Faida 12 za Kiafya za Limao zilizothibitiswa

Faida za kiafya za limao zinachangiwa na kiwango chake cha vitamin C ambacho husaidia kuimarisha ubora wa ngozi, huhamasisha kupunguza uzito, huimarisha mmeng'enyeo wa chakula, na hufanya kazi ya kuondoa harufu mbaya ya kinywa. Limao pia husaidia kwenye matibabu ya kukosa choo, mataizo ya meno, maambukizi ya koo, homa, hutibu ngozi iliyoungua, hutibu maradhi ya upumuaji, na shinikizo la juu la damu, vilevile pia vitamin C ikiipa faida nywele zako. Kwa vizazi na vizazi limekuwa likijulikana kwa sifa yake ya kutibu, limao pia husaidia kuimarisha mfumo wa kinga yako ya mwili.

Sharubati/Juisi ya limao, hasa, ina faida kadhaa za kiafya inayojihusisha nayo. Hata zaidi, kama kinywaji cha kuburudisa, juisi ya limao hukusaidia kuwa mtulivu na kupoa. 


Limao ni nini?

Limao ni tunda lililosheheni flavonoids, ambavyo ni virutubisho vyenye antioxidant (viondosha sumu) na sifa za kupambana na kansa. Husaidia kutibu tatizo la kukosa choo na kuimarisha afya ya ngozi.

Watu hutumia limao kutengeneza sharubati ya limao (lemonade) kwa kuchanganya majimaji ya limao na maji. Watu wengi pia hutumia pia kama kisaidizi cha kusafishia, kwa sababu ya uwezo wake wa kuondoa uchafu. Harufu yake kali inaweza kutumika kufukuzia mbu, wakati unywaji wa sharubati ya limao pamoja na mafuta ya mzaituni (olive oil) ni tiba unayoweza kutumia ukiwa nyumbani kuondoa mawe ya kwenye figo (galstones). Limao linajulikana sana kwa nguvu yake ya kutibu na linatumika kwa namna nyingi tofauti. Kulingana na matokeo yaliyoripotiwa kwenye utafiti wa jarida linalohusu magonjwa ya uvimbe kwenye maungio (Annals of the Rheumatic Diseases ), maji ya limao yanaweza kuweka ulinzi dhidi ya ugonjwa wa Inflammatory Arthritis (ugonjwa unaoleta uvimbe na maumivu kwenye maungio ya viungo vya mwili). [1] Hata hivyo, utafiti zaidi unahitajika kuthibitisha matokeo haya.

Faida za Kiafya za Limao

Faida kadhaa za kiafya za limao zimeelezewa kwa kina kama ifuatavyo hapa chini:


Hudhibiti Shinikizo la Damu

Juisi ya limao inaweza kukusaidia kudhibiti shinikizo la damu ukitumia kwa kipindi kirefu. Kulingana na utafiti uliochapishwa na  jarida la Lishe bora ufanyaji kazi wake ( Journal of Nutrition and Metabolism) ulaji wa limao kila siku, na kutembea (mwendo wa wastani wa mwili) vilisaidia kwenye kushusha shinikizo la juu la damu. [3] Makala ya utafiti wa mwaka 2014 unakubaliana na ugunduzi huu huku ukitambua kwamba sifa za juisi ya limao kushusha shinikizo la juu la damu huthibitishwa na wagonjwa wenye shnikizo la juu la damu (hypertension), kuliko watu wenye shinikizo la kawaida la damu. [4]


Husaidia Kupunguza Uzito

Kinywaji cha maji ya uvuguvugu pamoja na juisi ya limao na asali asubuhi husemekana kusaidia athari za kupunguza uzito. Wakati iyo inaweza isifanye kazi kwako, utafiti uliofanywa kwenye Panya ulithibitisha ya kwamba polyphenols zilizomo kwenye limao hudidimiza ongezeko la uzito wa mwili na mlundikano wa mafuta mwilini. [5] Hii inaweza kuleta athari chanya kwa kunywa juisi ya limao kwenye kupunguza uzito wa mwili wa binadamu.


Huzuia Mawe ya Figo

Limao, liwe limetoka kwenye tunda lenyewe na hata kwenye juisi yake baada ya kukamuliwa, lina kiwango kikubwa cha citric acid kwa lita moja kuliko mchanganyiko wa juisi ya Zabibu na Chungwa kwa pamoja.  Hii imethibitishwa kweye utafiti kwenye jarida la Journal of Endourology  Dr. Stephen Nakada. [6] Utafiti mwingine [7] umethibitisha kwamba kiwango kikubwa cha citric acid kwenye tunda husaidia kuongeza viwango vya citrate kwenye mkojo zaidi ya mara 2 bila kubadilisha jumla ya ujazo wa mkojo. Kwa hivyo, Juisi ya limao (lemonade) yaweza kutumika kama mbadala wa kutibu hypocitraturia calcium nephrolithiasis (mawe ya mkojo yanayotokea kutokana na uwepo mdogo wa citrate ). Tafiti zilizofanyika American Urological Association zinaangazia ukweli kwamba  lemonade au juisi ya limao inaweza kuondoa uwepo wa mawe kweny figo kwa kutengeneza citrate ya mkojo, ambayo huzuia utengenezwaji wa changarawe kwenye figo.


Matunzo ya Kinywa

Utafiti uliofanywa ulioongozwa na Dr. Pirkko Pussinen wa Chuo Kikuu cha Helsinki huripoti kwamba kiwango kidogo cha vitamin C kinaweza kusababisha periodontitis (maambukizi kwenye fizi). [8]

Kama juisi ya limao (maji ya limao) ikiwekwa kwenye jino linalouma, inaweza kusaidia kutuliza maumivu. Ukisugulia maji ya limao kwenye fizi inaweza kuzuia fizi kutoa damu wakati pia ikiondoa harufu mbaya ya kinywa inayotokana na baadhi ya magonjwa ya fizi. Kwa tatizo lolote linalozidi kuhusu kinywa, ni vizuri zaidi kupata ushauri wa daktari kwa matibabu.

Zaidi, inaweza kutumika kusafisha meno yako. Chagua dawa ya  meno (tooth paste) yenye limao kama moja vilivyomo humo, au ongeza matone yake kwenye dawa yako ya meno ya kawida. Baadi ya watu husugua meno yao kwa kutumia ganda la limao (upande wa ndani ndio unagusa meno yako) baada ya kukamua maji yake. Lakini kuwa makini, inaweza kuwa na acid nyingi, kwahiyo kama mdomo unaanza kuungua, sukutua fizi na meno yako kwa maji.


Matunzo ya Nywele

Maji ya Limao yamejithibitishia yenyewe kuwa ni kisaidizi kwenye  matibabu ya nywele zilizoharibrika kwenye nyanja pana. Ikipakwa kwenye uwaraza, maji ya limao yanaweza kukamata matatizo kama mba, nywele kupotea, na matatizo mengine yanayohusiana na nywele na uwaraza. Kama ukipaka maji haya moja kwa moja kwenye nywele, yanaweza kuyapa nywele zako mng'ao vile vile.


Matunzo ya Ngozi

Maji ya Limao, yakiwa dawa ya asili ya kukinzana na vimelea vibaya vya magonjwa, yanaweza pia kutibu matatizo yanayohusiana na ngozi. Maji haya yanaweza kutumika kutuliza maumivu ya kuungua na Jua na husaidia pia kutuliza maumivu ya kung'atwa na nyuki. Pia maji haya ni mazuri kwa kutibu chunusi(acne) na pumu ya ngozi(eczema). Hufanya kazi kama tiba ya kukinzana na uzee na yanaweza kuondoa makunyanzi na madoa meusi. Unapokunywa juisi yake iliyochanganywa na maji na asali huleta mng'ao wa kiafya kwenye ngozi, na kama tafuta vizuri ndani ya soko la vipodozi, utakutana na baadi ya sabuni zenye maji haya, lakini si kazi raisi rahisi kuzipata.


Afueni kwenye Vidonda

UsingKutumia maji ya limao kwenye makovu kunaweza kusaidia kupoteza makovu, na kwasababu ni wakala wa kuleta ubaridi, maji ya limao hupunguza hali ya kuungua na joto kwenye ngozi wakati una muwasho na joto.


Huzuia Jeraha dogo la kutokwa na Damu

Limao lina sifa ya kuzia vijidudu vya magonjwa na kugandisha damu (antiseptic & coagulant properties), kwahiyo lina sifa ya kuzuia utokwaji mdogo wa damu.Unaweza kuweka maji ya limao kwenye pamba na kuweka ndani ya pua kuzuia damu inayotiririka kutoka kwenye tundu za pua (nose bleeding).

Hupoozesha matatizo ya upumuaji

Maji ya limao husaidia kwenye kupunguza matatizo ya mfumo wa hewa mwilini na upumuaji, kama vile kumsaidia mtu aliyepatwa na shambulizi la pumu (an asthma attack). Kuwa na utajiri wa canzo cha vitamin C, husaidia kupambana na matatizo ya muda mrefu ya mfumo hewa kwenye mwili vile vile.

Kupumzisha mguu (Foot Relaxation)

Limao ni wakala wa kuua vidudu vyenye kuleta magonjwa na arufu yenye kutibu maradhi na hutumika kwa kupumzisha miguu. Weka maji ya limao kiasi kwenye maji ya vugu-vugu na tumbukiza miguu yako kwenye mchanganyiko uo kupata nafuu na kufanya misuli yako i-relax.

Hupunguza Kukakamaa kwa ngozi

Maji ya limao yanaweza kupunguza ukomavu kwenye ngozi, kwa hiyo yanaweza kutumika kwenye maeneo ambayo ngozi imekakamaa na kuwa ngumu kama kwenye unyayo na viganja vyako vyako vya mikono. [9]

Maoni