Kitunguu swaum ama garlic kwa lugha ya kiingereza au unaweza kukiita Allium sativum kwa lugha ya kisayansi ni kiungo cha asili chenye harufu kali, ladha kali (pungent tasting) ambacho kimeonekana kuwa na faida nyingi kiafya. Sababu kubwa ni juu ya kampaundi yenye nguvu ya asili iliyomo kwenye kitunguu swaum, inayoitwa allicin. Faida za kiafya ni pamoja na kupambana na homa, kitunguu saumu/swaum husaidia kushusha presha ya damu na, kupambana na matatizo yanayoambatana na moyo na yawezekana pia vitunguu saumu vikasaidia kupambana na magonjwa yanayoshambulia neurons kwenye ubongo
Vitunguu Swaum ni nini?
Vitunguu swaum vinataka vikaribiane na vitunguu maji (onions), asili yake ni bara la Asia ya kati (Central Asia). Vimekuwa vikitumika kama viungo kwa kuongeza ladha kwenye chakula kwa miaka mingi, vilevile kwenye tamaduni na dawa tiba mbadala. Binadamu ametambua ubora wa kutibu wa dawa hii ya asili kwa zaidi ya miaka 3,000 iliyopita. Sir Louis Pasteur, mwanasayansi aliyegundua pasteurization ,alivitumia vitunguu swaum kwa uwezo wake kuzuia bakteria kwa kipindi kirefu toka mwaka 1858. [1] Ripoti iliyotolewa kwenye jarida la Journal of Pharmaceutical Research imependekeza kwamba ulaji wa punje moja ya kitunguu swaum kwa siku unaweza kuongeza uimara mkubwa afya yako kwa ujumla, wakati ulaji wa punje mbili hadi tatu kila siku husaidia kuweka homa mbali nawe.[2]
Virutubisho
Kitunguu swaum kina uchache wa calorie, saturated fat, na sodium. Kina madini mengi ya muhimu kama phosphorus, potassium, magnesium, zinc, calcium, na iron (madini joto), bila kusahau madini adimu kupatikana kama iodine, sulfur, na chlorine.
Kulingana na Database ya kitaifa ya virutubisho kutoka USDA, kitunguu swaum ni chanzo cha utajiri wa B-vitamins (folate, thiamine, niacin, na B6), na vitamin C, A, na K. Kitunguu swaum ni moja chanzo adimu cha chakula chenye kampaundi za asili muhimu, allicin, allisatin 1, na allisatin 2.[3]
Faida za Vitunguu Swaum Vibichi
Faida za kiafya za ulaji wa punje za vitunguu swaum vibichi zimeelezewa kwa undani kama ifuatavyo.
Huondoa Homa na Kifua
Jarida lililochapwa mwaka 2014 kwenye 'Cochrane Database of Systematic Reviews' liliangaza kwenye tafiti iliyofanyika kwa wagonjwa 146 ndani ya miezi mitatu kuchunguza athari iliyowafika wagonjwa wanaosumbuliwa na homa na kifua. [4] Kama sehemu ya utafiti, jumla ya idadi ya washiriki iligawanywa kwenye makundi mawili yaliyo sawa. Kundi moja lilichukua kidonge cha Placebo wakati kundi lingine lilibeba kidonge cha kitunguu swaum.
Mwisho wa tafiti, ilionekana kwamba watu waliotumia kitunguu swaum kila siku kwa miezi mitatu badala ya placebo walikuwa na dalili chache za homa ukilinganisha na kundi lilitumia placebo. Kwa maana hiyo, ulaji wa punje za kitunguu swaum unaweza kuondoa dalili za homa na kifua.
Hupunguza Shinikizo la juu la damu(Hypertension)
Kitunguu swaum hutumika mara nyingi kwa kupunguza presha ya juu ya damu. Kitunguu kikiwekwa kwenye viwango vya juu vya damu, kitu kinachojulikana kama nitric oxide hulegeza mishipa ya damu na kusababisha itanuke. Pia hupambana dhidi ya thrombosis(ufanyikaji wa madonge ya damu ndani mishipa ya damu na kusababisha kuzuia damu isipite sawia) .
Hupunguza kiwango cha Cholesterol
Kwa mara nyingine tena, Kitunguu swaum kibichi, chenye utajiri wa kampaundi asilia ya allicin huzuia LDL ( cholesterol mbaya ). Baadhi ya tafiti zimeonyesha kupunguka kwa cholestetol na triglycerides kwa panya waliokula kitunguu swaum. Hata hivyo kufikia hatua hii, hakuna tafiti ya kutosha iliyofanywa kuhakikisha hilo.
Huimarisha Afya ya Moyo
Kitunguu swaum kinafikiriwa kuwa na sifa muhimu za kulinda moyo, ambapo husaidia kuzuia magonjwa kama atherosclerosis, hyperlipidemia, thrombosis, hypertension, na mengineyo. Wakati uchunguzi mwingi uliofanyika unaunga mkono mahusiano ya kati ya ulaji wa kitunguu swaum na ulinzi wa moyo, tafiti zaidi zahitajika kujua kiwango kamili na dozi. Unatakiwa kufahamu utumiaji sahihi wa kitunguu swaum ikimaanisha kutumia maandilizi tofauti tofauti yaliyopo, dozi, muda wa kutumia na muingiliano wake na madawa ya hospitali. [5]
Sifa ya kulinda Ubongo
Sifa ya kuondosha sumu na kuzuia uvimbe ya kitunguu swaum kibichi inaweza kuzuia magonjwa ya ubongo yanayoweza kujitokeza siku za usoni. [6]
Huzuia Sumu za metali nzito
Dozi kubwa ya ulaji wa kitunguu swaum inaweza kuzuia kuharibika kwa viungo kunakosababishwa na metali nzito. Kampaundi za sulfur kwenye dawa-asili hii hupunguza viwango vya metali ya lead kwenye damu.
Kwa kuongezea, pia huzuia dalili za sumu, kama kichwa kuuma na shinikizo la damu. Sulfur pia husaidia ufyonzaji mzuri wa madini joto (iron) na zinc kwenye damu. Ripoti iliyochapwa mwaka 2012 kwenye jarida la 'Basic and Clinical Pharmacology and Toxicology' limeweka wazi kwamba kitunguu swaum kina msaada mkubwa kwenye kupunguza tishu za damu zenye wingi wa lead kwa baadhi ya binadamu, halikadhalika na wanyama. [7] Bila shaka, kama unashauku kuhusu sumu za metali nzito, ni vyema ukaonana na mtaalamu wa madawa kwa matibabu.
Huponyesha Jeraha
Hufanya kazi kama tiba mbadala kwa jeraha. Weka punje mbili zilizosagwa za kitunguu swaum kwenye eneo ulipoumia kupata nafuu ya haraka.
Afya ya Mifupa
Viungo kama kitunguu swaum na kitunguu maji vinasemekana kutoa mchango kwenye viwango vya estrogen kwa wanawake waliokoma hedhi (menopausal women), kupunguza hatari ya kupata osteoathritis(ugonjwa unaoshambulia maungio ya mifupa). [8] Vinaweza pia kupunguza kupotea kwa mifupa na kuimarisha afya ya mifupa.
Huongeza uwezo wa Umeng'enyaji Chakula
Ulaji wa kila siku wa punje mbichi za kitunguu swaum kwenye msosi wako husaidia kuondoa matatizo ya umeng'enyaji chakula.
Hata kuvimba au kuuma kwa njia ya chakula kunaweza kupunguzwa kwa kutumia tiba hii asili. Inasemekana kwamba kitunguu swaum kinasaidia matatizo mengi yanayohusu utumbo kama kuharisha, kuharisha damu (dysentry), na colitis. Kazi yake ya kuondoa kabisa minyoo ni ya uhakika. Kitunguu swaum hakiharibu bakteria wazuri kwenye utumbo lakini huharibu wale wabaya. Haisaidii kuwezesha umeng'enyaji chakula pekee, lakin pia husaidia kuondoa gesi tumboni.
Huweka sawa Sukari ya Damu
Ulaji wa punje mbichi za kitunguu swaum moja kwa moja hupunguza kiwango cha sukari kwenye damu, kwenye somo mojawapo la mnyama.
Kwa maana hiyo ina lweza kikombozi kwa wale wanaosumbuliwa na kisukari au walio na hatari ya kuugua kisukari. [9]
Huongeza Kinga ya Mwili
Kitunguu swaum kina virutubisho vinavyosaidia kupunguza shinikizo la sumu, kwahiyo, huimarisha kinga ya mwili. Zaidi, kitunguu swaum hupunguza uchovu, pia huongeza nishati ya mwili na uwezo wa kudumu kufanya kazi bila uchovu. Ripoti ya 2012 kwenye jarida la African Journal of Traditional, Complementary and Alternative Medicines liliweka wazi utafiti uliofanywa kwa panya kuona kama kitunguu swaum kina mchango wa kuimarisha kinga ya mwili. [10] baada ya panya kupewa chenye kitunguu swaum (Allium sativum) katika uwiano tofauti tofauti iligundulika kwamba, chakula, hasa kile chenye kitunguu swaum kwa wingi, kilisababisha kuongezeka kwa seli hai nyeupe za damu, na kuonyesha matokeo ya kuimarika kinga.
Matunzo ya Macho
Kitunguu swaum kina utajiri wa virutubisho kama selenium, quercetin, na vitamin C, vyote vikiwa vina mchango kwenye afya ya macho na kusaidia kwenye maambukizi ya macho na uvimbe. [11]
Huzuia Chunusi
Kitunguu swaum, pamoja na nyongeza nyinginezo kama asali, cream, na binzari, vinaweza kutumika kama tiba ya nyumbani ya madoa ya chunusi na hata kuzuia kabisa uwepo wa chunusi usoni. [12] . Dawa hii ya asili ni kisafisha ngozi kizuri na hupambana na bakteria ambapo husaidia kutatua matatizo kadhaa ya ngozi, ikiwemo harara, psoriasis, cold sores, na blisters. Pia husaidia kwenye kuilinda ngozi dhidi ya miale mikali ya jua, na kudhoofisha hali ya uzee.
Kwa tatizo la presha ya kupanda nashariwa kutumia kitunguu swaumu mara ngapi kwa siku? Na
JibuFutaNawezaje kuondoa harufu kali ya kitunguu swaumu mdomoni