Maajabu 5 ya Tango kwenye mwili wako.


Tango/matango ni zao lenye faida kwa afya ya mwili 
kiujumla na huliwa hasa kipindi cha majira ya joto kutokana na wingi wa maji uliosheheni ndani ya tango.
Matango pia yana utajiri wa virutubisho ambavyo ni muhimu kwa binadamu.

Tango zuri lina utajiri wa vitamin A, vitamin C, na Folic Acid, wakati ngozi ngumu ya nje ina utajiri wa nyuzi nyuzi (fiber) na aina kadhaa za madini yakiwemo Magbesium, Molybdenum na Potassium.


Kuhusu Tango

Matango yameanzia nchini India karibia miaka 10,000 iliyopita, lakini sasa hivi yanalimwa kwenye nchi nyingi. Aina tofauti tofauti za matango huuzwa kwenye soko la kimataifa na utayaona mengi mno karibia mwaka mzima.

Kwenye zama za zamani zilizostaarabikaza Misri, Ugiriki na Rumi, tango lilikuwa maarufu kwelikweli, na matumizi yake hayakuishia kwenye kutumika kama chakula tu. Ilikuwa likiheshimika kwa sifa yake ya kuleta athari chanya kwenye ngozi. Mfalme Louis XIV aliyapenda mno matango na mtindo wa kuyalima kwenye greenhouse uliundwa kipindi chake kuhakikisha aweze kuyapata na kufaidi matunda hayo msimu wowote. Hata wakoloni waliotawala Marekani walipeleka matango huko.

Bado haijajulikana ni kipindi gani matango yalianza kutumika kwenye kachumbari, lakini watafiti wanakisia ya kwamba aina mojawapo ya matango (ambayo yanaitwa 'gherkin' kwa kiingereza) yametokea kwenye mmea wa kiafrika.
Uhispania ilikuwa nchi mojawapo, kipindi cha zamani, iliyoanza kutumia matango kwenye  kachumbari toka watawala wa kirumi walipoyaingiza kutoka nchini kwao.

Matango yana utajiri wa virutubisho mbalimbali, vitamini, madini, nishati, na maji. Kutokana na tafiti za USDA matango ni chanzo kizuri cha Potassium, Phosphorus, vitamin C, na vitamin K. Pia yana kiasi kidogo cha madini joto, madini ya Sodium, na vitamini B ( riboflavin, niacin, na vitamin B-6).

Faida za Matango Kiafya

Faida za matango ni nyingi, kuanzia kutoka kwenye kuzuia acidity hadi kuifanya ngozi kuwa nzuri.

[Kuna baadhi ya maneno kama ume-notice nashindwa kutumia kiswahili kwa dhumuni ya kuelewana, kuna muda lugha yetu inakuwa ngeni kuliko lugha ngeni yenyewe].

1.Utunzaji wa Ngozi

Matango yana utajiri wa Silica, ambayo ni mhimili mkubwa unaosaidia kuendeleA tishu imara na zenye afya za misuli, ligaments, tendons, cartilage, na mifupa. Madaktari hushauri juisi ya matango kwa sababu ya silica iliyomo kwa ngozi yenye afya na ang'avu. Maji mengi ya tango yanaifanya ngozi kuwa na unyevu wa asili.

Ascorbic na Caffeic acid ni kampaundi mbili muhimu kwenye tango zinazosaidia kuzuia kupotea kwa maji kwenye mwili.

Matango hutumika kutibu matatizo kadhaa ya ngozi kama sunburn (ngozi kuathirika na miale mikali ya jua) na kuvimba kwa macho
Pia yanaweza kutumika kusaidia matatizo mengine ya ngozi kama psoriasis, eczema na acne (chunusi) . Hizi ni baadhi ya sababu kwanini matango yanatumika kutibu magonjwa kadhaa ngozi.

2. Huzuia  Constipation na Mawe kwenye Figo

Matango yana mchanganyiko kamili wa nyuzi nyuzi (fiber) na maji. Kwahiyo yanaulinda mwili wako kutokana na kutopata choo (constipation) na mawe kwenye figo. Mara nyingi kula kachumbari yenye matango ni namna nzuri ya kupata fiber. Tango pia ni chanzo kizuri cha vitamin C, silica, Potassium na Magnesium; vyote vina faida zake binafsi za kiafya.
Ngozi ya Tango ina kiwango kikubwa cha vitamin A, kwahiyo utaongeza faida ya kirubisho hiki kwa kula tango bila kumenya.

3. Hudhibiti Presha ya Damu

Somo lililofanyika DASH (Dietary Approaches to Stop Hypertension), chakula kamili kiliandaliwa kutoka na tafiti kutoka taasisi ya kitaifa ya Afya ya Marekani kama njia ya kusaidia kudhibiti presha ya damu. Iligundulika kwamba kutumia vyakula vyenye wingi wa magnesium, potassium, na fiber ndiyo funguo yenyewe. Wale waliokula chakula chenye mchanganyiko huo, pamoja na vyakula vingine kama vya bahari, vyakula vyenye mafuta kiasi vilivyotokana na maziwa, nyama ya kuku, ilionekana presha yao kushuka. Tango kwa maana hiyo, husaidia kudhibiti presha ya damu na kusaidia mpangilio mzuri wa tishu kwenye mwili wako zikiwemo zile za kwenye misuli, mifupa, ligament, na tendon.

4. Hudhibiti Kisukari

Tango limekuwa likitumika kusaidia kudhibiti glucose kwa wagonjwa wenye kisukari. Lina homoni inayohitajika na seli kipindi cha uzalishwaji wa insulini. Uwepo wa Carbohydrate na athari yake kwenye mwili hupimwa kwa kipimo kiitwacho Glycemic Index (GI). Glycemic Index hupima namna carbohydrate inavyochangia ongezeko la kiwango cha glucose (sukari ya damu) kwenye damu. Kila aina ya chakula ina virutubisho muhimu katika kiwango tofauti tofauti. Glycemic Index ya Tango ni sifuri [0], ikiwa na maana ni chaguo zuri kwa mgonjwa wa kisukari, na, kwa maana hiyo, inafanya kiwango cha sukari kiwe kwenye uangalizi mzuri.

5. Huchangia Nguvu ya Kuondosha Sumu


Tango huwa kama kiondosha sumu likiliwa pamoja na vyakula vy viwandani na vile vyenye sukari nyingi. Kama ilivyochapwa kwenye jarida la The Journal of Nutrition, Health, and Aging, ulaji wa unga wa tango kwa muda wa mwezi mzima unaonesha kuongezeka uwezo wa mwili kuondosha sumu.





Maoni

  1. Nashukuru kwa elimu hii nzuri sana, umeniongezea kitu, umenipa maarifa zaidi. Mungu akubariki kwa kazi hii nzuri ya kuelimisha watu wake juu ya ubora wa MIMEA.

    JibuFuta

Chapisha Maoni