisha Tumbo
Maji ya limao kwa kipindi kirefu yamekuwa yakijulikana kama diuretics na yanaweza kuufanya mwili utoe mkojo, kwa maana hiyo huondoa sumu zilizozidi, chumvi, mafuta (fats), na maji. [5] Hii ni habari njema kwa mafigo, kwani hupunguza mkandamizo na shinikizo kwenye viungo hivyo na kuhakikisha kwamba mwili wako unabakia na kiwango kidogo cha sumu. Zaidi, jaribio lililowekwa kwenye jarida la BMC Urology linashauri kwamba maji ya limao yanazuia tatizo la urolithiasis, ambayo ni uwepo wa mfano wa mawe magumu kwenye kibofu cha mkojo na njia ya mkojo. [6]
Meno Meupe
Kulingana na jaribio lililochapwa kwenye jarida la American Dental Association, dawa za meno zenye baking soda ni nzuri na salama zikitumika kwa kufanya meno kuwa meupe. [7] Hatahivyo, ni muhimu kutambua kwamba muda mwingine asili ya ukali wa limao una asili ya kukwangua gamba la juu la meno (tooth enamel). Mwanzoni hupunguza kutu kwenye meno, na kushusha viwango vya acid mdomoni, lakini kuna njia zaidi kuliko kutumia mkorogo huu kama dawa ya meno. [8]
Washauri wengi wa mchanganyiko huu wa baking soda na maji ya limao kutumika kwa kufanya meno yawe meupe hudai kuwa athari mbaya za limao husawazishwa na viwango vya juu vya pH ya baking soda, kwa maana hiyo kuifanya mchanganyiko huu kuwa salama kwa matumizi. Utafiti zaidi unahitajika kuthibitisha jambo hili.
Mmeng'enyo Ulioboreshwa
Mchanganyiko wa baking soda na maji ya limao hufanya kazi kama kipoozesha acid kizuri na hujulikana kwa kupunguza dalili za indigestion (hali ya chakula kutomeng'enywa tumboni) kwa haraka, kupunguza gesi iliyozidi kwenye njia ya chakula ( excess flatulence), kuvimbilwa (bloating), misuli kukaza (cramping), na kiungulia (kiungulia). [9] Kwa kuzuia uvimbe(inflammation) tumboni, ambayo elementi mbaya ya mfumo wa kinga mwilini, maji ya limao na baking soda vinaweza kuimarisha afya ya tumbo lako. Jaribio lililofanyika kwa muda usiopungua mwaka mmoja kwenye Chuo cha Albert Einstein College of Medicine, New York, lilionyesha kwamba kwa wagonjwa wenye acidosis(hali ya viwango vya acid kuzidi mwilini) ya kawaida husumbuliwa na ugonjwa sugu wa figo, utumiaji wa sodium bicarbonate huimarisha kupunguza nguvu iliyopitiliza ya misuli. [10]
Afya Ya Moyo
Tafiti zimeonyesha kwamba ukinywa maji yaliyochanganywa na baking soda yanaweza kusaidia kushusha viwango vya cholesterol mbaya, na kuimarisha viwango vya HDL cholesterol. [11] Hii hupunguza uwezekano wako wa kupata atherosclerosis, na kwa maana hiyo kushusha hatari ya wewe kupata mstuko wa moyo na kiharusi. Ni muhimu ukazingatia pia kuna ushahidi wa kukinzana kwenye jambo hili ambapo baking soda imekuwa si nzuri kiafya kwa moyo. [12] Utafiti zaidi kwenye faida za athari za baking soda na maji ya limao kwenye moyo unahitajika.
Uzito Kupungua
Hakuna muunganiko wa moja kwa moja kati ya kutumia baking soda na maji ya limao kwenye kupunguza uzito, lakini kuna ushahidi kwamba baking soda can inaweza kuongeza nishati zaidi na uvumilivu kipindi cha ufanyaji wa mazoezi ya viungo. Nishati hii iliyozidi na shughuli za kila siku kwahiyo huipa motisha na kuongeza kasi ya ufanyaji kazi wa kimetaboliki (metabolism) hata kipindi cha mapumziko wakati wa mazoezi. Ijapokuwa kupungua uzito ni athari ya pili, inawezekana kusaidia jitahada zako za kupunguza uzito na mchanganyiko huu.
Kinywaji cha Kuondoa Sumu Cha Baking Soda na Maji ya Limao
Unaweza kutengeneza kinywaji cha kuondoa sumu cha baking soda na limao kwa kuongeza kijiko kimoja cha baking soda cha chai na maji ya limao kwenye glasi ya maji safi. Kwa matokeo mazuri kuwa na hakika kwamba unakunywa hii kwenye lililo tupu yaani kabla hujala chochote wakati wa asubuhi, ili ufurahie athari zake za umeng'enyaji siku nzima! Jaribu kutokunywa kinywaji hiki karibu na muda wako wa kula kwani haitofanya kazi kwa haraka kwenye mwili, na kwa maana hiyo, hakutakuwa na athari.
Neno la Tahadhari:Kama wewe ni mgonjwa wa moyo au unasumbuliwa na tatizo lolote sugu, mjamzito, au unanyonyesha, inashauriwa kupata usauri wa daktari wako au mtaalamu wako wa tiba kabla ya kutumia kinywaji hiki kwa namna yoyote. Zaidi, wastani unashauriwa, usiifanye iwe ni tabia yako ya kila siku kunywa sharubati ya baking soda na limao kwa umeng'enyaji. Kabla ya kujaribu tiba hii ya asili, ni busara kuzungumza na daktari wako au Tabibu wa tiba.
Je,banking soda ukiitumia kusafisha kwapani na sehemu za siri mama mjamzito unapata madhara?
JibuFutaBelgina ndunguru
Futa