Kiasi kiduchu cha pilipili manga kilichoongezwa kwenye pishi lolote hufanya kazi zaidi ya kuwa kiongeza ladha. Mara nyingi huitwa mfalme wa viungo, pilipili manga inajulikana kutoa faida nyingi za kiafya huku ikitoa ladha nzuri kwenye pishi lolote. Utumiaji wa pilipili manga kwenye mlo husaidia kupunguza uzito, kuimarisha umeng'enyaji, huleta unafuu kwenye homa na kifua, huimarisha shughuli za kimetaboliki, na kutibu matatizo ya ngozi.
Pilipili manga ni tunda kutokea kwenye mimea jamii ya Piperaceae na hutumika kwa namna zote mbili, kama kiungo na dawa. [1] Kemikali ya Piperine, ipatikanayo kwenye pilipili manga, ndio kisababishi cha ladha ya kiungo hiki. Asili ya pilipili manga ni Kerala, jimbo lipatikanalo kusini mwa India. Tokea zama za zamani, pilipili manga ni moja kati ya viungo vilivyouzwa zaidi ya viungo vingine duniani. Pilipili manga si mmea wa msimu, ndio maana hupatikana kupatikana mwaka mzima. Kulingana na sifa zake za kuzuia bakteria, pilipili manga hutumika kutunzia vyakula. Pilipili manga pia ni wakala mzuri wa kuzuia uvimbe kwenye mwili.
Pilipili manga ina madini kama potassium, calcium, magnesium, phosphorus, sodium, vile vile baadhi ya vitamini kama thiamin, riboflavin, niacin, na vitamin B6, kutokana na takwimu za kitaifa za virutubisho za USDA. {2} Virutubisho vingine vilivyomo ni vitamin E, folate, na vitamin K.
Kiasi kikubwa cha pilipili manga pia kina nyuzi lishe (dietary fiber) na kiasi cha wanga na protini.
Faida za kiafya za Pilipili Manga
Pilipili manga husaidia kwenye kupunguza uzito, na huleta unafuu kwenye matatizo ya sinus, asthma(pumu), na matatizo ya njia ya pua. Pia hupunguza hatari ya ugonjwa wa kansa, na matatizo ya moyo na Ini. Sasa tujadili faida za pilipili manga kwa kina.
Sifa ya kuzuia Kansa
Viondosha sumu kwenye pilipili manga vinaweza kuzuia au kurekebisha uharibifu uliofanywa na sumu huru na kusaidia kuzuia magonjwa mengi. {3} Kulingana na utafiti ulioongozwa na mtafiti Jie Zheng, ambao ulifananisha viungo kadha wa kadha, pilipili manga ilionekana kuwa na uwezo wa kudhibiti shughuli za kansa kwa aina chache za kansa - ambazo zinajumuisha kansa ya titi, kansa ya utumbo na kansa ya tezi ya korodani. [4] [6] [5]
Ijapokuwa, tafiti zaidi na majaribio ya kitabibu yanahitajika kuhakikisha ubora wa kuzuia kansa.
Huimarisha Umeng'enyaji
Utumiaji wa pilipili manga huongeza uzalishwaji wa hydrochloric kwenye tumbo, ikimaanisha kuimarisha umeng'enyaji wa chakula. Umeng'enyaji sahihi unahitajika ili kuepusha matatizo ya utumbo yakiwemo kuharisha, kutopata choo, na kuvimbiwa kwa watoto. [7] Pilipili manga pia husaidia kuzuia utengenezwaji wa gesi kwenye utumbo, na inapoongezwa kwenye chalula cha mtu, inaweza kuchochea kutokwa jasho na kukojoa.
Kutoka jasho husaidia kuondoa sumu na vivamizi kwenye tundu za jasho ambavyo vilikaa humo. Pia inaweza kuondoa maji yaliyozidi. Kukojoa kunaondoa [8] uric acid, urea, maji yaliyozidi, na fati (ukweli unaofurahisha: 4% ya mkojo ni fati).
Kwahiyo, vyakula vya pilipili manga ni njia nzuri ya kupunguza uzito kiasili. Kipindi seli za fati zikivunjwavunjwa, zina shughulikiwa kwa urahisi na mwili na kutumika kwenye mambo mengine kuliko kujazana kwenye mwili wako na kukufanya kuzidi uzito.
Kwahiyo, vyakula vya pilipili manga ni njia nzuri ya kupunguza uzito kiasili. Kipindi seli za fati zikivunjwavunjwa, zina shughulikiwa kwa urahisi na mwili na kutumika kwenye mambo mengine kuliko kujazana kwenye mwili wako na kukufanya kuzidi uzito.
Utunzaji wa Ngozi
Pilipili manga inaweza kusaidia kutoa nafuu dhidi ya vitiligo, ambao ni ugonjwa wa ngozi unaosababisha baadhi ya maeneo ya ngozi kupoteza rangi yake ya kawaida na kuwa nyeupe. Kulingana na watafiti kutoka Chuo kikuu cha Afya na Sayansi cha Oregon, kiasi cha piperine cha pilipili manga kinaweza kuchochea ngozi kuzalisha pigment ziitwazo melanocytes. [9] Tiba ya ugonjwa wa vitiligo ya piperine pamoja na tiba ya asili ya kupunguza athari za mionzi mikali ya jua (ultraviolet) ni bora zaidi kuliko tiba zinazotegemea kemikali.
Pia hupunguza uwezekano wa kansa ya Ngozi kutokana na mionzi mingi sana ya Jua.
.
Pia hupunguza uwezekano wa kansa ya Ngozi kutokana na mionzi mingi sana ya Jua.
.
Maoni
Chapisha Maoni