Fahamu Kila Kitu Kuhusu Bawasiri

 


Bawasiri (Piles au hemorrhoids) ni mkusanyiko wa tishu zilizovimba/kuumuka ndani ya njia ya haha kubwa. Zina mishipa ya damu, tishu zinazosapoti, misuli, na nyuzinyuzi zenye kuvutika.

Watu wengi wana bawasiri, lakini dalili haziwezi kufanana mara zote. Bawasiri huonesha dalili walau kuanzia asilimia 50 ya watu wa Marekani kabla ya umri wa miaka 50.

Makala hii itaielezea bawasiri, sababu zinazopelekea kupata ugonjwa huu, namna ya kuufahamu, ngazi zake, na namna ya kutibu, na athari gani gani zinaweza kuleta kwenye mwili.

Ukweli wa Haraka Kuhusu Bawasiri:

  • Bawasiri ni mkusanyiko wa tishu na mishipa ya damu ambayo huumuka na kuvimba.
  • Ukubwa wa bawasiri unatofautiana, na hupatikana ndani na nje ya mkundu.
  • Bawasiri hutokea kutokana na tatizo la kuvimbiwa lililo komaa, tatizo la kuharisha lililo komaa, mazoezi ya kunyanyua vitu vizito, ujauzito, au kujikamua wakati kinyesi kinapotoka.
  • Daktari mara nyingi hutambua bawasiri kwa vipimo.
  • Bawasiri hupewa ngazi kwenye vipimo kuanzia I hadi IV. Kwenye ngazi ya III au IV, upasuaji unaweza kuhitajika.

Bawasiri ni Nini?



Bawasiri ni mkusanyiko wa tishu zilizoumuka na kuvimba kwenye eneo la haja kubwa.

Zinaweza kuwa na ukubwa tofauti tofauti, na zinaweza kuwa ndani au nje.

Bawasiri za ndani hupatikana kati ya sentimita(cm) 2 na 4 juu ya uwazi wa mkundu, na huwa ni za aina moja. Bawasiri ya nje ya ncha ya mkundu.

Dalili

Kwenye kesi nyingi, dalili za bawasiri hazina ugumu kuzitambua. Mara nyingi hujionesha baada ya siku chache.

Mtu mwenye bawasiri huweza kuwa na dalili zifuatazo:

  • Kuhisi uvimbe mgumu unaouma kuzunguka mkundu (njia ya haja kubwa). Uvimbe huo unaweza kuambata na damu. Bawasiri zinazoambatana na damu zinaitwa thrombosed external hemorrhoids.
  • Baada ya kinyesi kutoka, mtu mwenye bawasiri anaweza kuhisi bado kinyesi hakijaisha kwenye utumbo mkubwa.
  • Damu nyekundu hasa huonekana baada kinyesi kutoka.
  • Eneo kuzunguka mkundu huwasha, nyekundu, na kuuma.
  • Maumivu hutokea kipindi kinyesi kinapotoka.

Bawasiri inaweza kwenda na kuwa mbaya zaidi. Ikiwemo:

  • kutokwa na damu nyingi mkunduni, pia hupelekea kutokea kwa anemia.
  • maambukizi
  • Kutokuwa na uwezo wa kudhibiti mwendo wa njia ya chakula (bowel movements)
  • Fistula ya njia ya haja kubwa, ambapo mfereji hutengenezwa kati ya ngozi karibu na mkundu na ndani ya haja kubwa.
  • Bawasiri aina ya strangulated hemorrhoid, ambapo hukatisha usambaaji wa damu kwenye bawasiri, kusababisha matatizo yakiwemo maambukizi au damu kuganda.

Bawasiri imegawanyika kwenye ngazi nne:

  • Ngazi ya I: Kuna vivimbe vidogo, mara nyingi ndani ya kuta za mkundu. havionekani.
  • Ngazi ya II: Bawasiri ngazi ya II ni kubwa kuliko ngazi ya I, lakini pia ubakia ndani ya mkundu. Vinaweza kusukumwa nje kipindi kinyesi kinapopita, lakini hurudi bila kusaidiwa.
  • Ngazi ya III: Bawasiri hii pia hufahamika kama prolapsed hemorrhoids, na huonekana nje ya mkundu. Mtu huhisi vivimbe hivi kuning’inia kutoka kwenye puru, lakini vinaweza kurudishwa ndani.
  • Ngazi ya IV: Vivimbe hivi haviwezi kurudishwa ndani na huitaji matibabu. Ni vikubwa na hubakia nje ya mkundu.

Bawasiri ya nje hutengeneza vivimbe vidogo nje tu ya mkundu. Vinawasha sana na vinaweza kuuma sana kama kukitokea kuganda kwa damu, kwani kuganda kwa damu kunaziba mzunguko wa damu. Bawasiri za nje (Thrombosed external piles), ambazo zimegandisha damu, zinahitaji matibabu.

Sababu



Bawasiri husababishwa na ongezeko la shinikizo kwenye puru.

Mishipa ya damu kuzunguka mkundu na ndani ya puru itajivuta kwa shinikizo na inaweza kututumka au kuumuka, kutengeneza bawasiri. Hali hii inaweza kutokana na:

  • Tatizo sugu la kuziba choo (chronic constipation)
  • Ttaizo sugu la kuharisha (chronic diarrhea)
  • Kunyanyua vitu vizito
  • Ujauzito
  • Kujikamua kipindi unajisaidia haja kubwa.

Tabia ya kupatwa na bawasiri pia yaweza kuwa ni ya kurithi na huzidi kadri umri unavyoongezeka.

Utambuzi

Mara nyingi daktari hutambua bawasiri baada ya kuukagua mwili. Watakagua mkundu wa mtu kwa bawasiri wanazohisi kuwa unazo.

Daktari anaweza kukuuliza maswali yafuatayo:

  • Una ndugu wa karibu wenye bawasiri?
  • Kumeshawahi kuwepo kwa damu au kamasi kwenye kinyesi?
  • Hivi karibuni uzito wako umepungua?
  • Utaratibu wako wa kujisaidia haja kubwa umebadilika siku za karibuni?
  • Kinyesi kina rangi gani?

Kwa bawasiri ya ndani, daktari atatumia kipimo kiitwacho digital rectal examination (DRE) au kutumia proctoscope. Proctoscope ni bomba nyembamba iliyowekwa taa. Inamruhusu daktari kutazama mfreji wa mkundu kwa ukaribu. Wanaweza kucukua tisu kidogo kama sampo ndani ya puru. Sampo hii inaweza kupelekwa maabara kwa ajili ya uchunguzi .

Mtbibu anaweza kupendekeza kipimo kiitwacho colonoscopy kama mtu mwenye bawasiri anaonesha dalili ambazo zinapendekeza kuwepo kwa ugonjwa mwingine wa mmeng’enyo wa chakula, au kuonesha dalili zozote za hatari ya kuwepo kwa kansa ya utumbo(colorectal cancer).

Matibabu

Kwenye kesi nyingi, bawasiri hujitibu zenyewe bila kuhitaji matibabu ya aina yoyote. Hijapokuwa, baadhi ya matibabu yanaweza kusaidia kupunguza muwasho na kukerwa ambapo watu wengi hupatwa wanapopatwa na bawsiri.

Mabadiliko ya Mfumo wa Maisha



Daktari atapendekeza mabadiliko ya mfumo wa maisha kudhibiti bawasiri.

Chakula Bora: Bawasiri inaweza kutokea kutokana na ugumu wakati chakula kinapopita kwenye njia yake. Ugumu unapozidi ni matokeo ya kuvimbiwa(ugumu wa kupata choo). Mabadiliko ya chakula yanaweza kukifanya kinyesi kuwa cha kawaida na kilaini. Hii inahusisha ulaji wa fiber zaidi, kama vile matunda na mboga za majani, au kula vyakula vya nafaka isiyokobolewa (dona).

Daktari pia anaweza kumshauri mtu mwenye bawasiri aongeze kiwango chake cha unywaji maji. Ni vyema kujizuia kutumia caffeine.

Uzito wa Mwili: Kupunguza uzito husadia kupunguza uwezekano na ukali wa bawasiri.

Kuzuia Bawasiri, madaktari pia hushauri kufanya mazoezi na kujizuia kujikamua wakati wa kujisaidia haja kubwa. Mazoezi ni moja ya tiba kuu kwa bawasiri.

Tiba

Kuna dawa mbali mbali ambazo zinaweza kutatua tatizo la bawasiri. Dawa kama za kutuliza maumivu, mafuta ya kupakaa, cream, zinaweza kutuliza maumivu na uvimbe kuzunguka mkundu.

Dawa zinazopatikana hospitali (OTC) haziwezi kutibu bawasiri moja kwa moja lakini huweza kutibu dalili. Usitumie dawa hizi kwa zaidi ya siku 7 mfulululizo, kwa maana zinaweza kusababisha muwasho zaidi kwenye eneo na kufanya ngozi kuwa nyembamba. Usitumie dawa mbili au zaidi kwa mara moja isipokuwa upate ushauri wa kitiba kutoka kwa daktari.

Corticosteroids: Dawa hizi hupunguza uvimbe na maumivu.

Laxatives: Daktari anaweza kupendekeza laxatives kama mtu mwenye bawasiri anasumbuliwa na kutopata choo. Dawa hizi zinaweza kumsaidia mtu kupata choo kikubwa kirahisi eneo la chini la utumbo mpana.

Uchaguzi wa Upasuaji

Watu wenye bawasiri ni 1 katika 10 watakaoishia kuhitaji upasuaji.

Banding: Daktari hufunga mpira kwenye shina la bawasiri, kukata usambaaji wa damu. Baada ya siku chache, bawasiri inakatika yenyewe. Tiba hii hufaa kutibu bawasiri yenye hali ya ya chini ya ngazi ya IV.

Sclerotherapy: Unachomwa sindano yenye dawa kwenye bawasiri kuifanya inyauke. Hatimaye bawasiri hupotea. Tiba hiyo hufaa kwa bawasiri ngazi ya II na ya III na ni mbadala wa njia ya banding.

Infrared coagulation: Pia hujulikana kama infrared light coagulation, kifaa maalumu hutumika kuunguza tishu za bawasiri. Njia hii hutumika kutibu bawasiri ya ngazi ya I na ya II.

Hemorrhoidectomy: Tishu iliyozidi ambayo husababisha kuvuja damu huondolewa kwa upasuaji. Upasuaji huu hufanyika kwa njia tofauti tofauti na ganzi hutumika. Aina hii ya upasuaji ndio bora zaidi kwa kuondoa kabisa bawasiri, lakini kuna hatari ya kupata matatizo, yakiwemo matatizo ya kupata shida ya kupata choo kikubwa, na maambukizi kwenye njia ya mkojo.

Hemorrhoid stapling: Usambaaji wa damu huzuiliwa kwenye tishu za bawasiri. Kitendo mara nyingi hakina maumivu kama hemorrhoidectomy. Hatahivyo, njia hii hupelekea hatari ya bawasiri kujirudia na sehemu ya puru kujisukuma kutoka nje ya mkundu (Prolapse).

πŸ‰πŸ“πŸ“πŸ‰πŸ“πŸ‰πŸ“πŸ‰πŸ“πŸ‰πŸ“πŸ‰πŸ‰πŸ“πŸ“πŸ‰πŸ‰πŸ“

PILEX+
(Tiba ya Bawasiri)

⚫Ni dawa asili iliyofanyiwa utafiti wa hali ya juu yenye uwezo wa kutibu aina zote za bawasiri yaani bawasir ya nje na dawasiri ya ndani (internal and External hemorrhoids).

Dawa hizi:⤵⤵⤵

🌿➡️ Hutibu maumivu makali yatokanayo na bawasiri.
🌿➡️ Hutibu miwasho itokanayo na bawasiri.
🌿➡️Huondosha uvimbe/kinyama kitokanacho na bawasiri.
🌿➡️Huondosha kidonda na kutokwa na damu kutokana na bawasiri iliyopasuka yaani Thrombosed Hemorrhoid
🌿➡️ Hulainisha choo


Ni dawa yakupakaa na ya kunywa

⚫Asilimia 90 (90%) ya wateja wote waliotumia doze hii hawamalizi hata nusu doze tatizo huisha kabisa na kuendelea na shughuli zao kama kawaida. Dawa hii hutibu bawasiri ndani ya wiki moja na baadhi hutumia zaidi ya wiki moja kulingana na ukubwa wa tatizo

NB: Bawasiri ni katika magonjwa ambayo tiba yake husumbua sana hospital mpaka kupelekea watu kufanyiwa upasuaji mdogo lakini bawasiri haiishi kwa kufanyiwa upasuaji kwani huwa inarejea tena na inaweza kurejea kwa kasi zaidi na madhara zaidi kama ambavyo imeshuhudiliwa kwa wagonjwa wengi.

Kwa mahitaji ya dawa wasiliana nasi:⤵⤵⤵

Tabibu Kweli
Tiba Asili
Tanzania

+255 658 674 553

0658 674 553

Simu/ WhatsApp

NTAKUJIBU HARAKA

Tunapatikana jijini DAR ES SALAAM, TANDIKA KARIBU NA BENKI YA NMB na MBAGALA KIZUIANI . Kwa mteja unayeishi Dar es Salaam, ambaoye huna nafasi ya kufika ofisini kwetu, utaletewa dawa mahali popote ulipo kwa gharama yako ya usafiri. Kwa mteja unayeishi mkoani, utatumiwa dawa kwa njia ya mabasi. Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti. Kwa wateja waliopo Mombasa, watatumiwa dawa kupitia basi la TAHMEED. Kwa wateja waliopo jijini Nairobi, watatumiwa dawa kupitia basi la DAR EXRESS. Na kwa wateja waliopo ughaibuni, watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA ARAMEX au DHL Njia ya haraka ya kupata huduma na ushauri ni WHATSAPP kwa namba hii kama simu yako naina WHATSAPP eleza shida yako kwa sms ya kawaida nitakujibu  .

DAWA ZETU HIZI NI ZA ASILIA NA HAZINA KEMIKALI ZA VIWANDANI KARIBU NA ASANTE.

Jiunge na Channel yetu ya Telegram ,

LIKE Ukurasa wetu wa Facebook na

F OLLOW ukurasa wetu wa Instagram , Kwa updates za kila siku.

🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿 Tatizo la uzazi kwa Mwanamke bado ni Changamoto, pata dozi kamili kutibu matatizo ya vivimbe kwenye kizazi.

🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿

Soma:  https://afyakweli.blogspot.com/2022/05/chango-la-uzazi-ni-miongoni-mwa.html?m=1

















Maoni