Faida 13 za kiafya za Vitunguu


Faida za kiafya za kuvutia za vitunguu (vitunguu maji) ni pamoja na uwezo wake wa kuzuia na kupoza dalili za ugonjwa wa kansa, matatizo ya moyo, na ugonjwa wa kisukari. Vinasaidia pia kwenye kutibu homa, pumu, maambukizi ya bakteria, matatizo yanayo ambatana na mfumo wa upumuaji, angina, na matatizo ya kifua.


Vitunguu

Vitunguu (Onions) ama kwa lugha ya kisayansi vinaitwa Allium cepa vipo kwenye kundi la mbogamboga, ambavyo vimekuwa vikitumika kwa upishi na kwenye tiba kwa maelfu ya miaka sasa. Vinguu vina kampaundi ambazo ni viondosha sumu vingi ambavyo vipo imara kwenye kuua sumu huru (free radicals) zinazopatikana kwenye mwili.

Vitunguu vimekuwa ni mimea yenye kutumika mara nyingi  kwenye vyakula kwa zaidi ya miaka 7,000 , na katika muda huo mwingi vitunguu vilikuwa vinalimwa. Bado kuna aina ya vitunguu pori kwenye baadhi ya maeneo ya bara la Asia, lakini kwa ujumla, kitunguu ni mmea unaokua na kulimwa dunia nzima. Katika  kipindi cha historia vilikuwa vinaabudiwa na baadhi ya tamaduni, kama wamisri ambao walikuwa wanavizika pamoja na firauni (pharaoh).
Sifa ya vitunguu kupambana na bakteria ni pamoja na uwezo wa juu wa kuzuia matatizo yatokanayo na fangasi, tabia hiyo invifanya kuwa ni tiba ya kwanza kwa kupunguza makali ya fangasi ukiwa nyumbani. Vitunguu vinaweza kupandwa kwenye udongo wenye unyevu na maji kiasi. Unaweza kulima hata uwani kwako au kwenye bustani kuvuna faida zake za kiafya. Vitunguu vinachukua eneo muhimu kwenye mapishi duniani kote na unaweza kulima pamoja na mbogamboga au mimea mingine.

Vitunguu vimekuwa vikijulikana kwa uwezo wake wa kutibu tokea zama za zamani. Hata Shirika la kimataifa la afya duniani (WHO) limethibitisha kuwa vitunguu vinawanufaisha wale waliopungukiwa hamu ya kula na wale wanaosumbuliwa na atherosclerosis (kujirundika kwa cholesterol mbaya na vitu vingine ndani na nje ya mishipa ya damu, hali inayopelekea damu kupita kwa shida). Wataalamu wa afya wanatujuza ukweli kwamba vitunguu hutoa mchango mkubwa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na ugonjwa wa pumu iliyokomaa, wenye allergy ya koo, na homa yenye kuambatana na kifua.


Ukweli wa Virutubisho kwenye Vitunguu

Vitunguu vina matumizi mengi yenye thamani kama tiba kwa sababu ya virutubisho, vitamini, madini, na kampaundi za asili zilizomo. Hizi zikiwemo kampaundi za sulfuric na quercetin pia. Mbogamboga hizi pia zina madini kama vile calcium, magnesium, sodium, potassium, selenium, na phosphorus, na pia ni chanzo kizuri cha vitamini C, vitamini B6, na nyuzinyuzi (dietary fiber) pia. 


Faida za Kiafya za Vitunguu

Kitunguu ni chanzo kizuri cha virutubisho muhimu ambavyo miili yetu inavihitaji. Ngoja tuone faida za kiafya zenye thamani na zenye kutambulika za vitunguu.

Matunzo ya Kinywa

Mara nyingi vitunguu vimekuwa vikitumika kuzuia jino kuharibika na maambukizi ya kinywa. Kutafuna  kitunguu kibichi kwa dakika 2 hadi 3 kunasaidia kuua vijidudu vilivyomo kwenye eneo la kinywa na maeneo yanayozunguka kinywa kama vile koo na lips. 


Huongeza kinga ya Mwili

Kemikali za asili zilizopo kwa wingi kwenye kitunguu zinafanya kazi kama kiamsho cha vitamini C ndani ya mwili. Vitamin C huamsha mfumo wa kinga ya mwili kupambana dhidi ya sumu na baadhi ya vitu vitokavyo nje ambavyo vinaweza kuleta magonjwa na kuugua.


Kupunguza Hatari ya kupata Maradhi ya moyo

Vitunguu hufanya kazi ya kuzuia damu kuganda, pia hujulikana kama vilainisha damu, ambavyo huzuia chembe hai nyekundu za damu kujirundika sehemu moja kuwa nzito.
Kulingana na ripoti ya Dr. Barry S. Kendler wa Manhattan College, kwamba utumiaji wa kanuni fulani za vitunguu saumu na/au vitunguu maji una mchango chanya katika kuzuia hatari ya kupata ugonjwa wa atherosclerotic.


Hudhibiti Ugonjwa wa Kisukari

Vitunguu vina madini ya chromium, ambayo ni madini yasiyo ya kawaida kupatikana kwenye vyakula. Chromium husaidia mwili kudhibiti kiwango cha na sukari ya kwenye damu na kuhakikisha utoaji wa taratibu, kidogokidogo wa glucose kwenye misuli na seli za mwili. Zaidi, ripoti ya tafiti ya Mathew PT na Augusti KT iliyochapwa kwenye jarida la 'Indian journal of Physiology and Pharmacology', ilionekana kwamba juisi ya kitunguu, ilipopewa kwa wagonjwa wakisukari pamoja na vyakula vyao, ilisaidia kudhibiti hyperglycemia (sukari ya juu ya damu) kisawasawa. [1] Kwahiyo basi, kula vitunguu kunaweza kusaidia  kuweka sawa viwango vya sukari ya damu, ambayo ni muhimu kwa wagonjwa wa kisukari.


Hutumika kama kifukuza wadudu

Unaweza kupaka maji maji ya kitunguu kupunguza maumivu ya kung'atwa na nyuki wa asali. Juice halisi ya kitunguu au paste inaweza kutumika kwa matumizi ya nje ya mwili kwa kutuliza maumivu ya kung'atwa na kuchomwa na  wadudu. [2] Harufu ya kitunguu pia husababisha wadudu kukimbia, ndo maana vitunguu vinaweza kutumika kama vifukuza wadudu vilevile kutumika kutuliza maumivu ya aina fulani za kung'atwa na wadudu.


Huzuia Kansa

Vitunguu vina utajiri wa kampaundi ambazo zina uwezo wa kuzuia ukuaji na usambaaji wa seli za kansa.
Vitunguu vina kiasi kingi cha quercetin, ambayo ni kiondosha sumu chenye nguvu, mara zote huunganishwa na kuzuia au kupunguza usambaaji wa kansa. [3] Tafiti zilizochapwa kwenye jarida la Utafiti wa uzuiaji wa kansa (Cancer Prevention Research) zimeonyesha kwamba [4] utumiaji wa mbogamboga kama vitunguu saumu na vitunguu maji ambavyo vinatokea kwenye kundi la  Allium husaidia kuzuia magonjwa ya kansa, hasa kansa ya utumbo.

Vitamin C, iliyopo kwenye vitunguu, pia ni kiondosha sumu chenye nguvu ambacho kinaweza kupunguza uwepo  na athari za sumu huru kwenye mwili. Sumu huru ni chemikali zilizotolewa na zisizohitajika na seli na zinaweza kubadilisha seli zenye afya kuwa seli za kansa. Kwahiyo, chakula chochotw chenye utajiri wa viondosha sumu, ambavyo vinaua nguvu ya sumu huru (free radicals), ni faida kwa kila mmoja.


Hutuliza Maumivu ya Sikio

Matone machache ya maji ya kitunguu yanaweza kuwa faida kubwa kwa watu wanaosumbuliwa na maumivu makali ya sikio. [5] Tatizo la kusikia sauti ya kengele kwenye sikio lilitibiwa kwa kupaka maji kitunguu kwenye sikio kwa kutumia kipande pamba.

Utunzaji wa Ngozi

Juisi ya kitunguu iliyochanganywa na asali au mafuta ya zeituni (olive oil) yanasemekana kuwa tiba bora ya kutibu dalili na alama za acne. [6] Kitunguu pia ni kizuia-uvimbe cha asili, kwahiyo kampaundi imara zilizopo kwenye kitunguu zinaweza kupunguza uvimbe unaohusiana na matatizo ya ngozi kama acne. Vitunguu pia vinasaidia kupunguza maumivu yanayohusiana na hali ya uvimbe kama gout na arthritis.


Hutibu Kifua

Ukila mchanganyiko wa juisi ya kitunguu na asali katika kipimo kilicho sawa inaweza kupunguza maumivu ya koo na dalili za kifua. [7] 

Huongeza Hamu ya Tendo la Ndoa

Vitunguu vinasemekana kuongeza uhamasishaji katika maisha ya afya ya tendo la ndoa. [8] Kijiko kimoja cha mezani cha juisi ya kitunguu ikiambatana na kijiko kimoja kilichojaa majimaji ya tangawizi, vikimezwa mara tatu kwa siku, inaweza kuamsha hamu ya kujamiiana.


Hutibu Anemia

Hata matatizo ya anemia yanaweza kupunguzwa kwa ulaji wa  vitunguu sambamba na Jaggery ( imetokana na miwa pamoja na tende) na maji kwasababu huongeza kiasi cha madini kwenye mwili, hasa madini joto (iron), ambayo ni sehemu muhimu katika uzalishaji wa seli hai nyekundu za damu. [9] Kwahiyo, anemia, ambayo hufahmika kama upungufu wa madini joto, inaweza kuzuiwa kwa kuongeza kitunguu kwenye msosi wako.


Hupunguza Maumivu ya Tumbo

Vitunguu vina sifa ya kuzuia uvimbe na bakteria ambayo inaweza kupoza matatizo makali yatokanayo na tumbo na yanayohusiana na maeneo mengine tumboni. [10] Hii ni kutokana na Saponin zinazopatikana ndani yake. Hizi saponins ni vizuizi vya hali zitokeazo ghafla bila taarifa, ambazo zinahakikisha kutokuendelea kwa matatizo ya tumbo na kwamba tumbo lako lipo shwari na kufanya kazi zake bila shida.


Hutibu Matatizo ya Mkojo

Kwa wale wanaosumbuliwa na hali ya kama kuwaka moto kipindi cha wanapokojoa, vitunguu hutoa mchango mkubwa wa kutuliza tatizo. [11] Watu wanaosumbuliwa na hali hii wanatakiea wanywe maji yaliyochemshwa pamoja grm 6 hadi 7 za vitunguu.

Kutokana na Peace Health, kwa muda mrefu tu vitunguu vimekuwa vikitumika kwa kupunguza hatari ya baadhi ya magonjwa  kama tumor, kifua kisichokoma, na homa. Watafiti wa madawa asili wanahesabu kitunguu kama ni tiba kamili ya nyumbani kwa kutuliza matatizo kadhaa ya mwili na magonjwa. Zaidi Peace Health imeeleza kwamba ulaji wa kitunguu unaweza hata kusaidia  kuzuia Kansa ya tumbo na matiti.


Hutuliza Pumu (Asthma)

Tafiti za madawa zimeweka wazi kuwa hizi kampaundi za sulfuric huzuia msululu wa kuwepo kwa dalili za pumu. [12] kiwango cha sulfuric cha vitunguu kina mchango wa kuyeyusha phlegm kwa mgonjwa anayesumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikali. Juisi ya kitunguu iliyotoka kutengenezwa inashauriwa kwa wagonjwa, waliopoteza fahamu, kwasababu ya harufu yake na ubora wa kunasa kwenye pua, kinaweza kurudisha nguvu na afya kwa ghafla.


Matumizi ya Upishi

Katika masuala ya kazi ya vitunguu kwenye upishi mbalimbali, vimekuwa vikitumika kwa maelfu ya miaka kwenye uandaaji wa vyakula vingi. Hasa vimekuwa vikitumika kwenye vyakula visivyo vya mbogamboga ili kuficha shombo na harufu ya nyama.
Vitunguu vinaweza kuliwa vibichi, vikiwa kwenye kachumbari, vilivyokaangwa, kuokwa au kuchemshwa.

Kwa hakika vitunguu ni muhimu sana kwa wanadamu na ijapokuwa vinatufanya tuwe tunatoa machozi  mara kadhaa, faida zake nyingi za kiafya zinafidia hapo.




Maoni