Faida 16 za Kiafya na za Kushangaza za Ndizi

Faida za kiafya za ndizi ni kama kusaidia kupungua uzito, kupunguza kiriba tumbo, kutibu matatizo ya utumbo, kutibu tatizo la kutopata choo, na hali kama ya kuharisha, anemia, matatizo kwenye maungio ya viungo(arthritis), gout, na matatizo yanayotokea kwenye figo na kibofu.

Ndizi pia inaweza kusaidia kutatua matatizo ya mzunguko wa hedhi na kiungulia. Ni nzuri kwa kushusha shinikizo la damu, kulinda afya ya moyo, kuhimiza shughuli za kimetaboliki na kinga ya mwili, kupunguza ukomavu wa vidonda vya tumbo, ndizi zinahakikisha usalama wa afya ya macho, hujenga mifupa imara, na kuondoa sumu za mwili.



Ukweli wa Virutubisho vya Ndizi

Ndizi au banana kwa lugha ya kiingereza ambayo hujulikana kama Musa acuminata kwa lugha ya kisayansi ni chanzo cha utajiri wa protini, potassium, carbohydrate, na dietary fiber kulingana na USDA (United States Department of Agriculture). [1]Ndizi hazina kabisa fati na cholesterol, vilevile saidium isiyohitajika. Kiasi cha kudhangaza cha virutubisho  vilivyomo ni pamoja na vitamini kama vitamini C, vitamini B6, riboflavin, folate, pantothenic acid, na niacin, vilevile ndizi zina kiasi kingi cha vitamini nyingine adimu.
Ndizi pia zina madini kama phosphorus, calcium, manganese, magnesium, na copper.


Wanga na Kalori kwenye Ndizi

Ndizi ni chanzo kizuri cha virutubisho na gram 100 za ndizi mbichi zina kiasi cha kalori 89 na na gram 23 za carbohydrate (Chanzo: USDA [1]).


Faida za Kiafya za Ndizi

Ndizi zina faida nyingi za kushangaza za kiafya, ambazo zikiwemo zifuatazo: 


Hushusha Shinikizo la Damu

Kwa mujibu wa jaribio lililofanyika  Hypertension Institute, USA linasema ya kwamba potassium inafanya kazi ya uangalizi wa viwango vya kiafya vya shinikizo la damu. [2] Kutokana na ndizi kuwa ni chanzo kizuri cha utajiri wa potassium, zinasaidia kupunguza presha ya damu. 
Potassium husaidia kupunguza shinikizo kwenye mishipa ya ateri(arteries) na vena(veins), kwahiyo damu inaweza kusafiri kirahisi kwenye mwili na kufikisha oxygen kwenye baadhi ya viungo kuimarisha ufanyaji kazi wao. Hali hii huondoa atherosclerosis na magonjwa  yanayoambatana nayo ya stroke na mishtuko ya moyo ambayo hutokea mara kwa mara. Nyuzi lishe (fiber) zilizopo kwenye ndizi pia hukwangua cholesterol (lehemu) iliyozidi kwenye ateri na mishipa ya damu na zaidi huondoa shinikizo juu ya mfumo wa moyo.


Huleta Nafuu kwenye Dalili za Asthma(pumu)

 Kulingani na tafiti iliyofanyika kwenye Taasisi ya Moyo na Mapafu mwaka 2007, Imperial College London, London Uingereza, ndizi zinaweza kuwarinda watoto dhidi ya  kukohoa na dalili nyingi zinazohusiana na pumu (asthma). [3] 


Hutoa Nafuu kwa tatizo la kukosa choo 

Ndizi zina kiasi cha kutosha cha nyuzi lishe na kwa maana hiyo hurahisisha chakula kupita kwa urahisi kwenye njia yake. Nyuzi nyuzi  hizo hulainisha utoaji wa kinyesi na kumuondolea mtu balaa la kupata choo kwa shida. Tafiti zinasema kwamba ndizi pia husaidia kutibu matatizo yanayohusiana na tumbo. [4]


Husaidia Kudhibiti Kisukari

Somo lililochapishwa kwenye jarida la American Journal of  the Clinical Nutrition [5] lilivumbua kwamba pectin, iliyopo kwenye ndizi, inasemekana kuwa ni kirutubisho kisaidiacho kuimarisha kiwango cha glucose kwa wagonjwa wa kisukari. Kulingana na somo lililochapwa mwaka 2014, [6] ndizi huchangia gram 3 za dietary fiber, ambazo ni faida kwa wagonjwa wa kisukari type-1 na type-2.


Hutunza kumbukumbu na Kuimarisha hali ya mwili

Kulingana na jaribio lililofanywa mwaka 2015, amino acid tryptophan na viondosha sumu kama dopamine, kwenye ndizi, hufanya kazi kubwa mno kwenye kuimarisha hali nzuri ya mwili na kubakiza kumbukumbu. [7] Kwa kuongeza, magnesium husaidia misuli ku-relax na vitamini B6 hukusaidia kulala vizuri.


Hutoa Nafuu kwenye dalili za Anemia

Utafiti ulioongozwa na Dr. Olga P. GarcĂ­a, Autonomous University of Queretaro, Mexico, unaeleza ya kwamba ndizi zina kiwango cha juu madini joto(iron) na, kwa maana hiyo, husaidia  kwenye kutibu ugonjwa wa anemia kwa sababu madini joto(iron) ni sehemu muhimu ya seli hai nyekundu za damu. [8] Ndizi pia zina kiwango kizuri cha madini ya copper, ambayo ni madini muhimu kwenye utengenezaji wa seli hai nyekundu za damu. Kwa kuongeza wingi wa seli hai nyekundu za damu, hauzuii tu anemia peke yake, lakini pia unaweza kuongeza mzunguko kwenye maeneo yote ya mwili, kwa maana hiyo kutoa oxygen kwenye maeneo hayo na kurahisisha ufanisi wa kazi.

Kupungua Uzito

Ndizi ni muhimu kwa kupunguza uzito kwani makisio ya kalori 90 tu. Zina fiber nyingi vile vile na ni rahisi kumeng'enywa. Zaidi, hazina aina yoyote ya fati. Kwa maana hiyo watu wenye uzito uliokithiri hawahitaji kula sana kama diet zao zina ndizi kwa sababu zinashibisha. Nyuzi lishe pia hazitomfanya mtu ahisi njaa kwa kuzuia utolewaji wa homoni ya njaa, ghrelin. Hali hii itapunguza ulaji uliopindukia  na pia kusaidia kupunguza uzito. Utafiti uliofanyika 2012 pia unaeleza kwamba utumiaji wa ndizi unaweza kusaidia ufanisi wa kazi za kimetaboliki, kwa namna hiyo basi, uzito nao kupungua. [9] 


Huimarisha Mifupa

Uwepo wa fructooligosaccharide, ambaye ni prebiotic, ni bakteria mwenye faida kwenye njia yetu ya umeng'enyaji ambaye huchochea mwili kuchukua madini na virutubisho. Ndizi pia zimehusishwa kwenye ongezeko la ufyonzaji wa calcium. [10]Calcium ni element muhimu zaidi kwenye uzalishwaji na ukuzwaji wa mifupa kwenye mwili. Hupunguza uwezekano wa kuathirika na ugonjwa wa osteoporosis na kuishiwa nguvu kwa asili.



Sifa ya kuzuia Uvimbe

Tafiti zilizokusanywa kutoka kitengo cha  Ufamasia, Chuo Kikuu cha Aston, kilichopo Birmingham, UK na Shule ya Afya na Sayansi ya Michezo, Chuo kikuu cha North London, UK, zinaeleza ya kwamba kampaundi zilizomo kwenye ndizi ni vizuia uvimbe vya asili(anti-inflammatory), ikimaanisha zinaweza kupunguza uvimbe, inflammation na maumivu kwenye matatizo kama ya arthritis na gout. [11]  


Huimarisha Kuona

Ndizi, kama matunda mengine, yamesheheni viondosha sumu na carotenoids, vilevile mchanganyiko wa kiafya wa madini ambayo yanaweza kuimarisha afya ya macho yako. Ulaji wakawaida wa ndizi na matunda yanayoendana umeonyesha kutibu magonjwa ya macho kama macular degeneration, cataracts, night blindness, na glaucoma.


Huongeza Uzito

Ndizi zinaweza kuwa na umuhimu kwa kuongeza uzito. Zikiliwa na maziwa, ndizi husaidia kuongeza uzito wa mtu kwa haraka. Maziwa hutoa protini zinazohitajika na ndizi huchangia sukati. Zaidi, kwa sababu ndizi ni rahisi kumeng'enywa, mtu mwenye uzito mwepesi ana uwezo wa kula ndizi 4-6 kwa siku mbali na chakula chake cha kilasiku bila kupata tatizo la kupata choo. Hii hupelekea ongezeko la kalori 500-600, ambayo ni muhimu kwa ongezeko la uzito. Tokea ndizi kuwa na uwezo wa kutoa nishati papo hapo, wanamichezo hula ndizi kipindi mapumziko mafupi kipindi mechi zinaendelea kwa ajili ya kuongeza nishati ya ziada.



Unafuu wa Bawasiri

Ndizi zimekuwa zikitumika kama tiba asili kwa ugonjwa wa kidole tumbo kwani zina kiwango kikubwa cha fiber kinachowezesha kinyesi kutoka kwaurahisi. Athari za uwepesi huzuia aina yoyote ya shinikizo, hali hiyo huaaidia unafuu na kutibu hemorroids ( kuvimba kwa mishipa ya veins eneo linalozunguka njia ya kutolea haja kubwa).


Sifa ya kuzuia Vidonda vya Tumbo

Kitamaduni, ndizi zimekuwa zikitumika kama chakula chenye kutuliza acid tumbo linapochafuka kwani ndizi zina uwezo wa kuzuia utolewaji wa acid. Utafiti uliochapwa kwenye jarifa la British journal of Pharmacology  unadai kwamba ndizi zina sifa ya kuzuia vidonda vya tumbo. [12] Vizuizi vya protease kwenye ndizi huondoa bakteria wabaya ambayo wanahusika kwenye maendeleibya vidonda vya tumbo.



Huzuia Matatizo ya Figo

Tafiti iliyofanywa 2005 inadai kwamba potassium na baadhi ya viondosha sumu kwenye ndizi husaidia kutuliza ugumu kwenye figo na husaidia ukojoaji. [13] Hali hii husaidia sumu kutojilimbikiza kwenye mwili.


Hutuliza Matatizo ya Hedhi

Matumizi ya tiba asili ya ndizi ni pamoja na utumiaji wake wa kusaidia hedhi. [14] 
Maua yaliyochemshwa ya ndizi yanasaidia kwenye kutoa nafuu dhidi ya  maumivu na utokaji wa damu uliokithiri kipindi cha mzunguko wa hedhi na hutoa nafuu kwa matatizo mengine ya hedhi pia.


Diet ya Ndizi

Diet ya asubuhi ya ndizi kwa ajili ya  kupungua uzito imekuwa maarufu sana kiasi kwamba imesababisha kuwepo kwa uhaba wa ndizi kwenye maduka ya vyakula nchini Japan. Mpango huu wa diet unahusisha ulaji wa ndizi zisizo na idadi  pamoja na maji asubuhi, bila kujinyima chakula cha mchana na jioni. Na hakuna kula baada ya saa 2 usiku.



Madhara ya Utumiaji wa Ndizi

Ulaji wa ndizi unaweza kuwa na madhara athari hasi kama vile:

  • Kiwango kikubwa cha potassium: Baadhi ya madawa yanayotumika kwa ugonjwa wa moyo na presha ya kupanda yana uwezo wa kupandisha kiwango cha potassium kwenye mwili . Kwahiyo wale wanaotumia dawa wanashauriwa kupata ushauri wa daktari kabla ya kuanza kuongeza ndizi kwenye diet zao.
  • Allergy: Kwa wale ambao wana aleji wanaweza kuhisi kuwashwa, kuvimba na kukereketa kwenye koo na mdomo. 
  • Ndizi mbichi : Ndizi mbichi, endapo zikiliwa, huleta tatizo kubwa la mwili kushindwa kumeng'enya chakula na zinatakiwa kuliwa zikiwa zimepikwa tu. 
  • Migraine: Migraine ni hali kuumwa kichwa upande mmoja yenye kuambatana na kutoona vizuri upande unapoumwa kichwa. Kwahiyo kwa wale mnaopata mashambulizi ya migraine ya mara kea mara mnashauriwa kula si zaidi ya nusu ndizi kwa siku. 

Maoni