Kinywaji kipi na Chakula gani kizuri kwa Vidonda vya tumbo (Ulcers)?
Maji yasiyo na chochote kiujumla ni kitu kizuri sana kunywa kama una vidonda vya tumbo, wakati vyakula vyenye probiotic, bland foods, vyakula vyenye kiwango kikubwa cha nyuzi lishe (high-fiber), na baadhi ya matunda na mboga za majani ni muhimu. Tukigeuza upande mwengine, caffeine, pombe, na maziwa vinatakiwa uvikwepe vikiambatana na pilipili, vyakula vyenye asidi, fati, vilivyokaangwa, au vyakula vilivyosindikwa.
Makala hii inaelezea sababu, dalili na matatizo ya Vidonda vya tumbo (peptic ulcer). Pia inakupa orodha ya vyakula na vinywaji ambavyo ni vizuri na vibaya kwa ajili yako kama ukitambulika kuwa na vidonda vya tumbo (a stomach ulcer).
Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcers) ni nini?
Kidonda cha tumbo (a peptic ulcer) ni uvimbe uliowazi kwenye ukuta wa tumbo au duodenum (sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo unapoanzia). Kwenye utaalamu zaidi kidonda kinachotokea kwenye tumbo huitwa gastric ulcer, na kidonda kitokeacho kwenye duodenum huitwa duodenal ulcer. Kwa pamoja, hali hizi mbili hutambuliwa kama peptic ulcer disease.
Vidonda vya tumbo (Peptic ulcers) huathiri karibu watu milioni 4 nchini marekani Kila mwaka. Hutokea kipindi ukuta wa tumbo au duodenum umevunjwa kwa acid iliyopindukia na/au kuna upungufu ute ute (mucus) unaolinda kuta za tumbo au duodenum.
Kuna sababu nyingi za kuwepo kwa hali hii.
Sababu zilizo zoeleka
Watu wamezoea kufikiri vidonda vya tumbo husababishwa na msongo wa mawazo (stress). Lakini kilichokuja kujulikana, stress haionekani kuwa ndio sababu pekee kubwa iliyokuwepo.
Sababu zitoazo mara nyingi zinazoleta vidonda vya tumbo ni:
- Helicobacter pylori (H.Pylori): Huyu ni bacteria wa maambukizi ambaye anakula na kuondoa ute ute mwembamba unaolinda kuta za tumbo.
- Matumizi ya dawa za kutuliza maumivu za hospital : Dawa hizi kutoka hospital au tuseme dawa za kizungu za kutuliza maumivu zinapotumika kupitiliza. Hujumuisha aspirin, Aleve (naproxen), Advil (ibuprofen), na Celebrex (celecoxib).
- Zollinger-Ellison syndrome: Hii ni dalili adimu kutokea ambapo vivmbe kwenye kongosho au upande wa juu wa njia ya chakula huchochea uzalishwaji wa acid ya tumboni.3
Wakati vyakula "havisababishi" ulcers, kuna muda vinaweza kuamsha vidonda vya tumbo na kufanya hali kuwa mbaya zaidi.
Zipi ni dalili za Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcer)?
Dalili ya msingi ya Vidonda vya tumbo ni maumivu, mara nyingi huelelezwa na kiungulia katikati au sehemu ya juu ya tumbo. Maumivu huwa makali nyakati A usiku na mapema asubuhi wakati tumbo lipo tupu.
Dalili nyingine za Vidonda vya tumbo ni:
- Kuvimbiwa na gesi
- Kiungulia
- Kichefuchefu
Kama vidonda vimechachamaa na kusababisha kutokwa na damu, dalili zaweza kujitokeza, ambazo ni:
- Choo cheusi, kinachosababishwa na damu kutoka kwenye utumbo.
- Maumivu makali yenye kutesa, ya tumbo la chini ( abdominal pain ).
- Kutapika
- Kupungua uzito
Nini cha kunywa kwa Vidonda vya Tumbo
Kabla ya yote, kitu kizuri kuliko vyote kwa kunywa kama una vidonda vya tumbo ni maji. Huitaji maji yenye alkali au maji yoyote yale yaliyo spesho. Malengo makuu ni kujiweka na maji kuimarisha uponyaji na kusaidia kutuliza maumivu ya tumbo. Maji husaidia kuua nguvu za acid za tumbo.
.
Kuna watu hupendelea aina fulani ya vinywaji kusaidia kutibu vidonda vya tumbo au kupunguza maumivu. Vinywaji hivyo ni:
🌿Chai ya Chamomile
🌿Juisi ya Cranberry
🌿Chai kijani isiyo na caffeine (Decaffeinated green tea)
🌿Maji yenye asali
🌿Kefir
🌿Kombucha
🌿Chai ya manjno (Turmeric tea)
Je, unatakiwa unywe Maziwa kutibu Vidonda vya Tumbo ?
Kwa vizazi na vizazi, watu wenye Vidonda vya tumbo waliambiwa kwamba maziwa yangeweza kutuliza tumbo na hata kusaidia kwenye kutibu Vidonda vya tumbo. Walichonacho wanasayansi toka walipojifunza ni kwamba maziwa huchochea tumbo kuzalisha acid nyingi zaidi.
Kwahiyo yaweza onekana athari za kupoa za maziwa ni faida, yanaweza kuamsha vidonda vya tumbo na kufanya viwe hatari zaidi.
Maziwa yasiyo na lactose (Lactose-free) au maziwa ya soya (soy milk) yanaweza kuwa mbadala mzuri ambao hayawezi kuchochea vidonda vya tumbo.
Vinywaji Vingine vya Kuepuka
Hii iwe kama muongozo wa jumla, epuka vinywaji vyenye caffeine, vyenye acid, vilivyowekwa radha ya utamu, au pombe kama una vidonda vya tumbo.
Vinywaji vya kuviepuka ni pamoja na:
🌿Bia
🌿Chai nyeusi
🌿Vinywaji vyenye kabonidayoksaidi (Carbonated drinks)
🌿Kahawa (ikiwemo Kahawa iliyotolewa caffeine)
🌿Colas
🌿Chai ya kijani (Green tea)
🌿 Kakao ya moto (Hot cocoa)
🌿 Vinywaji vya kutia nishati (Energy drinks)
🌿 Juisi ya machungwa na Juisi nyengine za matunda machachu (citrus juices)
🌿Spirits
🌿Sweetened punches
🌿Juisi ya nyanya
🌿Mvinyo
Nini unapaswa kula kwa Vidonda vya Tumbo?
Iwe kama sheria, vyakula vyenye ladha iliyopoa vinatakiwa viliwe kipindi unapata nafuu ya kupona vidonda vya tumbo.
Probiotic bacteria kutoka kwenye vyakula vilivyolala (fermented foods) vinaweza kufyonza acid y tumbo iliyozidi.
Vyakula ambavyo vinaweza kusaidia kuponesha vidonda vya tumbo ni:
🌿Apples
🌿Ndizi
🌿Maharage na legumes
🌿Bell peppers
🌿Blackberries
🌿Blueberries
🌿Broccoli
🌿Cabbage
🌿Carrots
🌿Cauliflower
🌿Cherries
🌿Samaki
🌿Asali
🌿Leafy greens
🌿Miso
🌿Oatmeal
🌿Raspberries
🌿Raspberries
🌿Sauerkraut
🌿 Nyama ya kuku isiyo na ngozi
🌿Strawberries
🌿 Nafaka zisizokobolewa kama ngano, na mchele wa kahawia ( uliotwangwa na si uliokobolewa)
🌿tambi zilizotomana na nafaka isiyokobolewa na mkate pia.
🌿 Maziwa ya mtindi ( yenye fati kidogo, yasiyo matamu)
(Vyakula vilivyoandikwa kwa kiingereza vinaeleweka kuliko vingeandikwa kwa kiswahili)
Vyakula vya Kuepuka
Vyakula vyenye fati, vilivyokaangwa kwa mafuta, vilivyosindikwa, au vyenye acid vinatakiwa kuepukwa kama una vidonda vya tumbo. Vyakula hivi haviendi kuumiza vidonda pekee lakini pia vinaweza kuamsha uvimbe ambao unaharibu uzalizhwaji wa kawaida wa uteute wa tumbo (stomach mucus).
Vyakula vya kuviepuka ukiwa na vidonda vya tumbo ni:
🌿 Vyakula vya kuoka kama cupcakes na pastries
🌿Cheese
🌿Cream soups
🌿Citrus fruits kama machungwa, nanasi n.k
🌿Chocolate
🌿Fast foods, ikiwemo pizza
🌿 Vyakula vya kukaangwa na mafuta, ikiwemo chips, kuku waliokaangwa na maandazi.
🌿Gravy, sauces, salsas, na salad dressings
🌿Ice cream, custards, na puddings
🌿Nanasi
🌿Nyama za kusindikwa, kama hotdogs, bacon sausages, na salami
🌿Nyama nyekundu
🌿 Vyakula vya pilipili, ikiwemo chili sauce
🌿 Nyanya, tomato sauces, na supu za nyanya.
Kupona kwa Vidonda vya Tumbo
Vidonda vya tumbo huchukua wiki kadhaa kupona kukiwa na matibabu. Daktari wako atakupa dawa za kusaidia kupona, ikiwemo
antibiotics ya kuponya maambukizi ya H. pylori na vizuia histamine-2 (H2) au proton pump inhibitors (PPIs) kupunguza uzalizhwaji wa acid.
Madhara ya Vidonda vya Tumbo
Vikiachwa bila kutibiwa, vidonda vya tumbo vinaweza kupelekea madhara makubwa, kuna ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa maisha. Madhara haya ni:
⚠️Gastrointestinal bleeding: Huku ni kuvuja kwa damu ndani ya utumbo; damu inaweza kuvuja taratibu au kwa kasi na kusababisha anemia (kukosekana kwa chembe nyekundu za damu zilizobeba oksijeni) au tatizo la hemorrhage (kutokwa na damu nyingi kutoka kwenye tishu iliyoharibika)
⚠️Gastric outlet obstruction. Hii ni hali ya kufungwa kwa njia inayotoka tumboni kwenda kwenye utumbo mdogo
⚠️Gastric perforation: Hii hutokea kipindi vidonda vya tumbo vinatengeneza shimo kote kwenye kuta za tumbo
Muda upi wa kukimbilia Hospital?
Piga simu ya dharura au pata mtu kukuwahisha hospital aukwenye chumba cha dharura kilichopo karibu kama unaonesha dalili mbaya za kutokwa na damu, kama;
⚠️ Kutapika damu
⚠️Choo cha damu
⚠️ Maumivu makali ya tumbo
⚠️Clammy skin (hali ya ngozi kuwa na majimaji yenye kunata katika hali isiyopendeza)
⚠️Mapigo ya moyo yanaenda kasi kuzidi kawaida.
⚠️ Kizunguzungu au kuzimia.
Maoni
Chapisha Maoni