Dawa ya kutibu PID (Pelvic Inflammatory Disease) kwa wanawake



Pelvic inflammatory disease (PID) ni maambukizi ya viungo vya uzazi vya mwanamke. Mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa. Dalili zake ni ikiwemo ya maumivu chini ya tumbo na uke kutema majimaji yenye halufu mbaya. Matibabu ya haraka ya PID, mara nyingi huwa ni antibiotics, husaidia kuzuia matatizo kama ya
ugumba. Mwenzi wako anatakiwa kupimwa na kutibiwa pia.


Pelvic inflammatory disease (PID) ni nini?

Pelvic inflammatory disease, au PID, hutokea kipindi viungo vya uzazi vya mwanamke vimepata maambukizi, Mfumo wa uzazi wa mwanmke ni sehemu ya mwili wa mwanamke inayohusika kwenye kubeba mimba na kupata mtoto.

Viungo vya uzazi vinavyoathiriwa na PID ni uterus, ovari na mirija ya falopian. Kipindi una PID, utahisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu. Pia unaweza kutokwa na majimaji yasiyo ya kawaida kutoka kwenye uke wako.

Unapataje PID?

Watu wengi hupata PID kupitia ngono isiyo salama, hata hivyo 15% ya maambukizi haya hayaenezwi kwa njia ya ngono. Ngono inaweza kuruhusu bakteria kuingia kwenye mfumo wa uzazi, ambapo wanaweza kuathiri viungo.


Je, naathirika vipi na ugonjwa wa PID (pelvic inflammatory disease) ?

PID inaeweza kuharibu maeneo ya mfumo wako wa uzazi, yakiwemo uterus, ovari, na mirija ya falopian. PID inaweza kuwa mbaya na kufanya upate shida ya kubeba mimba siku za usoni. PID pia inaweza kuleta kifurushi cha maambukizi kwenye nyonga kinachoitwa tubovarian abscess (TOA) ambayo, kama hakijatibiwa inaweza kufanya watu waumwe sana.



Nani yupo kwenye hatari ya kupata PID?

Upo kwenye hatari kubwa ya kupata PID kama :

  • Una maambukizi yaenezwayo kwa ngono (STIs), hasa gonorrhea au or chlamydia.
  • Una wapenzi wengi, au una mpenzi mwenye wapenzi wengi.
  • Ulishawahi kuwa na PID siku za nyuma.
  • Unafanya mapenzi kiholela na una umri chini ya miaka 25.

Ugonjwa wa PID (pelvic inflammatory disease) umeenea kwa kiasi gani?

Kila mwaka,zaidi ya wanawakezaidi ya milioni 1 wanaoishi Amerika ya Kaskazini, hupata PID, na zaidi ya wanawake 100,000 huwa tasa kwa sababu ya ugonjwa huu, ikimaanisha hawawezi kupata mtoto. Kesi nyingi za mimba iliyotungwa nje ya kizazi (ectopic pregnancy) pia ni matokeo ya PID. Ectopic pregnancy ni mimba ambayo mtoto huanza kutungwa na kukua nje ya uterus, kawaida hutokea kwenye mirija ya falopian. Mimba iliyotungwa nje ya kizazi ambayo haijafanyiwa matibabu inahitaji umakini wa matibbu ya dharura.

Kesi za PID zimepungua kwa miaka ya hivi karibuni. Sababu yaweza kuwa wanawake wanawake hupata vipimo vya mara kwa mara vya chlamydia na gonorrhea, maambukizi mama yanayopelekea kuleta PID.


DALILI NA SABABU

Nini kinacho sababisha pelvic inflammatory disease (PID)?

Bakteria wanaoingia kwenye njia ya uzazi mara nyingi husababisha PID (pelvic inflammatory disease). Bakteria hawa hupita kutokea kwenye uke(vagina), kupitia kwenye cervix, hadi kwenye uterus, mirija ya falopian na ovari, na kwenye nyonga.

Kawaida, bakteria wanapoingia kwenye uke, cervix huzuia wasisambae ndani zaidi kwenye viungo vingine vya uzazi. Lakini muda mwingine, cervix hupata maambukizi kutokana magonjwa yaenezwayo kwa kwa ngono STI kama gonorrhea na chlamydia. Ikitokea hali hiyo, cervix haiwezi kuzuia bakteria wasiingingie ndani zaidi.

Ugonjwa wa gonorrhea na chlamydia ambao haukutibiwa husababisha takribani 90% za kesi za PID. Sababu nyingine ni ikiwemo:

  • Kutoa mimba.
  • Kujifungua mtoto.
  • Upasuaji kwenye nyonga.
  • Uingizwaji wa kifaa cha mkojo, insertion intrauterine device (IUD), Hatari ni kubwa kwenye wiki chache za mwanzo baada ya insertion. Nyakati nyingi maambukizi haya huzuiliwa kwa kufanya vipimo vy magaonjwa ya zinaa kipindi cha uwekwaji wa IUD.

Je, kufanya douching husababisha ugonjwa wa pelvic inflammatory disease (PID)?

Tafiti nyingi za zimeripoti ushirika dhaifu sana kati ya douching na PID. Douching ni kitendo cha kuingiza vidole ndani ya uke kwa lengo la kujisafisha na kutoa maji maji yenye kuleta harufu isiyopendeza. Kitu kinachoweza kusemwa hapa ni kwamba kufanya douching kunaweza kukupelekea kupata maambukizi ya bakteria, kitaalamu inaitwa bacteria vaginosis, lakini kuna ushirika mdogo kati ya douching na PID.

Dalili za PID ni zipi?

Unaweza usigundue kama una PID. Dalili zinaweza zikawa za kawaida au usizigundue. Lakini pia dalili za PID zinaweza kuanza ghafla na haraka. Zinaweza kuwa:

  • Maumivu kwenye tumbo au chini ya kitovu, dalili kubwa na maarufu.
  • Kutokwa na maji maji yasiyo ya kawaida ukeni, mara nyingi huwa na rangi ya manjano au kijani yakiambatana na harufu isiyopendeza.
  • Homa
  • Kichefuchefu na Kutapika
  • Maumivu kipindi cha kujamiiana.
  • Maumivu wakati wa kukojoa
  • Mpangilio wa hedhi kuvurugik, au kutokwa na damu kidogo sana au kupatwa maumivu ya edhi mwezi mzima.
  • Maumivu upande wa juu kulia wa tumbo (right upper abdomen), si mara nyingi.
UTAMBUZI NA VIPIMO

PID (pelvic inflammatory disease) hutambuliwaje?

Kama unahisi dalili za PID, onana na mtoa huduma wa afya haraka. Haraka unavyotibiwa, ndivyo unapata nafasi kubwa ya kupata mafanikio ya kupona.

Mara nyingi, mtaalamu wa afya hutambua PID kupitia:

  • Matibabu yako ya siku za nyuma, ikiwemo kukuuliza maswali kuhusu afya yako kwa ujumla, shughuli za kujamiiana na dalili.
  • Kipimo cha nyonga kutazama viungo vyako vya uzazi na dalili za maambukizi.
  • Kipimo cha vaginal culture ( kutazama kama kuna uwepo wa bakteria ukeni )

Vipimo gani vingine naweza kufanya kutambua uwepo wa PID?

Tabibu wako anweza pia kuagiza:

  • Vipimo vya damu.
  • Kipimo cha mkojo ili kuondoa UTI  ( urinary tract infection), ambayo husababisha maumivu yaleyale ya nyonga.
  • Kipimo cha Ultrasound kupata picha ya mfumo wa uzazi.

Kwenye baadhi ya kesi, tabibu wako atashauri:

  • Endometrial biopsy kuondoa na kupima kiasi kidogo cha tishu kutoka kwenye endometrium, ukuta wa uterus.
  • Laparoscopy, upasuaji wa kutumia mikato midogo na kifaa chenye mwanga kutazama kwa ukaribu kwenye viungo vya uzazi.
  • Culdocentesis, sindano inachomwa kwenye uke ili kutoa majimaji kwa utafiti. Kitendo ni adimu sana kutumika kama kilivyokuwa kikifanyika, lakini muda mwingine husaidia.

Pelvic inflammatory disease (PID) inatibika vipi?

Tabibu wako atapendekeza utumie antibiotics za kumeza. Hakikisha unameza dawa zote,hata kama umeanza kujisikia afadhari. Mara nyingi, dalili za PID huondoka kabla ya ugonjwa kuisha. Tabibu wako atashauri urudi siku chache baada ya kuanza dozi. Wanaweza kutazama matibabu yanavyofanya kazi.

Baadhi ya watu humeza antibiotics na bado dalili zipo. Kama ikitokea hivyo, unahitajika kwenda hospitali kupata dawa kupitia IV. Pia unahitajika matibabu ya IV kama:

  • Ni mjamzito.
  • Una maambukizi makubwa na unaumwa sana.
  • Una abscess (mkusanyiko wa uteu ute mchafu, pus) kwenye mirija yako ya falopian au ovari.

Nitahitahiji kufanyiwa upasuaji kwa ugonjwa wa PID?

Upasuaji ni nadra sana kwa PID lakini unaweza kusaidia kwenye baadi ya kesi. Kama bado una dalili au abscess baada ya kutumia antibiotics, ongea na tabibu wako kuhusu upasuaji.

Tiba Asili na Isiyo na Madhara, Huitaji kufanya Upasuaji

Piga simu 0658 674 553 ,





0658 674 553

Simu/ WhatsApp

NTAKUJIBU HARAKA

Tunapatikana jijini DAR ES SALAAM,  . Kwa mteja unayeishi Dar es Salaam, ambaoye huna nafasi ya kufika ofisini kwetu, utaletewa dawa mahali popote ulipo kwa gharama yako ya usafiri. Kwa mteja unayeishi mkoani, utatumiwa dawa kwa njia ya mabasi. Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti. Kwa wateja waliopo Mombasa, watatumiwa dawa kupitia basi la TAHMEED. Kwa wateja waliopo jijini Nairobi, watatumiwa dawa kupitia basi la DAR EXPRESS. Na kwa wateja waliopo ughaibuni, watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA ARAMEX au DHL Njia ya haraka ya kupata huduma na ushauri ni WHATSAPP kwa namba hii kama simu yako naina WHATSAPP eleza shida yako kwa sms ya kawaida nitakujibu  .

DAWA ZETU HIZI NI ZA ASILIA NA HAZINA KEMIKALI ZA VIWANDANI KARIBU NA ASANTE.

Jiunge na Channel yetu ya Telegram ,

LIKE Ukurasa wetu wa Facebook na

F OLLOW ukurasa wetu wa Instagram , Kwa updates za kila siku.

🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿 Tatizo la uzazi kwa Mwanamke bado ni Changamoto, pata dozi kamili kutibu matatizo ya vivimbe kwenye kizazi.

🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿🌿

Soma:  https://afyakweli.blogspot.com/2022/05/chango-la-uzazi-ni-miongoni-mwa.html?m=1

Maoni