Faida 11 za kustaajabisha za mchanganyiko wa Asali na Mdalasini


Faida za kiafya za mchanganyiko wa asali na mdalasini ni pamoja na uwezo wake wa kuhimiza mfumo imara wa kinga ya mwili na mfumo wa umeng'enyaji, mchanyiko huu unaimarisha afya ya moyo, mifupa, ngozi, meno, na afya ya nywele, vilevile unahimiza uzito wa mwili kupungua. Pia huleta nafuu kwenye kuwashwa ngozi, na dalili za ugonjwa wa mgongo. Makala hii imebeba faida za kiafya za asali na mdalasini kipindi zinapochanganywa.

Asali peke yake ina faida nyingi tu ukiitumia peke yake, na pia ukiichanganya na vyakula vingine, mchanganyiko uliobora kabisa hutokea inapochanganywa na mdalasini, au tangawizi, au na maziwa.



Thamani ya Virutubisho vilivyomo kwenye mchanganyiko wa Asali na Mdalasini


Asali na mdalasini vyote ni vyakula vyenye virutubisho na vina vitamin na madini ambazo zina imarisha afya bora. [1] [2] vyote vina virutubisho kama maji, protini, fiber, sukari, vitamini, na madini. Mdalasini pia una kiasi kidogo sana cha fati.

Madini kama calcium, iron(madini joto), sodium, potassium, magnesium, phosphotus na zinc yanapatikana kwenye asali na mdalasini. Kwenye masuala ya vitamini, vyote asali na mdalasini vina vitamini A, E, D, na K.


Faida za kiafya za mchanganyiko wa Asali na Mdalasini

Faida za kiafya [3] za mchanganyiko huu ni kama zifuatazo [4]:

Huongeza Kinga ya Mwili

Mkorogo wa asali na mdalasini ni mzuri kwa kuhimiza mfumo wa kinga wa mwili kuimarika, huondoa uchovu usiokoma, na kuongeza umri wa kuishi mtu. [5]  Mchanganyiko huu unaweza pia kutibu homa na mafua (influenza). Kutokana na viondosha sumu vipatikanavyo kwenye asali na mdalasini ambavyo vinaweza kuungana na kupambana na sumu huru kwenye mfumo wa viungo vya mwili.



Hudhibiti Kisukari

Mdalasini una kiondosha sumu ambacho athari yake inakaribiana kufanana na insulin, ikimaanisha mdalasini unaweza 
Kutoa glucose kwenye njia ya damu na kupeleka kwenye seli ambapo huitajika kwa nishati. Asali, kama chanzo cha sukari asili, haisababishi kiwango cha sukari kwenye damu kufulika ambapo vyanzo vingi vya sukari visivyo vya asili husababisha kupanda kwa kiwango cha sukari kwenye damu, na athari za mdalasini, ikichanganywa na asali, huonyesha utumiaji wa glucose ulio imara na mwili, na na kuleta nafuu kwenye aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari (type 2 diabetes), kama somo lililochapwa kwenye American Diabetes Association mwaka 2003. [6]

Husaidia Kuzuia Ugonjwa wa Kansa

Mchanganyiko wa asali na mdalasini unaweza kusaidia kupunguza hatari ya ugonjwa wa kansa.
Asali inajulikana kuwa na chanzo cha utajiri viondosha sumu vinavyosaidia kuua sumu huru. Kiasi cha kutosha cha polyphenols kinachopatikana kwenye asali imehusishwa kwenye kuzuia ugonjwa wa kansa. Tafiti pia zinashauri kwamba asali nyeusi(dark honey) inaonyesha kuwa na kiwango kikubwa cha viondosha sumu kuliko ile safi(clear honey). [7]

Hutibu Miwasho

Mchanganyo uliotokana na asali na mdalasini mara nyingi hutumika kutibu kama umeng'atwa na wadudu warukao na kuzuia uvimbe eneo husika. Mdalasini 
huchukuliwa kama kitu kinachozuia uvimbe, wakati asali yenyewe huzuia vijidudu vieneza-magonjwa visivyoonekana kwa macho na ni ponyo. [8] Kwahiyo, mchanganyiko huu hufanya kazi kwenye matatizo yote ya ngozi kuwasha na kung'atwa na wadudu warukao kwa wakati mmoja, wakati huo ukikuweka mbali na maambukizi tarajari.


Husaidia Umeng'enyaji 

Mchanganyiko wa asali na mdalasini  unaweza kusaidia kuongeza ufanisi na afya ya mfumo wa umeng'enyaji. Unaweza kuondoa gesi kwenye tumbo na utumbo na kutibu maumivu ya tumbo, gesi iliyozidi, tatizo la ung'enyaji chakula, na maambukizi ya kibofu. Ulaji wa mara kwa mara wa mdalasini na asali utasaidia kwenye kuimarisha afya ya umeng'enyaji, ambapo mfumo wa chakula utalindwa dhidi ya matatizo hatarishi.


Hutibu ugonjwa wa Arthritis

Arthritis( hata siufahamu kwa jina moja la kiwahili) ni ugonjwa unashambulia maungio ya viungo, kuvimba na kukaza kwa maungio pamoja na maumivu makali kwenye maungio, ugonjwa huu unakuwa mbaya zaidi umri unavyosonga.

Asali na mdalasini huleta nafuu kwenye ugonjwa huu wa arthritis. [9] Ulaji wa mara kwa mara wa mchanganyiko wa asali na mdalasini husaidia kuimarisha afya ya mifupa na kupoza maumivu kwenye maungio. Unaweza pia kuchanganya asali na unga wa mdalasini kwenye maji ya moto kufurahia matokeo.


Matunzo ya Ngozi

Faida za asali na mdalasini zimekwenda hadi kwenye matunzo ya ngozi pia, ambapo maambukizi madogo ya ngozi na chunusi yanaweza kutibiwa na mchanganyiko huu rahisi wa vyakula hivi viwili vizuri. Unaweza kupaka kwenye jeraha au kwenye ngozi kutokana na sifa yake ya kuzuia uvimbe, kuzuia bakteria, na kuondosha sumu huru ndani ya ngozi. [10]

Huzuia matatizo ya Moyo

Asali na mdalasini huzuia kiwango cha cholesterol(lehemu) na kwa maana hiyo huongeza ulinzi wa moyo wako. [11] Kiwango cha juu cha cholesterol (LDL au cholesterol mbaya) huweza kusababisha atherosclerosis au vitu yabisi kujirundika ndani na nje ya kuta za mishipa ya ateri, kupelekea kuzuia damu kusafiri kwa urahisi na kupelekea mshtuko wa moyo au ugonjwa wa stroke.


Kupungua Uzito

Mchanganyiko wa asali na mdalasini kwenye maji ya moto ni chanzo kizuri cha kunguza uzito. Bila shaka, kama zilivyo tiba nyingine za kupunguza uzito, matokeo huonekana ukiambatanisha na  diet na mazoezi ya mara kwa mara. [12] 



Matunzo ya Nywele

Asali na mdalasini huimarisha nywele, hupunguza kunyonyoka kwa nywele na huchangia kukuza nywele. [13]

Huimarisha Meno

 Zote asali na mdalasini kila moja hutumika kwenye kutunza meno. Mchanganyiko wa asali mdalasini pia hutumika kwenye afya ya kinywa, hasa kwenye kuondoa harufu mbaya na meno yanayouma. 

Inaaminika ya kwamba mchanganyiko wa asali na mdalasini unaweza kutibu ugumba kwa wanaume, na matatizo ya kusikia, lakini utafiti zaidi unahitajika kufanyika kuhusiana na madai hayo. Hadi hapo, endelea kufurahia hizi faida uwr na afya zaidi.


Toa maoni hapo chini kama umependezwa na makala hii. Share kwa mtu inayomfa.

Maoni

  1. Asee, basi ni muhimu kuwa na mchanganyiko huu nyumbani.

    JibuFuta

Chapisha Maoni