Chlamydia: Sababu, Dalili na Tiba Asilia

 

Maambukizi ya Chlamydia : Sababu Dalili & Tiba 

Chlamydia ni ugonjwa ambao husambaa kwa urahisi na una dalili hafifu au hauna dalili kabisa. Hali hii hufanya kuwa wa muhimu kujua sababu zake na dalili za ugonjwa huu ili wengi katika sisi kuuzuia.

Chlamydia ni nini?

Chlamydia ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya zinaa, sexually transmitted disease (STD), ambao husababishwa na bacteria maalumu wanaoitwa Chlamydia trachomatis. Ni gonjwa la zinaa linaloripotiwa kwa upana, kwa karibia kesi milioni 1 kwa marekani ya kaskazini pekee. Ijapokuwa moja ya hadithi za kufikirika za Chlamydia ni kwamba haiwezi kutibika, ambayo no uongo; antibiotics zinaweza kutumika kuuondoa ugonjwa huu kwenye mwili. Kwa kusemwa hivyo basi, ugonjwa uliokaa muda mrefu bila matibabu unaweza kusababisha athari na Madhara ya kudumu.[1]

Kwa wanawake, hata hivyo, dalili hazionekani kirahisi, ndio maana ni rahisi mno kuusambaza kwa  bila kujua kwa wanaume. Hata hivyo, kiumeni, hujionyesha kwa Kutokwa na Ute mweupe kipindi Cha kukojoa. Kama unaona alama na dalili za chlamydia, wasiliana na na daktari wako mara moja. 


Chlamydia ni ugonjwa wa  kawaida wa zinaa ambao unaweza kuwapata  wote mwanaume na mwanamke. Photo Credit: iStock

Sababu

Chlamydia husababishwa na seli ndogo sana zinazoishi bacteria wanaoitwa Chlamydia trachomatis  ambao  huishi kwenye mji wa mimba (uterus), uke (vagina), mlango wa mji wa mimba (cervix), urethra, puru (rrectum), na muda mwengine pia kwenye koo na  macho.  

  • Ngono isiyo salama: Ni ugonjwa unaoenezwa kwa zina, sexually transmitted disease (STD) na kwa maana hiyo yeyote ambaye anafanya ngono isiyo salama au akagusanisha viungo vyake vya siri na aliyeathihirika, yupo kwenye hatari ya kupata Chlamydia. Inaweza kusambazwa kwa njia ya mapenzi ya mdomo (oral sex) au kinyume na maumbile ( anal sex) na mtu aliye athirika. [2]
  • Vertically transmitted: Inaweza pia kuambukizwa kwa mtoto kipindi cha ujauzito kama mama ameathirika na bacteria na hana taarifa kama ameathirika.

Dalili

Maambukizi ya bacteria Chlamydia mara nyingi hufahamika kama muuaji mkimya (silent killer) kwa wanawake, kwani huanza na dalili za kudharaulika, ambazo, zikiachwa bila kutazamwa, zinaweza kuleta balaa zito kwa afya yako. Dalili unazohitaji kuzitambua kwa ugonjwa wa Chlamydia ni:- . [3]

Dalili za Kawaida 

  • Unahisi hali ya kuungua na maumivu kipindi unakojoa.
  • Unatokwa na uchafu wa njano au mfano wa maziwa (kutoka kwenye uume au uke)

Kwa wanawake

  • Kushindwa kujizuia mkojo. 
  • Maumivu wakati wa kujamiiana.
  • Kutokwa na damu kipindi cha kujamiiana.
  • Maumivu sehemu ya chini ya mgongo na chini ya kitovu. 
  • Uzito kwenye nyonga 
  • Homa

Kwa wanaume

  • Kuvimba kwenye eneo la korodani.
  • Maumivu ndani na  kuzunguka korodani 
  • Kuwasha na kuuma kwenye ncha kichwa cha uume. 

Kama ukiachwa bila kutibiwa, ugonjwa wa chlamydia unaweza kusababisha ugumba, PID, na bartholinitis kwa wanawake. Kwahiyo uchunguzi wa kina wa tatizo ni muhimu sana.  


Kwa tiba asilia na ushauri :
Tabibu Kweli
Tanzania 🇹🇿
Tiba Asili
Whatsapp: +255658674553
Call: +255766107722













Maoni