Chai ya Limao Tangawizi: Faida na Jinsi ya Kuiandaa

Watu wengi wamehamia kwenye chai ya limao tangawizi kuimarisha afya zao, kutokana na uwezo wake wa kuamsha mfumo wa kinga mwilini, kushusha homa, kuimarisha kumbukumbu, kuweka sawa sukari ya damu, msaada kwenye mmeng'enyo, hupoozesha maumivu, na kuimarisha nywele zenye afya na ngozi.

Faida za Chai ya Limao Tangawizi

Limao na Tangawizi vyote uhesabika kuwa na athari za kuondosha na kuimarisha mfumo wa kinga mwilinin na sifa hizi husaidia kuamsha mfumo wa kimetaboliki. Mbali na yenyewe kuitwa chai, chai hii ya limao tangawizi kiukweli ni mchanganyiko wa maji ya limao na tangawizi, na hakuna utaalamu wowowe  unaofanyika kuongeza majani ya chai. Hatahivyo, hii haifanyi kutokuwa na nguvu kwenye afya yako. Kwa maelfu ya miaka, limao na tangawizi  vimekuwa vitu muhimu kwenye tiba za kitamaduni, na kipindi zikitumika binafsi, kila moja inaweza kuleta matokeo mazuri kwenye mwili. Hatahivyo, kipindi viungo hivi viwili vikichanganywa kwenye kinywaji, huwa vinakuwa na umuhimu zaidi kwa afya. [1]


Faida za Chai ya Limao Tangawizi

Tutazame kwa ukaribu kwenye faida za kiafya zilizo muhimu zaidi za mchanganyiko huu usio wa kawaida!

Hutibu Kichefuchefu & Shida ya Mmeng'enyo

Tangawizi ina kiongezo chenye nguvu sana, kinaitwa zingiber, ambacho kina uwezo wa kuondoa kabisa vijidudu vya bacteria ambavyo mara nyingi hushambulia tumbo na kuzorotesha kazi za mmeng'enyo wa chakula. Tngawizi pia hujulikana kwa kupunguza kichefuchefu na kukata kutapika, hata kwenye ujauzito, kulingana na jaribio lililochapwa kwenye jarida la Obstetrics & Gynecology. [2] Pia huimarisha mmeng'enyo mzuri na virutubisho kufyonzwa vizuri. Kulingana na jaribio lingine lililochapwa kwenye jarida la National Library of Medicine Journal, gram 1 tu ya tangawizi inaweza kusaidia kupunguza au kuondoa kichefuchefun cha namna yoyote. [3] Limao, kwa upande mwingine, ipo na mahusiano ya karibu ya kupunguza shida ya mmeng'enyo na kiungulia. Ijapokuwa limao lina acid kiuhalisia, likichanganywa na maji linaweza kuwa na athari za kialkali kwenye mfumo wa umeng'enyaji. [4]


Huimarisha Kumbukumbu

Limao na tangawizi husaidia kuimarisha umakini na kumbukumbu. Kuna utafiti unaoonyesha kwamba tangawizi ni kuimarisha kumbukumbu kwa wanawake waliozeeka kidogo kwani ina uwezo wa kupoozesha neva za fahamu na kuimarisha hisia. [5] Athari za kiondosha sumu huondoa uwezekano wa sumu kuwepo kwenye mwili. Kwenye jaribio lingine lililochapwa kwenye jarida la British Journal of Nutrition, maji yenye citric acid, yakiwemo maji ya limao, yameonekana kutoa msaada mkubwa kwa damu kusafiri kwenda kwenye ubongo, na hatimaye kuimarisha uwezo wa kumbukumbu na akili. [6] Kwahiyo basi, haina haja ya kuendelea kusema kwamba limao na tangawizi vinaweza kuongeza uwezo wa ubongo kukumbuka vizuri. 

Matunzo ya Ngozi 

Jaribio mojawapo kwenye jarida la   Journal Food Chemistry linaonyesha kwamba vyakula vyenye tangawizi ni chanzo kizuri cha viondosha sumu. [7] Limao ni chanzo cha utajiri wa vitamin C, ambayo hufahamika kwa sifa zake za kukinzana na uzee. [8] Kwahiyo, kiwango cha juu cha vitamin cha limao na tangawizi, kinapochanganywa na viondosha sumu kadhaa, hufanya mchanganyiko huu  kuwa chaguo bora kwa kuimarisha afya ya ngozi. Unaweza kunywa chai hii au hata kuipakaa juu ngozi kuondoa muwasho. Viondosha sumu husaidia kupunguza uwezekano wa ngozi  kushambuliwa na sumu na kushawishi ukuaji wa seli mpya za ngozi, wakati huo huo chai hii ina uwezo wa asili wa kuzuia bakteria na virusi na kuzuia ngozi na maambukizi.  


Kupungua Uzito 

Tangawizi huchukuliwa na wengi kuamsha kazi za kimetaboliki na pia husaidia kutuliza hisia za njaa. Maji ya limao, pia, yana athari hizo hizo. Kulingana na jaribio la mwaka 2016 lililochapwa kwenye jarida la International Journal of Nursing Research and Practice, wakati wanafunzi manesi 30 wa kike  waliopitiliza uzito walipewa maji ya limao ya vuguvugu kwa wiki 3, walipoteza kati ya kilo 1 na 4 za uzito, na mzingo wa viuno vyao vilipungua kwa sentimeta 4-6. Kwahiyo, bilauli moja ya chai ya limao tangawizi asubuhi inaweza kusaidia wale wanaoitajin kupunguza uzito, kimsingi kwa kunywa chai hii itawafanya itakuwezesha kuunguza kalori kwa siku na kuzuia tamaa ya kula kila mara baada ya kula. [9] 

Matunzo ya Nywele

Ushahidi usio rasmi unaonyesha kwamba limao na tangawizi zote zimekuwa zikitumika kwa afya ya nywele kwa karne nyingi. Chai hii ina viwango vya juu vya vitamin A and C, vyote vina mahusiano ya kuimarisha afya ya nywele, kupunguza ukavu wa ngozi, na mba. Hii inaweza kusaidia kuzifanya nywele kuwa imara na kuzipa muonekano mzuri. Kwa kusemwa hayo, hakuna ushahidi wa kisayansi unaokubaliana na faida za chai ya limao tangawizi kwa nywele na kwa maana hiyo utafiti zaidi unahitajika.

Huimarisha Mfumo wa Kinga Mwilini

Kulingana na jarida la International Journal of Preventive Medicine, tangawizi ina sifa za vizuia uvimbe mwilini na vizuia sumu zinazoimarisha na kuamsha mfumo wa kinga mwilini. Malimao yana vitamin C, ambayo hufanya kazi kama kinga kizuizi dhidi ya maradhi tofauti tofauti. Vyote kwa pamoja limao na tangawizi vinajulikana dunia nzima kama visaidizi vya mfumo wa kinga mwilini, kwahiyo inatengeza hoja iliyo makini kwamba chai ya limao tangawizi inaweza kukulinda dhidi ya vijidudu vya maradhi na ugonjwa. Kipindi unasumbuliwa na homa au mafua, fanya kunywa  kikombe 1 au viwili vya chai hadi dalili zipotee na ndipo utakapoanza kuona mabadiliko na kupungua kwa muwasho kwenye njia zako za hewa. Hatahivyo, mara zote hushauriwa kupata ushauri wa daktari kwa dozi kamili kwani ukizidisha dozi itasababisha madhara. [10] [11]

Hudhibiti Kisukari

Linapokuja swala la kudhibiti sukari ya damu , tangawizi husaidia kupunguza hatari ya baadhi ya matatizo sugu ya kisukari, kama jaribio  [12] lililochapwa kwenye jarida la Iranian Journal of Pharmaceutical Research mwaka 2015. Kwa kuweka sawa utoaji wa insulini na sukari ya damu kwenye mwili wako, unaweza kuzuia kupanda na kushuka kwa sukari ya damu ambapo kunaweza kupelekea kupata ugonjwa wa kisukari au kumuathiri yule ambaye anao ugonjwa huu tayari.Taasisi ya Ugonjwa wa Kisukari Marekani [13] pia imedai kuwa malimao ni chakula kizuri kwa wenye kisukari. Kwahiyo jitengenezee mwenyewe kikombe cha chai ya limao tangawizi sasa!

Hutuliza Maumivu

Asili ya kuzuia uvimbe ya tangawizi haipunguzi tu muwasho, uvimbe, na kuumuka kwenye mwili bali pia inaweza kufanya kazi kama dawa ya kutuliza maumivu.  Jaribio lingine lililochapwa  kwenye jarida la National Library of Medicine limeonyesha kwamba kipindi gram 2 za tangawizi zilipoliwa kwa siku 11, maumivu ya misuli yaliyosababishwa na ufanyaji wa mazoezi uliokithiri yalipungua. Kwa maana hiyo, unywaji wa chai ya limao tangawizi unaweza kukusaidia kupona dhidi ya maumivu ya mwili, maumivu ya hedhi, homa, na upasuaji. [14] [15]

Namna ya Kuandaaa Chai ya Limao Tangawizi?

Kwenye kipindi cha baridi, hakuna kitu kinachoshinda kifua na homa zaidi ya unywaji wa chai ya tangawizi. Mchanganyiko wa limao na tangawizi husafisha njia za pua (sinuses) na kupunguza mikwaruzo na muwassho kwenye koo la hewa. Kwahiyo bila kupiga porojo nyingi, embu tuangalie hatua kwa hatua za kuandaa chai ya limao tangawizi ukiwa nyumbani.

Mahitaji

  •  Vikombe vya maji 3
  •  majani ya chai(kijiko cha chai) (kwa kila kikombe)
  • tangawizi iliyosagwa vizuri (kijiko cha chai) 
  • Maji ya limao (kijiko cha chai)
  • Asali/sukari kijiko cha chai

Maelekezo

Kuandaa chai ya limao tangawizi, kwanza, chemsha vikombe 3 vya maji kwenye sufuria.
  • Ongeza tangawizi iliyosagwa kwenye maji na iache ichemke.
  • Inapoanza kuchemka, ongeza maji ya limao na majani ya chai uache mchanganyiko huu uchemke kwa dakika 15-20 kwenye moto mdogo.
  • Unaweza kuongeza asali kama unapenda, lakini mchanganyiko wa limao na tanagwizi una ladha ya kipekee nzuri na tamu. Furahia chai yako ya moto.

Nyongeza

Unaweza pia kuongeza kidogo mdalasini, mwishoni, kuongezea ladha, kama ukipenda.
Unaweza kuongeza binzari kidogo kama ukitaka, kwani ina uwezo wa kuzuia mwili kuvimba (anti-inflammatory properties).
Unaweza kuongeza matone ya maji ya chungwa kwenye chai kama ladh ya limao ni kali sana. Chungwa litaifanya chai yako kuwa tamu. 

Maoni