TRIGLYCERIDES :Kwanini zina umuhimu sana kwenye mwili?

Kwani zina umuhimu gani mkubwa kwenye Mwili?


Natambua kwa jina hilohilo la kimombo la Triglycerides (matamshi: Traiglaiseraid).
Triglycerides ni kipimo muhimu kwenye afya ya moyo.
Yafuatayo yanathibitisha kwanini triglycerides zina umuhimu mkubwa kwenye mwili, na nini cha kufanya kama zikizidi kiwango stahiki.

Kama ulikuwa unapiga jicho kwenye shinikizo/presha ya damu na kiwango cha lehemu(cholesterol), kuna kitu kingine unahitajika kukimulika; triglycerides zako, aina ya mafuta yaliganda(fat/lipids) kwenye damu, yenye uwezo wa kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo. 
Ijapokuwa chaguzi za mfumo wa maisha zinazopendekeza kuishi kwa afya njema zinaweza kusaidia kupunguza triglycerides pia.


Ni nini hizi Triglycerides?

Ni aina ya fat au lipid (mafuta yabisi) yanayopatikana kwenye damu. Unapokula, mwili wako unabadilisha kalori zote zisizohitajika kutumika na kuwa triglyceride. Hizi triglycerides zinahifadhiwa kwenye seli zako za mafuta (fat cells). Baadae, homoni zinamwaga triglyceride wakati unapokula msosi. Kama wewe ni mtu wa kula kalori zaidi kuliko unavyoziunguza kwa mazoezi, mathalani kalori nyepesi kama vile carbohydrate(kabohaidreti) na fats(fati), unaweza kuwa na kiwango cha juu cha triglycerides( hypertriglyceridemia).

Hali gani inaonesha ukawaida?

Kipimo cha kawaida cha damu kinaweza kuonesha endapo triglycerides zako zimeangukia kwenye kiwango kipi cha afya.

  • Kawaida : Chini ya 150mg/dL au chini ya 1.7mmol/L
  • Kiwango cha juu kati : Kati ya 150 - 199 mg/dL (1.8 -2.2 mmol/L)
  • Kiwango cha juu : Kati ya 200 - 499mg/dL (2.3 - 5.6mmol/L)
  • Kiwango cha juu zaidi : Kati ya 500mg/dL au juu ya hapo (5.7mmol/L au juu yake)

Mtaalam wako wa afya ataangalia kiwango chako cha juu cha triglyceride kama sehemu ya  kipimo cha kiwango cha lehemu (cholesterol), muda mwingine huitwa lipid panel au lipid profile.
Ili kipimo cha triglycerides kipatikane kwa uhakika basi huna budi kufunga kula kwa masaa 9 hadi 12 kabla ya damu kutolewa.

Nini tofauti kati ya Triglyceride na Cholesterol

Triglyceride na cholesterol ni aina mbili tofauti za mafuta(lipids) zinazozunguka kwenye damu yako.Triglycerides zinahifadhi kalori zisizotumika na kuupa mwili nishati na cholesterol hutumika kujenga seli na aina fulani za homoni. Kwa sababu triglyceride na cholesterol haziwezi kuyeyuka kwenye damu, zinazunguka pamoja na damu, kwenye mwili wako wote kwa msaada wa protini zinazosafirisha mafuta (lipoprotein).


Kwanini triglyceride ya kiwango cha juu huzingatiwa zaidi?

Ijapokuwa haipo wazi ni kwa namna gani triglyceride ya kiwango cha juu inaweza kuchangia kukomaza mishipa ya ateri au kunenepesha kuta za mishipa ya ateri (atherosclerosis) ambayo huongeza hatari kupata ugonjwa wa stroke, mshtuko wa moyo, na ugonjwa wa moyo. Triglyceride ya kiwango cha juu zaidi kwa mfano juu ya 1000mg/dL (11.29mmol/L) inaweza pia kusababisha ugonjwa hatarishi wa kongosho.
Triglycerides ya kiwango cha juu huashiria alama ya hali nyingine ambayo inaongeza hatari ya ugonjwa wa moyo na stroke pia, ikiwemo kiriba tumbo(obesity)  na matatizo ya kimetaboliki ( metabolic syndrome) - hali inayoonyesha mlundikano wa mafuta kuzunguka kiuno, kiwango cha juu cha sukari ya damu, na kiwango kisicho cha kawaida cha lehemu(cholesterol).


Muda mwingine kiwango cha juu triglycerides ni ishara ya uzembe wa kudhibiti aina ya pili ya kisukari(type 2 diabetes), Ini, au ugonjwa wa figo, au tabia chache za kurithi ambazo zinaathiri namna mwili wako unabadilisha mafuta kwenda kuwa nishati.
Kiwango kikubwa cha triglyceride pia inaweza kuwa ni madhara ya matokeo ya kutumia madawa ya hospitali kama vile vidonge vya kuzuia mimba, diuretics, steroids, au beta blockers.



Je, ni njia gani nzuri ya kupunguza triglycerides?

Uchaguzi wa mfumo mzuri wa kiafya ndio funguo yenyewe

Punguza Uzito

Kama una uzito uliopitiliza kawaida, kupunguza kilo 2 hadi 5 kutakusaidia kupunguza triglycerides. Jipe matumaini na kuweka mtazamo wako kwenye faida za kupunguza uzito, kama vile nishati zaidi na afya kuimarika.

Punguza kalori

Kumbuka kwamba kalori zinazozidi zinabadilishwa kuwa triglyceride na kuhifadhiwa kama fati. Kupunguz kalori kunapunguza triglyceride.

Epuka vyakula vya sukari na vilivyosindikwa

Carbohydrate ya kawaida kama sukari, vyakula vilivyotengenezwa na kwa unga mweupe/sembe vinaweza kuongeza triglycerides.

Chagua mafuta mazuri

Pigia upatu kula mafuta yanayotokana na mimea kuliko yale yanayopatikana kwenye nyama, kama mafutaya mzaituni (olive oil), mafuta ya karanga, na kanola. Ondoa nyama nyekundu kwa kuweka samaki, wali na omega-3 nyingi.


Punguza kiwango cha pombe unachokunywa

Pombe ina kiwango cha juu cha kalori na sukari, na ina athari za triglyceride. Hata kiasi kidogo cha pombe kinaweza kupandisha kiwango cha triglyceride.

Fanya mazoezi mara kwa mara

Weka lengo la walau dakika30 au zaidi za mazoezi ya mwili kwa kila siku za wiki. Mazoezi ya mara kwa mara yanaweza kupunguza triglyceride na kuongeza lehemu(cholesterol nzuri). 
Chukua hatua ya kutembea kwa mguu  kila siku, ogelea na kikundi cha mazoezi. Kama huna muda wa kufanya mazoezi kwa dakika 30, jaribu kujibana kufanya kwa dakika 10 kwa muda. Chukua matembezi mafupi, tumia ngazi unapokuwa ofisini badala ya lifti (elevator) au jaribu 'sit-ups' au 'push-ups' kipindi unatazama luninga.

Vipi kuhusu Matibabu?

Kama mabadiliko ya maisha uliyofanya hayatoshi kudhibiti kiwango cha juu cha triglyceride, tabibu wako anaweza akashauri vifuatavyo:

1. Statins
Tabibu wako anaweza kukushauri kutumia dawa hizi zinazopunguza cholesterol kama una kiwango kidoho cha cholesterol cha HDL( High density lipoprotein) au kama umeshawahi kuwa na ateri zilizovunjika au kisukari.
Mfano wa hizo statins ni atorvastatin(lipitor) na simvastatin(zocor). Maumivu ya misuli ni matokeo mazuri ya utumiaji wa dawa hizi.

2. Mafuta ya Samaki
Yanajulikana kama Omega-3 fatty acids, virutubisho vya mafuta ya samaki vinaweza kusaidia  kupunguza triglyceride. Dozi kubwa huitajika, ijapokuwa, hii huwaitaji wale wenye kiwango cha triglyceride juu ya 500mg/dL( 5.7 mmol/L ).

3. Fibrates
Matibabu ya fibrate, kama vile fenofibrate(TriCor, Fenoglide, na nyinginezo) na gemfibrozil(lopid), pia zinaweza kupunguza viwango vya triglyceride. Fibrate inaonekana kufanya vizuri kwa watu wenye viwango vya triglyceride juu ya zaidi ya 500mg/dL(5.7 mmol/L). Fibrate inaweza kuongeza hatari ya matokeo hasi pindi zikitumiwa pamoja na statins.

4. Niacin
Muda mwingine huitwa nicotinic acid, inaweza kupunguza triglyceride na cholesterol mbaya (low-density lipoprotein au LDL, cholesterol). Hii ni maalumu kwa wale wenye viwango vya triglyceride zaidi ya 500mg/dL(5.7mmol/L). Usije ukachukua duka la dawa bila ushauri wa daktari kwanza. 
Niacin inaweza kuchanganywa na madawa mengine.



Maoni

  1. Ahsante kwa elimu ndugu safi saana!!

    JibuFuta
  2. Asante kwa kupitia chapisho hili Mwaluko04, naheshimu mchango kaka.

    JibuFuta

Chapisha Maoni