Mtama ni nini?
Mtama au Sorghum kwa lugha ya kiingereza, ni neno pana kwani aina nyingi za mtama ambazo asili yake ni maeneo ya kitropiki na nusu tropiki duniani kote. Wakati kukiwa na zaidi ya aina 30 tofauti za aina ya mtama, aina moja tu ndio huvunwa kwa matumizi ya binadamu, wakati aina nyingine zilizobaki hutumika kama malisho kwa wanyama.
Aina muhimu ya Mtama kwa binadamu, Sorghum bicolor, asili yake ni bara la Afrika, mtama umekuwa ukitumika uzalishaji wa sorghum molasses, sorghum syrup na pia kama nafaka. Pia, inaweza kutumika kwenye uzalishwaji wa vinywaji vya pombe na hata bio-fuels duniani kote.
[Note ninapoandika kiingereza baadhi ya maneno, kwa maana yangekuwa kwa kiswahili wengi hawataelewa, kuna muda lugha yetu inakuwa ngeni kuliko hata lugha ngeni yenyewe].
Inatambulika kwa upana kama zao la tano muhimu sana la nafaka duniani.
Uwezo wa mtama kuweza kuuandaa kwa namna tofauti, ukiongeza na ukweli kwamba unakubalika na watu wenye allergy na ngano kuula, unaufanya kuwa zao muhimu sana duniani. Zaidi, faida nyingi za kiafya zinazokwenda sambamba na mtama zinaufanya kuwa mbadala mzuri juu ya aina nyingine za nafaka zinazoliwa duniani.
Virutubisho vilivyomo kwenye Mtama
Kulingana na USDA, Mtama ni kalakana ya uzalishaji tunapokuja kwenye suala la virutubisho. Ikiongezwa kwenye diet, inaweza kutoa vitamin kama niacin, riboflavin, na thiamin, vilevile pia kiwango kikubwa cha magnesium, iron (madini joto), shaba (copper), calcium, phosphorus, na potassium, na karibia nusu ya protini inayohitajika kwa siku na nyuzi lishe (dietary fiber) muhimu zinazotakiwa.
Faida za kiafya za mtama
Faida za kiafya za mtama kutemeana na mahusiano umeng'enyaji hazihesabiki. Husaidia kutibu magonjwa mengi vilevile. Embu tujadili kwa undani kidogo.
1. Huboresha Afya ya Umeng'enyaji Chakula
Mtama ni moja ya chakula bora zaidi kwa dietary fiber. Kikombe kimoja kilichojaa punje za mtama kina gramu 12.9 za dietary fiber, ikiwa na maana kwamba njia yako ya umeng'enyaji itafanya chakula chako kupita bila shida, kuzuia kufungamana njiani, kutopata choo, maumivu ya tumbo, gesi kuzidi, na kuharisha.
Zaidi, kiasi cha nyuzi lishe (dietary fiber) kinachozidi kwenye mwili husaidia kukwangua na kuondoa cholesterol hatari (LDL), ambayo huboreaha afya ya moyo na kuulinda mwili wako na dalili za atherosclerosis, mshutuko wa moyo, na kiharusi.
2. Inaweza kusaidia kuzuia Kansa
Utafiti uliofanyika 2018 na watafiti wa kimarekani ulipendekeza kwamba mtama wenye utajiri wa polyphenol unaweza kuwa na kizuia-kansa na ushaihidi wa kisayansi unahitajika. [1] Utafiti mwingine ulichapishwa kwenye jarida la 'PLoS One' unaelezea kwamba mtama unatabia ya kiashiria cha kuzuia ukuaji wa kansa na kizuia uvimbe (anti-tumor) na inaweza kuzuia kansa muendelezo wa kansa kama vile kansa ya titi. [2] Pia vilevile ina athari za kuzuia shida ya njia ya chakula.
Tafiti nyingine iliyofanyika kwa mnyama iliyoongozwa na watafiti kutoka Brazil uligundua kwamba kutokana na uwepo wa 3-deoxy anthocyanidins na tannins inaweza kutoa sifa za kuzuia kansa. [3]
Utafiti ulioongozwa na Dr. Joseph M. Awika kutoka 'Soil and Crop Science Department, Texas A&M University', uligundua kwamba ganda la nje la punje za mtama lina viondosha sumu, anthrocyanins, ambavyo havipatikani kwenye vyakula vya aina vingi. [4] Viondosha sumu hivi vimeunganika moja kwa moja kwenye kupunguza aina kadhaa za kansa, ikiwemo kansa ya koo, ukilinganisha na watu wanaokula mahindi na ngano mara kwa mara.
Viondosha sumu ni kampaundi zenye faida ambazo huzima na kuondoa kabisa sumu huru (free radicals) kwenye mwili, ambazo mara nyingi husababisha seli zenye afya kwenye mwili kubadilika na kuwa seli za kansa.
3. Hudhibiti Ugonjwa wa Kansa
Utumiaji uliokithiri wa carbohydrate huvunjwavunjwa kwenda kuwa sukari nyepesi na kusababisha uharibifu makubwa kwenye kiwango cha glucose kwenye mwili, kupelekea mtu kupata Kisukari, au kusababisha mtafaruku kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari tayari. [5] Hatahivyo, ganda la nje lenye utajiri wa tannin lina enzymes zinazozuia mwili kuingiza starch, amabyo inaweza kusaidia kudhibiti kiwango cha insulin na glucose kwenye mwili. Kwa maana hiyo basi, wenye ugonjwa wa kisukari hawatapata shida za hapa na pale katika kiwango cha glucose yao.
4. Hupunguza Allergy ya Gluten
Ugonjwa wa Celiac ni allergy inayotokea kipindi vyakula vyenye asili kuvutika kama ngano vikiliwa. Kinga ya mwili hujaribu kupambana pindi 'gluten' inapoliwa na kusababisha kuharibika kwa utumbo mdogo. Gluten inapatikana kwenye maelfu ya vyakula vya kawaida, na kufanya hali kuwa ngumu mno kwa wale wenye ugonjwa wa celiac. Kwa bahati nzuri, jarida la 'Clinical Nutrition' lilichapisha utafiti uliofanywa kwa pamoja, ambapo liliangazia kwamba nafaka mbadala kama mtama, zinaweza kuliwa kwa usalama na wale wanaosumbuliwa na tatizo hilo linalozidi kuongezeka, bila maumivu ya uvimbe, kichefuchefu, na uharibifu wa utumbo unaosababishwa na gluten.
5. Huimarisha Afya ya Mifupa
Magnesium ipo katika viwango vya juu sana kwenye mtama, ina maanisha kiwango chako cha Calcium kitakuwa kimedhibitiwa, kwani magnesium huongeza uingizwaji wa calcium kwenye mwili. Madini haya mawili pia ni muhimu kwenye maendeleo ya tishu za mifupa na kuharakisha kupona kwa mfupa ulioharibika au mifupa iliyozeeka. Hii huweza kuzuia hali kama osteoporosis na homa ya uti wa mgongo, kukufanya kuwa imara na mwenye afya kwenye umri wako wa uzee.
6. Huongeza Mzunguko wa Damu
Kama tafiti iliyochapwa kwenye jarida la
'Science of The Total Environment', madini kama copper, iron (madin joto), zinc, magnesium, na calcium yanapatikana kwenye mtama. [6] Uwepo wa copper husaidia uingizwaji wa iron (madini joto) kwenye mwili. Hii inamaanisha uwezekano wa kupunguza kasi ya ugonjwa wa anemia, ambayo ni jina lingine la upungufu wa madini joto. Kukiwa na madini ya kutosha ya copper na iron kwenye mfumo, chembe hai nyekundu za damu huongezeka, hali hiyo huongeza mzunguko wa damu, kuongeza ukuaji wa seli na kurekebisha seli zilizoharibika, na kuongezeka ukuaji wa nywele, wakati kipindi hiko pia huongeza kiwango cha nishati kwenye mwili.
7. Huzidisha kiwango cha Nishati
Kulingana na tafiti iliyofanywa na 'Department of Nutritional Sciences', chuo kikuu cha California, mtama una niacin. [7] Niacin pia hufahamika kama vitamin B3, ambayo ndiyo funguo kuu ya kubadilisha chakula kuwa nishati inayotumika kwa mwili kwa kuvunjavunja na kutumia virutubisho kuwa nishati.
Neno la Tahadhari
Hakuna maelezo yanayofahamika kuhusu kutotumia mtama kwenye diet yako.
Kama ilivyo, kuna uwezekano wa baadhi ya watu kuwa na allergy na mtama, lakini kesi za mtama kuleta allergy ni nadra mno.
Zaidi, kwa matumizi ya kiwango kikubwa ya madini ya aina fulani na vitamin, hatari pekee iliyokuwepo ni kutumia kitu kizuri kupitiliza, kwahiyo kula mtama kwa wastani na faidi faida zote nzuri za kiafya.
Mbona nasikia chakula ya mtama inafunga choose yaan kupata choo no shida na inakuwa ngumu kutokaunjikamua sana
JibuFutaAsante kwa somo
JibuFuta