Mafuta ya Virgin Coconut Oil ni yapi na zipi faida zake?

Virgin coconut oil  hufahamika kwa manukato yake mazuri na ladha, vilevile kwa viondosha sumu vilivyomo (antioxidants), medium-chain fatty acids (MCFA), na vitamini. Wakati mafuta ya nazi kwa hakika si kitu kigeni kwa wengi, haya mafuta ya  Virgin Coconut Oil yaweza kuwa kitu kigeni. Sio jina jipya lililotolewa na kampuni fulani kwenye mafuta ya nazi ya kawaida ili kuongeza idadi ya mauzo, kama wengi wanavyodhani. Kwahiyo haya ni mafuta gani, hasa?

 

Mafuta ya Virgin Coconut Oil ni kitu gani?

Virgin coconut oil ni mafuta yanayozalishwa kutoka kwenye nazi bila kuyapitisha kwenye joto. Mafuta haya yameanza kujizolea umaarufu duniani kote ukilinganisha na mafuta ya nazi ya kawaida tuliyoyazoea na kwa sababu nyingi nzuri. Mafuta haya yanatofautiana na mafuta ya nazi ya kawaida kwa namna nyingi.Tofauti hizi hasa hulalia kwenye chanzo (muonekano wa kimaumbile wa chanzo). njia ya uzalishaji, na faida za mafuta haya.


Uzalishwaji wa Virgin Coconut Oil

Utofauti mkuu uliopo kati ya mafuta ya nazi ya kawaida na virgin coconut oil (VCO) umelalia kwenye uzalishwaji wao. Mafuta ya nazi ya kawaida hupatikana kwa kukamuliwa nazi kavu iliyochambuliwa (kwa mashine maalumu au kibao chambuzi) kukiwa na kama asilimia sita ya kimiminika (Tui la nazi).  Mafuta ya VCO huzalishwa kutoka kwenye tui lililotoka kwenye nazi ambazo hazijakauka (fresh coconuts). Baada ya hapo, kwa kutumia njia kama ya fermentation, kuchuja tui, kuweka kwenye friji, na kutumia vimeng'enyo (enzymes), mafuta hutenganishwa kutoka kwenye maji au unyevu. Kwenye kesi kadhaa, mafuta haya ya nazi huchemshwa kwa kuvukiza maji au unyevu uliopo.
Hata hivyo, kwenye kesi ya virgin coconut oil, malighafi na njia za uzalishaji hazitakiwi kuhusishwa na joto. Kwahiyo, kwenye uzalishaji mzuri virgin coconut oil, umakini wa hali ya juu unahitajika kuhakikisha nazi zilizochambuliwa na tui hazikutani na mwanga wa jua au joto, kwenye mfumo mzima wa uzalishaji. Kwenye baadhi ya kesi, Mafuta virgin coconut oil huzalishwa kwa kukamuliwa kwa nyama za nazi iliyokauka. Kitendo hiki kinaitwa Micro-expelling.


Mafuta ya Virgin coconut oil yaliyozalishwa kwa njia ya cold compression husemekana kuwa ni mazuri kuliko yale yaliyotokana na nji ya fermentation kutoka na mafuta yaliyozalishwa kwa njia ya fermentation  yana  kiwango kikubwa cha uyevu na uharibika haraka. Kama utahitaji kuyayeyusha (kipindi cha baridi), usiyawweke kwemoto moja kwa moja. Badala yake, yaweke kwenye kikombe na weka kikombe kwenye maji ya moto.

Utofauti kati ya Virgin na Mafuta ya Nazi ya Kawaida

Tukiachana na namna yanavyozalishwa, tofauti iliyo muhimu kati ya mafuta ya nazi ya kawaida na yale ya virgin, baadhi ya sifa za mafuta haya huyafanya dada hawa wawili, waliozaliwa na mama mmoja, kuwa tofauti sana, huku kwa namna nyinezo hubakia kufanana.

Muonekano

Virgin coconut oil huonekana tofauti kidogo na mafuta ya nazi ya kawaida; hata hivyo, tofauti hii haiwezi kufanywa kwa macho pekee.[1] Utofauti huu ni kutokana na uwepo wa chembe chembe ndogo zisizoonekana kwa macho na unyevu uliopo. Kwa upande mwingine, mafuta ya nazi ya kawaida  huchujwa na kubakishwa fatty acids ndani yake. Kimawazo, mafuta haya yalitakiwa yawe na muonekano kama maji. Hata hivyo, rangi yake hutofautiana kulingana njia iliyotumika kuzalishwa.


Usafi

Mafuta ya Virgin coconut oil yana ladha nzuri na harufu kwa maana yametokea kwenye nazi mpya (fresh coconut) na yamepitishwa kwenye moto mdogo sana na mwanga wa jua. Pia hayajasafishwa kwa kuwekwa kemikali. Hii hubakisha uzuri wa asili wa mafuta haya, ikiwemo kiwango cha juu cha vitamin E na madini,
Virutubisho hivi huibiwa kwenye mafuta ya nazi ya kawaida kipindi cha uchemshaji, kuchuja, refining, na bleaching, ambayo hufanywa ili mafuta yasiwe na rangi na harufu. Zaidi, VCO hufanya kazi kama wakala wa kurudisha unyevu kwenye ngozi. Sifa zake za kuondosha sumu ni nzuri mno kuliko zile za mafuta ya kawaida ya nazi.

Muundo


Mafuta haya mawili hayana tofauti sana kwenye muundo, ila ukweli ni kwamba baadhi ya polyphenols, vitamins, na madini ambayo yanachangia kwenye radha, harufu, na uzuri wa mafuta ya nazi hupatikana zaidi kwenye virgin coconut oil kuliko kwenye mafuta ya kawaida ya nazi. Zaidi, mafuta ya vco yana utajiri wa medium-chain fatty acids.

Faida za Virgin Coconut Oil


Kutokana na kutohusishwa na moto (au hata kama upo basi ni joto dogo sana), or mwanga wa jua, na huzalishwa kutoka kwenye nazi zisizokauka kwa njia tofauti ya uzalishaji, mafuta ya virgin coconut oil bila shaka yana utajiri wa faida kuliko mafuta ya nazi ya kawaida. Yana kiwango kikubwa cha vitamin, viondosha sumu (antioxidants) ambavyo hakuna kabisa kwenye mafuta ya kawaida ya nazi, madini, medium-chain fatty acids, radha, harufu nzuri, na hata kiwango cha protein.
Umri wa kudumu wa mafuta ya virgin coconut oil ni mkubwa zaidi ukilinganisha  na mafuta mengine yoyote ya mimea, na mafuta ya nazi yaliyopitia njia ya RBD (Refined Bleached Deodirized)


Bei ya Virgin Coconut Oil 

Kama tujuavyo, vitu vizuri vina gharama. Mafuta ya virgin coconut oil hayana tofauti na hiyo sheria. Yanapendwa kuliko mafuta ya kawaida ya nazi (Kutokana na uzalishwaji wake ni mgumu na unagharimu). 
Bei yaweza kuwa tofauti kulingana na mzalishaji, ubora, na wingi(rejareja na jumla). Mbali na hizo tofauti zao chche, mafuta ya virgin coconut oil yana gharama kubwa ukilinganisha na mafuta ya nazi ya kawaida.


Ufilipino, Indonesia, Burma, Sri Lanka, India, na nchi nyinginezo za ukanda wa tropiki ndio wazalishaji wakubwa wa mafuta ya virgin coconut oil. Mafuta haya yana bei rahisi kwenye nchi hizi ukilinganisha na Marekani, Canada na nchi zaUlaya. Haijalishi  bei ipoje, kama umetoka kwenda kununua mafuta ya vco, ni lazima ukaenda kwa watengenezaji/wauzaji wenye kuaminika. Kuna matapeli wengi kwenye soko la mafuta haya wanao ongeza radha feki kwenye mafuta ya kawaida ya nazi na kuyauza kama virgin coconut oil.

 Extra Virgin Coconut Oil ni Kitu gani?


Mara nyingi tunasikia kuhusu "extra virgin coconut oil", lakini ndio kitu gani hiki? Ina utofauti gani na virgin coconut oil?
Kulingana na taasisi ya Asian and Pacific Coconut Community, ambayo imetenga viwango vya ubora vya APCC vya mafuta ya Virgin coconut oil.Mafuta haya hupatikana kutoka kwenye nyama za nazi fresh iliyokomaa kwa njia ya mashine au asili bila kutumia moto au kwa kutumia moto kidogo sana, ambayo haiwezi kupelekea kuharibu mafuta. [2]

Kipindi mtu akidai kuwa mafuta hayo ya nazi ni "extra virgin", hilo neno extra linamaanisha kuongezeka kwa mafuta hayo na wala lisikupe mhagaiko.  Taasisi ya APCC haijaorodhesha chochote kuhusu "extra virgin coconut oil". Kwa maana hiyo, kwa lengo kufanya majaribio, extra virgin coconut oil, kwa ushauri wangu, inatakiwa ichukuliwe kama virgin coconut oil.

Maoni

Chapisha Maoni