Faida 13 za Kiafya zilizo hakikiwa za Tende

 

Faida za kiafya za Tende za nguvu zikiwemo kuimarisha nishati ya mwili, kuongeza madini joto kwenye mwili,  na kusaidia mmeng'enyo wa chakula. Tende ina utajiri wa virutubisho kadhaa, fiber, na antioxidants, Tende ni maarufu duniani kote. Matunda haya yaliyokaushwa ni yenye faida kwa kutibu matatizo kadhaa kutoka na tabia yake ya kuzuia uvimbe kwenye mwili, kuzuia sumu (antioxidant), na kuzuia tumor. 

 Tende ni nini?

Tende ni tunda tamu la kutafuna litokanalo na mti wa mtende, kitaalamu huitwa Phoenix dactylifera. Tende zimekuwa moja ya chakula kikuu cha nchi za Mashariki ya kati kwa maelfu ya miaka sasa. [1] Waislamu huchukulia miti ya mitende na tende zenyewe kama utukufu, na kipindi chote cha mwezi mtukufu wa kufunga wa Ramadhan, matunda haya ni kiunganishi muhimu kwenye msosi. ila tende in kariibia asilimia 60 hadi 70 ya sukari na ina kiwango kikubwa cha fiber (nyuzi lishe), kutegemeana na aina ya tende, kitu kinachofanya tende kuwa  mbadala mzuri kiafya wa kuongeza nishati ya mwili. [2] Pia tende ina kiasi ikubwa cha madini joto (iron) na husaidia kupambna na anemia. 

Tende sasa ni maarufu duniani kote na hutumika kama kiongeza utamu cha asili kwenye vinywaji kama smoothies, juices, sharubati za virutubisho, na bidhaa za kuoka kama keki na muffins.   


Virutubisho vya Tende 

Kulingana na takwimu za USDA, tende ni chanzo kizuri cha nishati, fiber, suari, na baadhi ya vitamini na madini. [3] Madini muhimu kama vile Calcium, madini joto (iron), phosphorus, sodium, potassium, magnesium, sulfur, na zinc yanaweza kupatikana kwenye tende.Mballi na virutubisho vilivyotajwa hapo juu, tende pia zina vitamini muhimu kama thiamin, riboflavin, niacin, vitamin B6, folate, vitamin A, na vitamin K.


Faida za Kiafya

Hebu tuangalie baadhi ya faida muhimu za tende kwa kina hapa chini.


Chanzo kizuri cha Nishati


Tende zina kiwango kikubwa cha sukari kama glucose, fructose, na sucrose. Kiwango kikubwa cha nishati kinachopatikana kinaweza kuchanfiwa na kiwango hiki kikubwa cha sukari iliyopo. [5] [6] Watu wengi duniani hula tende mchana kipindi wakihisi uchovu kuweza kuwasaidia kurudisha kiwango cha nishati kwa haraka.
Mara nyingi unapokuwa kwenye mazoezi gym, nje au hata kwenye machine ya mazoezi nyumbani kwako, hujihisi kuchoka. Tafiti iliyochapishwa kwenye jarida la International Journal of Food Sciences and Nutrition inashauri kwamba tende iliyo na utajiiri wa virutubisho muhimu inaweza kukusaidia urudisha nishati ya mwili ghafla. [7]
Waumini wa kiislam hufungua funga zao kwa kula tende na maji. Hii pia husaidia kuzuia ulafi wa chakula pindi funga imemalizika.

 Inaweza Kuimarisha Afya ya Ubongo

Tafiti iliyofanywa na kuongozwa na Musthafa Mohamed Essa, Ph.D. [8] et al. inashauri kwamba tende hukulinda dhidi ya sumu ziletwazo na msongo wa mawazo (oxidative stress) na uvimbe (inflammation) kwenye ubongo. Kulingana na utafiti, " tende ni chanzo kizuri cha nyuzi lishe na zina utajiri wa phenolics na viondosha sumu vya asili, kama vile anthocyanins, ferulic acid, protocatechuic acid, na caffeic acid”. [9] Uwepo wa kampaundi hizi za polyphenolic kunaweza kusaidia kupoozesha kukua kwa ugonjwa wa Alzheimer na dementia. 



Inaweza kusaidia kupunguza Kuvimbiwa


Kwenye matibabu ya asili ya Tunisia, tende hutumika kutibu hali ya kuvimbiwa. [10] Kulingana na utafiti juu ya athari za nyuzi lishe, vyakula vyenye utajiri wa nyuzi lishe (dietary fiber) ni muhimu kwa kuimarisha mwendo wa chakula kwenye njia yake na uhaikisha chakula kinapita bila tabu kwenye njia ya utumbo. [11] Tafiti ya mwaka 2005 iliyochapwa kwenye jarida la Journal of Agricultural and Food Chemistry pia inasema wamba tende zina kiwango kiwango kikubwa dietery fiber na insoluble fiber, kwa ujumla. [12] Insoluble fiber inayopatikana kwenye tende huchangia mmeng'enyo mzuri wa chakula kwa kukusanya kinyesi kwa pamoja na pia inaweza kusaidia kupunguza dalili za kuvimbiwa. [13] [14]
Namna ya Kutumia: Anza kwa kuloweka tende usiku mzima ndani ya maji ili zilainike. Baada ya hapo weka tende zilizolowekwa na maji yake yaliyotumika kulowekea kidogo kwenye mashine ya kusagia kama blender kuifanya iwe rojo zito, lenye utajiri wa nyuzi lishe.


Huleta afueni dhidi ya matatizo ya Utumbo  

Tafiti zinasema kwamba tende zina insoluble fiber(nyuzi lishe zisizo yeyuka kwenye maji) na soluble fibers (nyuzi lishe zinazoyeyuka kwenye maji), sambamba na amino acid nyingi ambazo zinazoweza kuimarisha mmeng'enyo wa chakula  na kuhakikisha kinapita kwa haraka kwenye njia ya kongosho. [15] Kulingana na mrejeo uliochapwa kwenye jarida la uchambuzi la virutubisho, nyuzi lishe pia zinaweza kusaidia kwenye matibabu ya matatizo kama ugonjwa wa gastroesophageal reflux disease (GERD), diverticulitis na hemorrhoids. [16]

Hutoa Afueni kutoka kwenye Anemia

Tende ni chanzo kizuri cha virutubisho vingi, ikiwemo madini joto (iron). Upungufu wa madini joto huchangiwa na ugonjwa wa Anemia, hali inayoletwa na uchovu, kizunguzungu, kucha zilizo pauka na kuishiwa pumzi mara kwa mara. Kwa bahati, ongezeko la ulaji wa vyakula vyenye utajiri wa madini joto kama vile tende kunaweza kusaidia kutoa afueni kwenye dalili za anemia. Hata hivyo, hakuna utafiti uliofanywa unaoelezea kazi yake ya moja kwa moja katika kutibu anemia. [17]


Huzuia Magonjwa ya Moyo


Tafiti iliyowekwa na Waseem Rock et al. kwenye jarida la Journal of Agricultural and Food Chemistry imehitimisha kwamba ulaji wa tende ulileta athari chanya katika kupunguza  kiwango cha triglyceride na kupunguza mgandamizo wa sumu, vyote kwa pamoja ni vyanzo hatari vya ugonjwa wa moyo na atherogenesis, ambayo ni kujengeka kwa fati yabisi ndani ya mishipa ya ateri. [18] [19]
Matunda haya yaliyokaushwa yana utajiri wa antioxidants, ambazo zinaweza kusaidia kuzuia atherogenesis na kusaidia kwenye kupunguza hatari ya ugonjwa wa stroke.[20] Tende pia zina utajiri wa baadhi ya phytochemicals  ambazo pia zinaweza kusaidia ulinzi dhidi ya ugonjwa wa moyo. [21]

Zaidi, tende ni chanzo cha utajiri wa potassium, ambayo tafiti nyingi zimeonyesha  uwa na uwezo wa kupunguza shinikizo la damu na kupunguza hatari ya ugonjwa wa stroke sambamba na magonjwa mengine yanayohusiana na moyo. [12] [22]



Hutibu Matatizo ya Nguvu za Kiume


Kuna faida nyyingi za tende kwwa wanaume lakini hii hufanya kuwa ni ya muhimu kuliko zote.
Mwaka 2006, utafiti uliofanywa kwa mnyama uliweka bayana athari ya poleni za tende na mafuta yake kwenye teno la kujamiiana, utafiti uliripoti kwamba kiwango kikubwa cha estradiol na flavonoid kwenye tende zinasaidia kuongeza idadi ya mbegu za uzazi na mwendokasi wa mbegu hizo. [23] Utafiti mwingine uliofanyika nchini India unaelezea kwamba poleni za tende zimekuwa zikitumika kutibu ugumba kwa wanaume kwenye tiba asili.
Kwa maana hiyo, kama unatafuta njia rahisi ya kuamsha hamu ya tendo la ndoa, unaweza kuamua kula tende asilia isiyoongezwa kemikali za kuhifadhia. Shukrani kwa sifa zake za kuongeza nguvu za kiume.
Namna ya kutumia: Loweka tende kiasi cha kiganja cha mkono kwenye maziwa ya mbuzi fresh usiku mzima, halafu zisage pamoja na maziwa yaleyale  pamoja na mchanganyiko wa unga wa mdalasini na asali. Hata hivyo, kupata ushauri wa mtabibu wa kuaminika inashauriwa kwa nguvu zote kutambua ni tiba gani itakusaidia wewe. 

Huzuia Night Blindness

Night blindness ni tatizo la macho kutoweza kuona vizuri nyakati za usiku au mahali kwenye mwanga hafifu.

Upungufu wa Vitamin A  mara nyingi husababisha night blindness, sambamba na dlili nyingine kama ukavu macho, na hatari ya ongezeo la maambukizi. Kulingana makala ya iliyoandikwa na H.A. Hajar Al Binali, M.D. kwenye jarida la Heart Views, tende zina utajiri wa carotenoids, ambazo husaidia kuzuia night blindness na kubakisha afya nzuri ya macho. [24] 


Husaidia Kutibu Tatizo Sugu la Kuharisha

Kulingana na maala iliyochapwa na Columbia University Medical Center, vyakula vyenye utajiri wa potassium kama vile tende vinaweza kusaidia kurudisha na kubakisha vimiminika ulivyoweza kupoteza  kutokana na tatizo la kuharisha. [25] Shukrani kwa utajiri wake mwingi wa nyuzi lishe, zinaweza pia kusaidia kwenye mmeng'enyo wa chakula  na kuondoa dalili za kuwepo viashiria vya kuharisha.


Zinaweza kuwa na Sifa ya Kupambana na Kansa

Utafiti uliofanywa na Prof. [26] Dr. Jeremy PE Spencer et al unaeleza kwamba ulaji wa tende unaweza kusaidia kuimarisha afya ya njia ya chakula na kuzorotesha uwezekano wa kukua na kusambaa kwa seli za kansa ya utumbo (colorectal cancer cells). Tafiti pia zinasema kwamba matunda haya yaliyokaushwa huzuia uvimbe kutokea, ijapokuwa njia hasa inayotumika hapa haijulikani na inahitaji tafiti zaidi. [1]



Husaidia Afya ya Mifupa


Chapisho la Julie Garden-Robinson, Ph.D., L.R.D., et al. [27] na wenzake wa  North Dakota State University linashauri ya kwamba tende zina virutubisho viitwavyo boron ambavyo vinahamisisha afya ya mifupa. Utafiti uliochapishwa kwenye jarida la uchambuzi wa kina kwenye Sayansi ya Chakula na Virutubisho linasema kna magonjwa kama osteoporosis. [28]
Tende ambazo hazijaongezwa kemikali za kuhifadhia zina madini ya selenium, manganese, copper, na magnesium, yote yanaweza kusaidia kwenye udhibiti wa afya ya mifupa, hasa kwa wazee.

Zinaweza Kukuza Afya ya Kuongeza Uzito


Kulingana na USDA, matunda haya yaliyokaushwa yamesheheni sukari sambamba na protini, na vitamini nyingine muhimu nyingi na madini. [3] Pia zimesheheni nyuzi lishe, ambazo zinaweza kusaidia  kwenye kudhibiti uzito.
Utafiti uliofanywa kwa mnyama mwaka 2014 unashauri kwamba ulaji wa tende unaweza kusaidia kuongeza uzito. [29] Hata hivyo, utafiti mwingine  uliofanyika mwaka 2016 haukuonyesha ongezeko lolote la uzito. [30] Kutokana na ripoti hizi kukinzana, utafiti zaidi unahitajika kusapoti faida hii.


Mwisho, weka akilini kwamba tende zina kiwango kikubwa cha sukari na kalori, ambazo zinaweza kuchangia uzito kuongezeka na matatizo mengine ya kiafya kama zikiliwa kwa wingi kupitiliza.Kwahiyo, ni bora kula kwa wastani na ufurahie  sehemu ya afya bora ili kuongeza faida za kiafya.




































Maoni