Faida za kushangaza za binzari na curcumin ni kama zifuatazo, ikiwemo uwezo wa kupunguza uvimbe, kutibu vidonda, kuboresha afya ya ngozi, kulinda uwezo wa utambuzi, na kupoza maumivu ya hedhi.
Binzari pia husaidia kuondoa msongo wa mawazo, kupunguza maumivu, kupunguza kasi ya uzee, kulinda njia ya umeng'enyaji chakula, na kuzuia kansa.
Binzari ni nini?
Inataka kufanana na jamii nyingine ya familia ya tangawizi, binzari (turmeric) kwa jina la kisayansi huitwa,Curcuna longa, ni zao linaloweza kuishi zaidi ya miaka miwili (perennial crop), ni mti shamba, asili yake ni India. Binzari inafanana na tangawizi mbichi ,kabla ya kupatikana kwa unga wake muhimu kwa matumizi.
Huitaji jotoridi la kiasi na mazingira ili kustawi, kwahiyo si zao linaweza kulimwa dunia nzima lakini husafirishwa duniani kutokana na namna inavyopendwa.
Rangi kali ya njano ya mti shamba huu yawezekana ikawa ndio sifa yake kuu.
Itakuwa umewahi kuiona, hata kama hukuitambua, na kama umewahi kufaidi chakula cha kihindi , basi kwa hakika utakuwa umewahi kuionja au kuila.
Virutubisho
Binzari ni moja ya mmea wenye utajiri wa virutubisho vingi mno. Yasemekana, kutokana na USDA, binzari ina kiasi kizuri cha protein, vitamin C, calcium, iron (madini joto), nyuzi nyuzi (dietary fiber), sodium, na kalori 24 kwenye kijiko kimoja cha mezani chenye unga ya binzari. Pia inachangia utoaji mkubwa wa vitamin B6, potassium, magnesium, na manganese.
Faida za binzari na curcumin
Curcumin ndio kompaundi au kemikali pekee ipatikanayo kwenye binzari, na ndiyo inaipa rangi kali ya manjano.
Faida kuu za kiafya za binzari na curcumin ni kama zifuatazo:
1. Anti-Inflammatory
Tabia au sifa ya kitu kuzuia hali ya uvimbe isitokee.
Binzari, kutokana na uwepo wa curcumin, inafanya kazi kama wakala wa kuzuia uvimbe kwenye mwili (anti-inflammatory agent), wanasema watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Arizona, Tucson, USA. Kiukweli hata kiasi kidogo tu cha binzari kinaweza kupunguza uvimbe wa hemorrhoids.
2. Utunzaji wa Ngozi
Binzari husaidia kuweka ngozi yako kwenye afya kwa namna nyingi.
- Huondoa chunusi kwa kuzuia bakteria wanaosababisha chunusi na kupunguza uzalishwaji wa mafuta na tezi za mafuta kwenye ngozi (sebaceous glands)
- Utumiaji wa kudumu wa binzari hufuta mabaka ya ngozi, ambayo huifanya ngozi yako kuwa bila karaha na yenye kuwaka.
- Tabia yake ya kuzuia bakteria na kuzuia uvimbe inaharakisha kuponesha jeraha la lililotokana na kujikata na kitu chenye ncha kali na kupooza muwasho wa ngozi.
- Curcumin iliyopo kwenye binzari ni kiondosha sumu kinachopambana na ishara za uzee kama mikunjo na mabaka kwa kuharibu ukuaji wa free radicals (sumu huru).
3. Utajiri wa Viondosha Sumu
Curcumin inayopatikana kwenue binzari ni wakala mkubwa wa kuondosha sumu ambayo husaidia kwa namna nyingi ikiwemo faida zake nyingi za urembo na tiba. [1] Somo lililofanyika na watafiti kwenye chuo kikuu cha Edinburgh, iliichapa makala kwenye jarida la 'the Antioxidants & Redox Signaling', iliyoangazia umuhimu wa kazi ya uondoshaji sumu wa curcumin.
4. Kupunguza Uzito
Kiungo cha dhahabu, binzari, husaidia kasi ya hufanyaji kazi wa mfumo wa chakula na kusaidia mwili wako kuunguza kalori nyingi, kitendo kinachopelekea kupunguza uzito. Ina saidia pia kwenye kupunguza mafuta yaliyoganda na kusaidia Ini kuondoa sumu, ambavyo ni vitu vya muhimu sana linapokuja swala la jitihada ya kupata 'diet' ya kupunguza uzito. Pia, na curcumin, binzari inaweza kuwa kirutubisho muhimu kwa kupunguza uzito kwani kinashusha kiwango cha LDL (Cholesterol mbaya). Pia ina wajibika vilivyo kwenye kuzuia taarifa za vivimbe kwenye misuli, kongosho, na seli za mafuta. Kwahiyo, kipindi mwili wako haupambani na uvimbe, kwa urahisi binzari inaweza kufocus kwenye kupunguza uzito kirahisi
5. Huboresha Afya ya Ini
Binzari na kampaundi zake muhimu za asili zilizosheheni zimegundulika kuimarisha ufanyaji kazi wa ini na kupunguza kiwango cha sumu kwenye mwili kwa kuweka sawa mfumo limfu (lymphatic system) na kuondoa sumu kiuhakika
Kutokana na tafiti iliyofanywa 2018, uwezo wa kuondoa sumu wa binzari unaweza kuwa msaada kwenye kupunguza kuharibika kwa ini na kiungo hiki kinaweza kutumika kama mbadala wa kutibu matatizo ya ini kama cirrhosis na fatty liver disease [2].
6. Huboresha Kazi za Ubongo
Kweny matibabu ya kitamaduni, mara zote iliegemea kwenye kuongeza uwezo wa utambuzi, kuongeza umakini, na kuongeza uwezo wa kumbukumbu. Nyingi katika hizo imani za kitamaduni ziliishia kuhakikiwa na tafiti, na binzari bado inakuwa ni dawa yenye kuongeza ufanisi wa ubongo. [3] Inaweza pia kulinda njia ya mfumo wa neva za fahamukutoka na mlundikano wa muda mrefu wa sumu.
Dr. Yousef Tizabi et al., wa Howard University College of Medicine, kwenye jaribio, alithibitisha uwezo wa athari za curcumin kwenye kuimariaha neva za fahamu, ambapo jaribio hilo lilifanywa kwa panya. [4]
7. Huzuia Damu Kuganda
Unga wa binzari una nguvu kubwa ya kulainisha damu kutokana na uwepo wa curcumin ndani yake. Curcumin inazuia chembe chembe za damu kushikana pamoja.
8. Huboresha Afya ya Moyo
Binzari yenye utajiri wa curcumin na vitamin B6 pia inaboresha afya ya moyo. Vitamin B6 inaweza kudhibiti na kuzuia uzalishwaji wa homocysteine, ambayo ni zao hasi linaloharibu kuta za seli. Hizi kuta dhaifu zinaweza kuleta matatizo ndani ya moyo, hasa ikishinikizwa na presha ya juu ya damu.
Moja kwa moja Curcumin inaweka sawa kiwango cha cholesterol kwa kuondoa cholesterol mbaya iliyozidi (LDL) kutoka kwenye Ateri na mishipa ya damu. Hii inaweza kusaidia kuzuia atherosclerosis (kitendo cha cholesterol, fat na vitu vingine kujijenga kwenye kuta za ateri ndani na nje ya ateri) , na ikijumuishwa kwenye mishipa imara ya damu, dawa hii ya asili ina inatoa suluhisho pana mno kwa matatizo yanayohusu moyo, kama tafiti ya kawaida iliyofanyika kwenye Cardiology. [5]
9. Sifa ya Kuzuia Kansa
Jaribio lililofanyika juu ya panya na watafiti Taasisi ya Utafiti wa Kansa, Tata Memorial Center, Mumbai, India kumenukuliwa uwezekano wa athari ya binzari kuzuia kansa ya tumbo na ngozi. [6] Jaribio kubwa la utafiti wa athari za binzari kwenye kuzuia kansa ulifanyika kwenye kansa ya utumbo mkubwa (colon cancer) ambapo aina nyingine za kansa kuhusiana na curcumin kwa sasa bado zipo njiani.
10. Inazuia Ugonjwa wa Alzheimer's
Ugonjwa wa Alzheimer's (Alzheimer's disease au Senile dementia) ni ugonjwa unaoendelea ambao unaharibu kumbukumbu na kazi nyingine za akili. Vinavyounganisha seli za ubongo na seli zenyewe zinadumaa na kufa, hatimaye kuharibu kumbukumbu na kazi nyingine muhimu za akili.
Kama ilivyo na nguvu kubwa ya kuondosha sumu, binzari inaweza kuamsha kazi za ubongo na kuzuia matatizo ya utambuzi, ambayo mara nyingi huja kwenye namna ya Alzheimer's na dementia.
Tafiti iliyofanywa na Srikant Mishra kutoka 'Departmentbof Neurology, Plummer Street, Sepulveda, CA, curcumin ina uwezo mkubwa wa kusafisha au kuondoa protini iitwayo amyloid kwenye mishipa ya damu, ambayo kiashiria kikuu cha muendelezo wa ugonjwa wa Alzheimer. [7] Jaribio lingine lililofanyika pia limegundua kwamba virutubisho mbadala vyenye binzari huimarisha hali mwili na uwezo wa utambuzi kwa watu wenye umri mkubwa wasio na matatizo kumbukumbu.
Faida Nyingine
Faida nyingine za binzari na curcumin ni kama zifuatazo:
Huzuia homa ya Uti wa Mgongo na hupunguza maumivu
Virutubisho mbadala vyenye binzari (Turmeric supplements) mara nyingi hushauriwa vitumike kwa kupunguza maumivu uti wa mgongo, gout, na maumivu ya misuli yaliyotokana na mazoezi au ajali. Utumiaji wa mara kwa mara wa binzari unaweza kutibu tatizo. Curcumin pia husaidia kwenye kupunguza matatizo yanayopelekea kuzeeka kama atherosclerosis, kulingana na tafiti iliyochapwa kwenye jarida la 'Immunity and Ageing. [8]
Hutibu Msongo wa Mawazo
Curcumin kiukweli ni kitu muhimu sana, na tafiti zimeweza hata kujaribu athari zake kwenye kudhibiti homoni ndani mwili.Tafiti zimeonyesha kwamba curcumin ina athari sawa na Prozac kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo, hali ya mwili kulegalega, wasiwasi, na stress. Hii inaifanya kuwa mbadala wenye nguvu kwa madawa ya hospitali, ambayo mara nyingi yana hatari ya au athari mbaya baada ya kutumia.
Huchelewesha Uzee
Curcumin iliyopo kwenye binzari, ikiwa na viondosha sumu vingine, hushambulia dalili au alama za uzee kama mikunjo na mabaka kwa kuzuia ukuaji wa sumu huru (free radicals)
Hutibu Kisukari
Curcumin kwenye poda ya binzari kinasaidia kushusha kiwango cha sukari ya damu na kuzuia hatari ya kisukari type-1 na type-2 .
-Hutibu matatizo yatokanayo na Hedhi
- Hutibu Fibrosis
Matumizi
-Binzari hutumika kwenye mapishi na hata urembo vilevile.
Matumizi ya Urembo
Juisi ya binzari yawezekana ikawa ndio maarufu kwa matumizi ya dawa, lakini yaweza kuchanganywa vitu vingine na cream. Mafuta yaliyotokana na binzari ni wakala mzuri wa afya.
- Kung'arisha Meno: wakati ikfahamika kwa kuacha madoa ya njano kwenye nguo, inashangaza kuweza kung'arisha meno ikichanhanywa na mafuta ya nazi na baking soda.
- Sabuni: binzari yenye sifa ya kuzuia uvimbe na kung'arisha ngozi hutumika kwenye sabuni za asili.
- Tiba ya ngozi iliyoathirika na miale ya jua: Unaweza kuichanganya na maziwa mtindi au aloe vera gel kwa kupunguza makali ngozi iliyoungua na miale ya jua.
- Majeraha: Dawa ya meno yenye binzari ndani yake inaweza kutibu majeraha ya kujikata na vitu vyenye ncha kali.
- Face Mask: Binzari imekuwa ikitumika kwenye kufanya face mask toka zama za zamani kutokana na kuboresha ngozi na kuzuia harara. Inaweza kuchanganywa na maziwa mtindi, asali, aloe vera, au vitamin E.
- Skin Moisturizer: ngacc Binzari iliyochanganywa na mafuta mzeituni (olive oil) au mafuta ya nazi (coconut oil) hutengeneza ngozi ya asili yenye kuvitia, ngozi hubakia na unyevu bila kukauka mara kwa mara.
Matumizi ya Mapishi
Binzari pia ni kiungo maarufu kwenye supu, sauces, curries, msosi wa nyama, maandalizi wa mchele, na hutumika kama kiungo chenye kuleta ladha kwenye chakula kwa zaidi ya dazani ya vyakula vingine vya kitamaduni.
- Smoothies: Unaweza kuiongeza kwenye smoothies kwani huipa ladha tamu kwa namna ya kipekee, Ladha flani hivi kama 'pina colada' pamoja na faida za kiafya juu yake.
- Maziwa: Maziwa ya moto yaliyochanganywa na binzari (kijiko cha chai) inasaidia kupata nafuu kutokana na homa, baridi, na hufanya kazi kama sedative (-enye kukufanya usinzie, u-relax, utulie) ya asili.
- Chai: Changanya binzari (kijiko cha chai) na maji ya moto kufanya chai. Chai hii inatoa faida za kiafya na pia inahakikisha upo na ngozi yenye kung'aa.
Madhara
Ijapokuwa si kitu kilichozoeleka kusababisha allergy, binzari inaweza kuleta madhara kwenye mwili, hasa ukiitumia kwenye kiwango kikubwa. Madhara hayo ni kama yafuatayo:
- Kichefuchefu
- Kizunguzungu
- Kuhara
Kwenye baadhi ya kesi, matumizi yaliyopitiliza ya curcumin kwenye kiwango cha dawa yamesababisha mapigo ya moyo kupiga tofauti. Pia, inaweza kuzolotesha kuganda kwa damu kwa kuongeza athari za dawa zinazozuia damu kuganda. Kwa maana hiyo, watu wenye shida ya kuganda kwa damu au wenye kutumia dawa za kufanya damu kuwa nyepesi ni lazima kuepuka binzari. Mara zote ongea na wataalamu kabla ya kuongeza kitu hiki chenye nguvu kwenye diet yako, na kumbuka --kila kitu kinatakiwa kichukuliwe kwa wastani!
Makala hii ni copy & paste ya makala hii
Reference: Ingia hapa kwenye makala halisi kwa lugha ya kiingereza.
Nimejaribu kutafsiri kwa faida ya wale wengi wenye ulewa kidogo na lugha ya kiingereza na wala si kwa ajili ya kupata faida.
- Ripoti wizi au makosa uliyoyaona baada ya kusoma.
Asante
Nimependa some hili. Nitakuwa Barozi wa Binaries hii.
JibuFutaBinzari, sio Binaries.
JibuFuta