Faida 10 za Kiafya za Asali na Mdalasini

 

Faida 10 za Kiafya za Asali & Mdalasini

Faida za kiafya za mchanganyiko wa Asali na mdalasini huweza kujumuisha uwezo wake wa kuimarisha mfumo wenye nguvu zaidi wa kinga na umeng'enyaji chakula, kuimarisha afya ya moyo, kuimarisha mifupa, ngozi, meno, na afya ya nywele,vile vile kuchochea kupungua uzito. Pia husaidia kutoa afueni kwenye miwasho na dalili za ugonjwa wa baridi yabisi (arthritis). Makala hii imesheheni faida za Kiafya za asali na mdalasini zikiwa zimechanganywa. [1]

Asali huja na faida za kiafya kadha wa kadha inapotumiwa yenyewe peke yake, na pia ikitumiwa kwenye mchanganyiko na vyakula vingine, michanganyiko mizuri zaidi hutokea ikichanganywa na mdalasini, tangawizi, na maziwa.

   

Thamani ya Virutubisho vya Asali & Mdalasini 

Asali na mdalasini vyote ni vyakula vyenye virutubisho na vimesheheni vitamini na madini ambayo husaidia kubakisha afya nzuri. Mchanganyiko huu una virutubisho vikiwemo maji, protini, nyuzi lishe (fiber), sukari, vitamini, na madini. Mdalasini pia una kiwango kidogo sana cha fati. [2] [3]


Madini kama calsium, madini joto (iron), sodium, phosphorus, na zinc hupatikana kwenye asali na mdalasini. Kwenye upande wa vitamini, mchanganyiko huu una vitamini C, vitamini B6, folate, niacin, na riboflavin. Mdalasini pia una vitamini A,E,D, na K.   

Faida za Kiafya za Asali &  Mdalasini

Faida za mchanganyiko wa Asali na Mdalasini hujumuisha yafuatayo: [4] [5]

Unaweza Kuhuisha Kinga ya Mwili 

Mchanganyiko wa asali na mdalasini ni mzuri kwa kuamsha mfumo wa kinga ya mwili, kuondoa uchovu uliokithiri, na kuongeza umri wa kuishi kwa watu. Unaweza pia kutumika kwa kutibu homa na mafua. Hii yawezekana labda kwa uwepo wa viondosha sumu ambavyo vipo kwenye mdalasini na asali ambavyo vinaweza kuungana na kushambulia sumu huru kwenye mifumo ya viungo vya mwili. [6]

Inaweza kudhibiti Kisukari 

Mdalasini una viondosha sumu vya  flavonoids ambavyo athari yake inaukaribu na ufanano na insulini, ambayo inamaanisha inaweza kuchochea glucose kutoka kwenye damu na kuingia kwenye seli ambapo huitajika kwa ajili ya nishati. Asali, kama chanzo asilia cha sukari, haisababishi kufurika kwa viwango vya sukari kwenye damu ambapo vyanzo vingi visivyo asilia vya sukari hufanya hivyo, na athari za mdalasini, inapochanganywa nayo, huonyeaha matumizi ya haraka ya glucose kwenye mwili, na kuimarika kwa aina ya pili ya kisukari, kama jaribio lililochapwa kwenye jarida la American Diabetes Association mwaka 2003. [7]

 Hutibu Muwasho

Mchanganyiko uliotokana na asali na mdalasini mara nyingi hutumika kutibu palipong'atwa na mdudu na kuondoa uvimbe kwenye chanzo. Mdalasini yawezekana ukatambulika kama kitu cha kuondoa uvimbe, wakati asali yenyewe ni kizuia vijidudu vya magonjwa na kiungo kinachofaa kuwekwa kwenye bidhaa nyingi za urembo. Kwahiyo, mchanganyiko wao hufanya kazi kwenye mambo yote yahusiyo muwasho wa ngozi na ming'ato ya wadudu wakati huo huo, wakati ukikuzuia usipate maambukizi. [8] [9]


Husaidia Kwenye Mmeng'enyo 

Asali na mdalasini vinaweza kusaidia kuongeza afya na utendaji kazi wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Inaweza kuondoa gesi tumboni na utumbo na kutibu hali kutomeng'enywa chakula, na maambukizi ya kibofu. Ulaji wa mara kwa mara wa mdalasini na asali utakusaidia Kubakisha mmeng'enyo wenye afya, ambao hulinda mfumo wa utumbo dhidi ya magonjwa mengi hatarishi. [10]


Hutibu Baridi Yabisi (Arthritis)

Asali na mdalasini vina faida kwenye kutoa nafuu dhidi ya baridi yabisi. Ulaji wa mchanganyiko wako wa mara kwa mara husaidia kuimarisha afya ya mfupa na kuondoa maumivu kwenye maungio. Unaweza pia kuchanganya asali na unga wa mdalasini kwenye maji ya moto kiasi na ukafaidi zao lake. [11]


Husaidia kutunza ngozi 

Faida za asali na mdalasini zimejitanua kwenye matunzo ya ngozi vilevile, ambapo maambukizi madogo ya ngozi na chunusi yanaweza kutibiwa kwa kupakaa mkorogo unaotokana na vyakula hivi vya kipekee. Unaweza kupakaa kwenye majeraha au kwenye ngozi kama mafuta yako ya kawaida kutokana na uwezekano wa tabia za kuzuia uvimbe, kuzuia vimelea vya magonjwa, na kuondoa sumu, ambazo zinaweza kupunguza makunyanzi na madoa yanayohusiana na uzee kwa kupunguza athari za sumu huru(free radicals) kwenye ngozi. [12


Inaweza Kuzuia Magonjwa ya Moyo 

Asali na mdalasini hutumika kupunguza viwango vya cholesterol na kwa maana hiyo hutoa nyongeza ya ulinzi kwa moyo wako. Uwezekano wa kiwango cha juu cha cholesterol (LDL au cholesterol mbaya) kinaweza kupelekea ugonjwa wa atherosclerosis au kujengeka kwa mafuta yabisi kwenye kuta za ateri na mishia mengine ya damu, hivyo kuongeza uwezekano wa damu kushindwa kupita ambayo hupelekea kwenye mshtuko wa moyo au ugonjwa wa stroke. [13]


Inaweza Kusaidia Kwenye Kupunguza Uzito 

Mchanganyiko wa asali na mdalasini kwenye maji ya moto kiasi huchukuliwa kama kifaa kizuri Cha kupunguza uzito. Bila shaka, kama tiba nyingine za kupunguza uzito, matokeo huonekana tu ukichanganya na chakula kilichopangiliwa na mazoezi ya mara kwa mara. [14

Inaweza Kusaidia Kwenye Kutunza Nywele

Asali na mdalasini hutunza nywele, hupunguza kupotea kwa nywele na hukuza nywele. [15]

Inaweza Kusaidia Kwenye Matunzo ya Meno 

Zote asali na mdalasini kila moja ikiwa peke yake hutumika kwenye matunzo ya meno. Na mchanganyiko ulioandaliwa kutokana na viwili hivi pia hutumika kwenye matunzo ya meno, hasa kwenye kuondoa Harufu mbaya na maumivu ya meno. [16]

Pia huaminika kwamba asali na mdalasini inaweza kusaidia kwenye kutibu ugumba kwa wanaume, na matatizo ya kusikia, lakini uchunguzi zaidi unahitajika kuhusiana na madai hayo. Hadi hapo furahia faida hizi na kuwa na afya zaidi!

     













Maoni