Jambo la kushangaza ni kwamba chai ya tangawizi na binzari husaidia kuondoa uvimbe, kuongeza nguvu ya kinga ya mwili dhidi ya magonjwa, huboresha mfumo wa umeng'enyaji chakula, hupunguza maumivu, na kuongeza uwezo wa utambuzi wa mtu. Pia husaidia kulinda moyo, kudhibiti kisukari, kupunguza kiwango cha wasiwasi, na kuboresha ubora wa ngozi.
Binzari kama kiungo, imekuea ikiumika kwenye nchi za bara la Asia kama India kwa matumizi ya mapishi. Hata hivyo, kutokana na tafiti inayoendelea juu ya utajiri wa curcumin iliyopo kwenye binzari, sasa unaweza kuiona karibu kwenye kila nyumba dunia nzima. Unapokunywa chai ya binzari ni namna nzuri ya kuongeza kiungo hiki kwa afya bora kwenye shughuli zako za kila siku.
(Curcumin ni kemikali yenye rangi ya manjano inayopatikana kwenye jamii ya miziz ya binzari )
Chai ya Tangawizi na Binzari
Chai hii inaandaliwa kwa kuloweka tangawizi na binzari mbichi kwenye maji ya moto kwa pamoja. Tangawizi (Zingiber officinale) na binzari (Curcuna longa) hutumika kila moja kivyake kwa namna ya kurutubisha na pia hutumika kama dawa pia. Dawa hizi mbili za asili zenye nguvu zimesambaa Dunia nzima na zimefanyiwa tafiti kutokana na umaarufu wake.
Chai ya binzari ni kama ibada huko Okinawa, Japan ambapo kuna wingi wa watu wenye umri mrefu zaidi duniani, hii inakuhakikishia kwamba kinywaji hiki cha manjano ni kinaongeza umri wa kuishi.
Chai ya binzari ni kama ibada huko Okinawa, Japan ambapo kuna wingi wa watu wenye umri mrefu zaidi duniani, hii inakuhakikishia kwamba kinywaji hiki cha manjano ni kinaongeza umri wa kuishi.
Faida za Chai ya Tangawizi na Binzari
Tuone faida za chai hii kwa undani.
1. Hulinda Afya ya Moyo
Masomo kadhaa yaliyofanyika yamegundua kwamba tangawizi na binzari zote zina nguvu ya kupunguza kiwango cha cholesterol, haswa LDL cholesterol. LDL ina mchango mkubwa wa kuziba mishipa ya Ateri (arteties) kwa kuzuia damu kupita kwa urahisi, ambayo hupelekea mtu kupatwa na hatari ya mishtuko ya moyo na hata kiharusi.
2.Huboresha Utambuzi
Asili ya tangawizi kuchangamsha ubongo inafahamika vizuri, na mchanganyiko wa kipekee wa viondosha sumu vipatikanavyo kwenye chai hii inaweza kusaidia kuweka sawa matendo ya ubongo, kuongeza umakini, na kupunguza mrundikano wa protini iitwayo beta amyloid, ambayo husababisha ugonjwa wa Alzheimer (Alzheimer's disease) , na dementia. Hii ilihakikiwa kwenye tafiti iliyofanywa na Dr. Shrikant Mishra, Department of Neurology Care Center, Calfornia, US .
3. Ina Sifa ya Kupunguza Maumivu
Curcumin na gingerol, ni kemikali mbili za asili muhimu zinazopatikana kwenye chai hii, zina sifa ya kupoza maumivu, ikimaanisha zinaweza kupunguza maumivu mwili mzima. Hii ikiwa ni nyongeza ya kuwa na sifa ya kuzuia uvimbe ambayo inaweza kupoza maumivu ya maungio ya viungo na maeneo mengine yenye kusumbua ya misuli na tishu za mwili. Kuna ushahidi pia kwamba binzari ipo vyema kwenye kupunguza maumivu ya maungio ya viungo yanayohusiana na ugonjwa wa uti wa mgongo
4. Huongeza Nguvu ya Kinga ya Mwili
Chai ya binzari na tangawizi huongeza ufanisi wa kuzuia vijidudu nyemelezi vya magonjwa ( antimicrobial, antibacterial, anti-fungal, na ni antiseptic ) ambayo huifanya chai hii kuwa kisaidizi muhimu cha mfumo wa kinga ya mwili, kulingana na tafiti iliyofanywa na Dr. Shalini Tattari et al.,National Institute of Nutrition, Hyderabad, India.
Kama unasumbuliwa na kinga dhaifu ya mwili na homa inakushika mara kwa mara, chai hii ya dawa inaweza kuwa mkombozi wako. Kwa kuongeza zaidi, kwa kifua, homa, na kutopata haja kubwa, mchanganyiko wa vitu hivi vyenye nguvu husaidia kuharakisha kupona na kuondoa maradhi yanayokusumbua.
5. Utunzaji wa Ngozi
Binzari kwenye chai hii ya tiba imekuwa ikitumika kutibu matatizo ya ngozi, hasa chunusi na matatizo mengine kama psoriasis na eczema. Kemikali ya gingerol iliyopo kwenye chai hii pia ni kiondosha bakteria na kiondosha sumu kizuri ambayo inalinda ngozi na maambukizi, kipindi ambacho huchangia ukuaji wa seli mpya na kuzuia alama za kuzeeka, kama mikunjo na mabaka, kwahiyo, hutaki kuzeeka, kunywa chai ya binzari na tangawizi.
6. Husaidia Umeng'enyaji wa Chakula
Tangawizi ina uwezo mkubwa wa kuzuia tabia ya uvimbe kwa viungo ambayo inasaidia tumbo kutulia, kupunguza hali ya kutaka kutapika, na kuchangia umeng'enyaji mzuri wa chakula. Inaweza kusaidia chakula kupita kwa urahisi kwenye njia yake (peristalic motion) .
Kwa maana hiyo matatizo ya kutopata choo utayasikia kwa jirani. Chai ya binzari na tangawizi inaweza pia kusaidia kutibu Irritable Bowel Syndrome (IBS) [ IBS ni tatizo linalotokea kwenye utumbo mdogo ambalo hupelekea tumbo kuuma, kunyonga, na kuhara au kutopata choo], hata vidonda vya tumbo pia!
7. Hudhibiti Ugonjwa wa Kisukari
Tafiti iliyochapishwa kwenye jarida la Kiingereza la Chakula bora (British Journal of Nutrition) imeonyesha kuwa uwezo wa tangawizi na binzari kudhibiti sukari ya damu umefahamika vizuri, kwahiyo kwa pamoja zikichanganywa, zina mchango mkubwa wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa kisukari. Kwa kuweka kiwango cha glucose na insulini katika usawa unaohitajika, chai ya binzari na tangawizi inazuia ongezeko na kupungua kwa kasi sukari iliyopo kwenye damu ambayo ni hatari kwa kuleta ugonjwa wa kisukari.
Namna ya Kuandaa Chai ya Binzari na Tangawizi?
Chai ya binzari na tangawizi inaweza kuandaliwa nyumbani kwa urahisi na unachotakiwa kuwa navyo ni tangawizi mbichi, binzari mbichi, limao, asali, na pilipili manga. Kwa hiyo hivi ndivyo unavyoweza kuandaa chai ya binzari na tangawizi nyumbani.
Vinavyohitajika:
- Maji masafi (kikombe kimoja)
- Tangawizi iliyosagwa (kijiko cha chai)
- Binzari iliyosagwa/ ya unga (kijiko 1-2)
- Asali/maji ya limao (kijiko cha chai)
- Pilipili manga ya unga (kijiko cha chai)
Maelekezo:
- Kupika chai ya binzari na tangawizi, kwanza, chemsha maji kwenye sufuria.
- Kabla hujaanza, ungependelea tangawizi mbichi ambayo tayari imeshasagwa kwa kuandaa chai. Vivyo hivyo kwa binzari pia, uipate mbich na uisage kwa ajili ya kuandaa chai hii.
3. Weka binzari na tangawizi iliyosagwa, punguza moto ichemke taratibu.
4. Acha mchanganyiko uchemke kwa dakika 10-15. Unaweza kuuacha kwa muda mchache zaidi kama huna mpango wa kuifanya iwe kali.
5. Mimini chai kwenye chupa ya chai. Weka pilipili manga, maji ya limao, na asali, na furahia chai yako.
Kwa mara ngapi natakiwa kunywa chai ya binzari na tangawizi ?
Chai hii ina nguvu sana, kwahiyo kunywa kikombe kimoja cha chai hii muhimu inatosha kupata faida zilizotajwa hapo juu. Kunywa zaidi ya hivi si tu ni hatari, bali huleta athari ya madhara mengine.
Madhara ya Chai ya Binzari na Tangawizi
Madhara ya chai ya binzari na tangawizi kwa ukubwa huletwa na utumiaji uliokithiri wa chai hii, madhara hayo ni matatizo yanayotokea kwenye utumbo (gastrointestinal problems). Pia yanaweza kutokea kutokana na muingiliano wa dawa za hospitali, matatizo ya ujauzito, unywaji uliokithiri wa chai, ambao haushauriwi.
Andika maoni yako kama umewahi kujaribu Chai hii ya tiba.
Asante kwa darasa. Binzari mbichi ni adimu je, binzari ya unga si inafaa?
JibuFutaAsante kwa kupitia makala hii. Ndio, binzari ya unga pia inafaa.
FutaSafi elimu nzuri
JibuFutaTangawizi,binzari zilizokaushwa na usagwa zinafaa?
JibuFuta