Mafuta ya Zaituni (Olive Oil) : Maajabu Yake na Faida 10 za Kiafya

Mara nyingi ni ajabu kwa mpishi mahili kukosa chupa ya mafuta ya zaituni jikoni kwake. Sababu ikiwa, mafuta ya zaituni hufanya kila kitu kiwe na ladha nzuri zaidi na yenye kuleta afya nzuri zaidi!

Kuna faida kemkem za kiafya za mafuta ya zaituni kama kutibu kansa ya utumbo mpana na kansa ya matiti, kisukari, matatizo ya moyo , ugonjwa wa arthritis (hupelekea maungio ya viungo kuvimba na kuuma, zipo aina nyingi za ugonjwa huu), na lehemu ya kiwango cha juu (high cholesterol). Pia hujumuisha udhibiti wa kupungua uzito, kuboresha mfumo wa kimetaboliki, kkurahisisha mmeng'enyo wa chakula, na kuzuia kuzeeka. Ni kiungo kinachotumiwa kwenye maandalilzi ya mapishi mengi na pia hutumika kwa kusudi la matibabu. 



Mafuta ya Zaituni (Olive Oil) ni nini?

Mafuta ya zaituni ni mafuta muhimu yatokanayo na mafuta ya tunda la zaituni, Mti wa mzaituni hupatikana sana maeneo ya Mediterania. Mafuta haya yamekuwa yakitumika na binadamu kwa karne nyingi. Hutumika kwenye mapishi, kuzalisha bidhaa za vipodozi na sabuni, hutumika kwa dhumuni la matibabu, na kama dawa za hospitalini. Pia mafuta ya zaituni yanaweza kutumika kama fuel kwa kuwashia kandili/chemli.


Aina za Mafuta ya Zaituni

Zifuatazo ni aina za Mafuta ya Zaituni:
  • Virgin Olive Oil: Aina hii hutumika kwa kupikia yakiwa na kiwango kidogo cha acid.
  • Extra Virgin Olive Oil: Hii ni aina bora zaidi na hutengenezwa kwa kukamuliwa kwa tunda la zaituni kwenye hali ya baridi . Yana kiasi kikubwa cha polyphenols kwasababu ndiyo aina ya mafuta yanayopitia sehemu chache zaidi kwenye matengenezo yake. 
  • Pure Olive Oil: Aina hii ni mchanganyiko wa virgin oil na yale yaliyoongezwa kemikali. Mafuta haya yana kiwango kikubwa cha acid.
  • Light Olive Oil: Aina hii ya mafuta haya yana ladha ndogo mno na kufanya kuwa chaguo zuri la wale wasiopenda ladha nzito ya mafuta ya zaituni.
  • Lampante Oil: Hutumika kama fuel na hayashauriwi kwa matumizi ya mapishi.


 Faida za kiafya za Mafuta ya Zaituni

Mafuta ya zaituni yana faida kemkem zilizo bora. Kati ya faida hizo ni kama zifuatazo:


Hushusha Lehemu (Cholesterol)


Tafiti iliyofanywa kwa ushirika wa  Harvard School of Public Health [3] na vyuo vingine vingi imebaini kuhusu aina ya mafuta ya zaituni ya extra virgin kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo.
LDL cholesterol ni aina mbaya ya cholesterol, ambayo huongeza hatari ya mshtuko wa moyo na magonjwa ya moyo. Extra virgin olive oil, ambayo yana utajiri wa karibu aina 40 za kemikali viondosha sumu (40 antioxidant chemicals), husaidia kupunguza athari za LDL cholesterol. Pia husaidia kuongeza kiwango cha  HDL cholesterol.

Hudhibiti Kisukari (Diabetes)

Kwenye tafiti iliyochapishwa kwenye jarida la Nutrition and Diabetes mwaka 2017, inaonyesha ya kwamba mafuta ya zaituni yanaweza kusaidia kwenye kuzuia na kudhibiti kisukari yakitumika kwenye chakula cha kila siku. [4]



Kupunguza Uzito

Wataalamu wa tiba wanadai ya kwamba ni vigumu sana kuongezeka uzito kutokana na mono-unsaturated fats zilizopo kwenye mafuta ya zaituni. Tafiti zilizofanywa kwenye mafuta haya ya Mediterania zimeleta matokeo chanya kwenye upande wa kuyatumia kwa lengo la kupunguza uzito kwani yana fati nzuri na ni mbadala mzuri wa mafuta mengine yenye kalori [5] Mafuta ya zaituni  yanaweza kuongeza mmeng'enyo wa chakula baada ya kula na kusaidia kupunguza kiasi cha chakula kinacholiwa kwa kukufanya ujihisi umeshiba kwa kiasi kidogo cha chakkula. [6] Yanapochanganywa na mbogamboga kwenye chakula, mafuta ya zaituni yanaweza kuwa na athari chanya  kwenye mfumo wa umeng'enyaji chakula ambayo yanaweza kuathiri moja kwa moja kudhibiti uzito. 

Mafuta ya zaituni yana utajiri wa polyphenols ambazo zina sifa ya anti-inflammatory na antimicrobial .Matokeo yake, matumizi yake husaidia kudhibiti ukuaji wa bakteria waletao magonjwa na kupungua inflammation. [7]



Huboresha Mmeng'enyo wa Chakula

Mafuta ya zaituni hujulikana kwa kusaidia kwenye shughuli za umeng'enyaji . hutumikana kama mafuta dawa kusafisha njia ya umeng'enyaji chakula na kuboresha chakula kupita vizuri kweye njia hiyo.


Huchelewesha Uzee

Yenye utajiri wa antioxidants, mafuta ya zaituni hupunguza shughuli za kiasili za kukua za mwili wa binadamu. Kiasi cha monosaturated fats inayopatikana kwenye mafuta ya zaituni husaidia seli kutochoka. Hutumika kwenye bidhaa za vipodozi na matibabu ya asili, hufanya maajabu kwenye ngozi kwa kuipa mng'ao wa asili.

Huzuia Mawe ya Kibofu (Gallstones)

Matumizi ya mafuta zaituni pia ni muhimu kwenye kuzuia mawe ya kibofu (gallstones ) kwani yana athari ya kilainishi. Hutumika mara nyingi na watu wanaosafisha kibofu cha mkojo.


Huimarisha kuta za Seli

Kutokana na tafiti ya mwaka 2018 iliyochapishwa kweny jarida la International Journal of Molecular Sciences [8], mafuta ya zaituni yana polyphenols ambazo husaidia kujenga kuta za seli zilizo imara. Pia huongeza hali ya kuvutika kwa kuta za ateri, kukulinda dhidi ya matatizo kadhaa ya moyo.



Kizuia Kansa Muhimu

Mafuta nda mwili wa binadamu dhidi ya ukuaji wwa kansa, hasa kansa ya utumbo, sambamba na kansa ya matiti na ngozi. Tafiti ya madawa iliyofanyika Oxford University imeonyesha ishara chanya kwamba kiwango cha acid cha mafuta haya kinaweza kuzuia kuanza kwa  kansa ya rectum na njia ya chakula.


Jarida la Carcinogenesis [9] limesheheni tafiti ya 2018 ikisema kwamba Extra virgin oil ndio dhahabu yenyewe yunapokuja kwenye suala la kuzuia seli za kansa kukua kwenye mwili. 
Tafiti nyingine imethibitisha athari hiyo hiyo  na kuweka wazi kwamba, mafuta ya zaituni yameonyesha athari kubwa chanya kwenye kansa ya titi. [10] Hydroxytyrosol, ambayo ni kijenzi kikuu cha mafuta haya kinaweza kusaidia kuzuia kansa ya titi kwa wanawake waliokoma hedhi.

Hushusha Shinikizo la Juu la Damu(Hypertension)

Tafiti za hivi karibuni zinaeleza kwamba chakula cha kiMediterania chenye wingi wa  unsaturated fats (inayopatikana kwenye mafuta ya zaituni), nitrite, na nitrate (inayopatikana kwenye majani ya kijani ya mbogamboga) huweza kukulinda  dhidi ya shinikizo la juu la damu .[8] [11]

Maoni

  1. Nimefurahi sana kuzijua faida za tibw ya mafuta ya mzeituni

    JibuFuta
  2. nijambo la heri kujua matumizi ya mafuta ya zaituni je kuna faida nyingine au ndio hizitu?

    JibuFuta
  3. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  4. Nakala muhimu sana, Mafuta ya Zaituni ni ya afya kweli, angalia SDS au MSDS

    JibuFuta

Chapisha Maoni